Leo tarehe 15 April, Wahariri, Meneja na Wamiliki wa vyombo vya Habari wameshiriki katika mafunzo ya siku mbili yanayohusu masuala ya Haki ya Afya ya Uzazi kwa wanawake na wasichana kwa lengo la kuongeza uhamasishaji na elimu kwa jamii juu ya masuala haya muhimu.
USHAURI WANGU KWA VIJANA WENZANGU
...
Kwenye maisha usitegemee watu wote wakupende au wakuzungumzie vizuri, wapo walioambiwa uongo mwingi kuhusu wewe na wakaamini. Ila usikate tamaa ya kuishi, Mola wako yupo pamoja na wewe 🙏🏽
..
#SautiYaVijana#MtotoWaMkweziNaMkulima#KaziNaUtu
Ahsanteni nyote kwa salamu za kheri, umoja na upendo katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.
Nchi yetu imepiga hatua kubwa katika kuufikia usawa wa kijinsia ikiwa ni sehemu ya kazi ya kujenga Tanzania jumuishi yenye ustawi, haki na isiyo na ubaguzi kwa sababu zozote zile ziwe za kidini, kikanda, kiitikadi au kijinsia.
Siku hii pia ni fursa kwetu kutathmini mafanikio makubwa tunayoendelea kuyapata katika sekta mbalimbali, yanayohakikisha kila msichana na mwanamke anapata nafasi ya kufikia ndoto zake. Mafanikio haya ni pamoja na hatua kubwa tuliyopiga katika sekta ya elimu na sekta ya afya, ambazo zimeweka msingi imara na mwanzo madhubuti katika safari yetu ya mafanikio.
Katika muendelezo wa kuwanoa waandishi wa habari kuandika habari za masuala ya haki ya afya ya uzazi, TAMWA ZNZ imetoa mafunzo ya siku mbili kwa waandishi wa habari 27 wa Unguja ili kuongeza uchechemuzi na kuongeza elimu ya masuala haya katika jamii.
#SRHR
Kumeshakucha ni wakati Sasa kuendelea na majukumu ya ujenzi wa kitaifa bila kusahau ni wakati wa kujiandaa, wanawake kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ili kufikia azma ya 50/50.
Mkurugenzi wa Miradi na Ushirikiano wa Taasisi inayosimamia elimu bora kwa Watoto wa kike nchini(CAMFED) Ana Sawaki amesema kuna umuhimu wa kuwawezesha wasichana kielimu na kiuchumi ili kuwasaidia kutimiza ndoto zao na kuwaepusha na ndoa za utotoni. @IEQC @TenMet@camfed#IEQC
Licha ya kuwa sehemu ya mabadiliko na utetezi wa haki za binadamu kwa muda mrefu, waandishi wa habari bado wana jukumu la kufanya kazi kwa umoja kuwezesha upatikanaji wa sheria mpya ya Huduma za Habari Zanzibar.
#ZAMECO2024
Husahauliki #MaalimSeif. Alama ya Upendo, Umoja na Amani. Hazina ya Hekima, Busara na Uvumilivu. Vazi la Ubinadamu, Utu na Uungwana. Kiongozi thabiti uliyekuwa na msimamo na kusimamia ulichokiamini. Leo tunakumbuka siku uliyozaliwa tukimuomba Allah Ajaalie Pepo yawe makaazi yako.