#TaifaKwanza#KataaVurugu
Hongera Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kushiriki jukwaa la uchumi la 29 la St. Petersburg nchini Urusi. Aidha hongera kwa kuzindua jukwaa la uchumi la Tanzania na Urusi kwa ajili ya kuratibu ushirikiano wa kibiashara kati ya Tanzania na Urusi. Wanaharakati Uchwara wamekosa hoja za maana kufuatia kazi nzuri ya Rais wetu. Tumewapuuza Wanaharakati uchwara na washirika wao.
#HakiNaWajibu
๐Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Makamu wa Rais Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi pamoja na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM)Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere tarehe 06 Juni, 2026 baada ya kuhitimisha Ziara yake ya Kitaifa, St. Petersburg nchini Urusi tarehe 05 Juni, 2026 kufuatia mwaliko wa Rais wa Nchi hiyo Mhe. Vladmir Putinโ๏ธ๐น๐ฟ
Rais Samia Suluhu Hassan amerejea salama nyumbani Tanzania kutoka katika ziara ya kihistoria Urusi na kupokelewa na Makamu wa Rais Dkt. Emmanuel Nchimbi, Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama, Katibu Mkuu wa Chama cha Mapindunzi Dkt. Asha rose Migiro, pamoja na wananchi wa Tanzania.
Ni vile tu wanaharakati wamekosa akili ya kufikiria mambo kwa mapana ila kwa kweli mambo anayofanya VP walitakiwa wajitasmin sana juu ya kauli zao zisizo miguu wala kichwa
Rais karejea Tanzania salama usalmin baada ya ziara yake ya siku3 Nchi RUSSIA
#KAZIENDELEE
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (JWTZ), Jenerali Jacob Mkunda, amesema Taifa imara halijengwi na Watu wanaojihusisha na vitendo vya utapeli, ugomvi, uhalifu na uvunjifu wa sheria, huku akisisitiza kuwa maendeleo ya Nchi yanategemea uwepo wa Wananchi wenye maadili mema.
Jenerali Mkunda ametoa kauli hiyo leo Juni 5, 2026 wakati wa uzinduzi wa jengo la ghorofa la kusomea Wanafunzi katika Shule ya Sekondari Makongo, Jijini Dar es salaam ambapo amesema Vijana wanapaswa kupewa elimu bora itakayowajengea uwezo wa kuwa raia wema na kuchangia maendeleo ya Taifa badala ya kujiingiza katika vitendo vinavyohatarisha usalama na ustawi wa Jamii.
โJengeni moyo wa kizalendo wa kuhakikisha Taifa letu linaloelekea kuwa huru, imara na kuheshimika kwa miaka elfu ijayo,โamesema Jenereli Mkunda.
#MillardAyoUPDATES
Kuna watu walisema atakamatwa akamatwe na nani? Gen z munajiongopea kwa siasa za chuki na uchwara.
Karibu Tena nyumbani kwako Mh Raisi Dr Samia suluhu Hassan the president of united republic of Tanzania hakika una energy ya kutosha MUNGU akupe zaidi na zaidi neema kubwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Makamu wa Rais Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi pamoja na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM)Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere tarehe 06 Juni, 2026 baada ya kuhitimisha Ziara yake ya Kitaifa, St. Petersburg nchini Urusi tarehe 05 Juni, 2026 kufuatia mwaliko wa Rais wa Nchi hiyo Mhe. Vladmir Putin.
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Kenani Kihongosi amewataka baadhi ya Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakutane naye ili wabishane kwa hoja.
Akizungumza leo Juni 5, 2026 Jijini Arusha, Kihongosi amemtaka Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche, Mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Nyanza, Joseph Mbilinyi โSuguโ, Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Godbless Lema na Mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Pwani, Boniface Jacob wakutane ili wabishane kwa hoja.
โSisi wengine ukitutukana tunatabasamu tunasikia raha, mwambie mwenzio raha, matusi yamewahi kuua? Waje hapa, mimi namtaka Heche, Lema aje hapa na Boni Yai na yule Sugu wa Mbeya akae hapa halafu wote wawepo hao mimi niwe peke yangu wao wanne.โAmesema Kihongosi.
#MillardAyoUPDATES
MPINA NI MPUMBAVU...
Kuna muda unajiuliza Tanzania iliwezaje kuwa na watu wa aina hii na wakaachwa kuwa watunga sheria kwa muda mrefu sana.. Yaani huyu ni mtu aliyetaka kabisa kugombea urais wa Tanzania na hizi ndiyo akili zake..
Kwa kweli aliyeweka pingamizi huyu pumbunda asigombee alilisaidia sana hili taifa na aliliokoa na ujinga mwingi sana ambao tungeenda kukutana nao kwenye kampeni zake.. Yaani kusikiliza tu ujinga wake kungetosha kulifanya hili taifa liuugue sana.
MPINA anaongelea watu 518 kwa kuwa kwake wahuni wale waliokuwa wanachoma moto mali za watu na mali za umma za mabilioni ya shilingi ni muhimu kuliko hasara waliyoisababishia kwa watu binafsi na serikali..
MPINA anaongelea watu 518 lakini haongelei hasara na uharibifu uliofanywa na wahuni wale na vibaka wale waliokuwa wanajiita wanaandamanaji wakati ni wezi na vikaba waliokuwa wanataka kupindua serikali na walioharibu mali za watu kwa kiasi kikubwa sana.
MPINA anaona watu 518 wana faida sana kuliko mali za watu zilizoharibiwa! Anaona walikuwa na haki kuharibu mali za watu na mali za umma lakini hana uthubutu wa kuongelea madhara waliyosababisha..
UNAPOKUWA na watu kama MPINA kwenye taifa na wakajiingiza kwenye siasa ni hasara sana kwa kuwa ni kuwa na watu wapumbavu kwenye mifumo ya kisiasa na watu wa hivi ni sumu sana kwa ustawi wa taifa.
HUWEZI kuwa na akili timamu ukaongelea uhai wa vibaka waliokuw wanakata vidole watu kwa kuwa walipiga kura. Huwezi kuwa na akili timamu ukawa unatetea watu waliochomo moto mwendokasi na vituo vyake.. Huwezi kuwa na akili timamu ukawa unawatetea vibaka waliochoma vituo vya mafuta na kupora mali za watu
Wale walikuwa CRIMINALS na walishughulikia kama CRIMINALS msituletee ujinga hapa.. Kama mnapenda sana kuongelea haki za watu kuna sehemu nyingi nendeni Lebanon na Gaza mkaongelee kile kinachofanyika huko ๐
#KigogoMediaUpdates
ZIARA YA MH RAIS SAMIA URUSI NA "GEOPOLITICAL DIPLOMATIC SHIFT" YA DUNIA.
George Michael Uledi.
June 2,2026.06:54AM.
Baada ya Serikali ya Tz jana kutangaza kuwa Mh Rais Samia Suluhu Hassan kesho June 3,2026 anaanza ziara ya siku mbili Nchini Urusi ilinifurahisha sana.
Hii inaweza kuwa ni ziara bora zaidi na ya kimkakati sana tangu Mh Rais Samia Suluhu Hassan aingie Ikulu baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.Hii ziara ya Nchini Urusi ya Mh Rais Samia,kwangu mimi ni zaidi ya ziara.
Ziara hii imenipa nafasi ya kuja na neno lingine jipya kwenye mawanda mapana ya mahusiano ya kimataifa-mkakati yaani "GEOPOLITICAL DEPLOMACY".Kwenye mfumo huu mpya ambao wajuzi wa mahusiano ya kimataifa Mkakati wanatakiwa kuwafundisha Wanafunzi wao huko Vyuoni ni kwamba๐๐ฝ๐๐ฝ๐๐ฝ
Kuna mambo Makuu kama Matatu hivi kwa mtazamo wangu Mimi "a state has to achieve" katika siasa mKakati za kimataifa za kisasa ambayo ni (I)Strategic Alliance to consolidate nation's powers(II)Alliance for Resource share na tatu (III)while defending National Security and Sovereignity.
Ziara ya Mh Rais Nchini Urusi inakwenda "kuioffer"Nchi yangu Tanzania mambo yote matatu kwa pamoja na hii ndio MIMI nimeipa jina leo kuwa ni aina mpya ya diplomasia ya dunia ambayo ni lazima(TZ) unakubali kuwa hauwezi kuwa na (I)Maadui wote na hauwezi kuwa na (II)Marafiki wote ndani ya dunia hii.
IPO HIVI๐๐ฝ๐๐ฝ
Katika aina hii mpya ya Diplomasia ya dunia ni kwamba,kwa maoni yangu inaigawa dunia katika mafungu makuu matatu ya kimkakati;(I)Alliance ya CHINA URUSI na wafuasi wao(II)Marekani na Ulaya na washirika wao na (III)Mashariki ya kati na washirika wao.
Katika aina hii ya "Triangle Geopolitical Diplomacy"Nchi za bara la Afrika Tanzania ikiwemo zitalazimika kuchagua strategic wadau ambao wanaweza kulinda kwanza (I)Maslahi yake ya Ulinzi Usalama na Uhuru wake kama Taifa kabla wadau hao hawajalinda(II)maslahi yake ya kiuchumi pekee yake na hii ndio nimeiita "Geepolitical diplomatic shift".
Mfano,Mswada wa Bunge la Senate la Marekani dhidi ya Tanzania unaoendelea kuchakatwa kule Marekani na Wabunge wetu kuupigia kelele sana wiki jana kuwa unaingilia Uhuru wetu kama Nchi ni mfano mzuri wa " Geopolitical alliance" ambayo hailindi maslahi ya ULINZI NA UHURU wa Tanzania ambao kwangu mimi mswada ule ni hatari kwa maslahi mapana ya uhuru wa Taifa langu Tanzania.
Ziara ya Mh Rais Samia Nchini URUSI kwa jicho la Sovereignity Diplomacy una lengo kuu la kulinda Uhuru wa Nchi kwanza then utatupa pia maslahi yetu mengine ya kiuchumi kama Nchi.
Kama Wanaharakati na wana Chadema wanaendelea kudhani kuwa wanaweza "kutumia"Nchi flani flani kubwa huko duniani kutekeleza programu zao za Political Terrorism ndsni ya Tanzania nadhani ziara ya Mh Rais URUSI IMEWAVURUGA๐
Mfano mwingine ni huu mgogoro wa Mkondo bahari wa Hormus pale Iran unaweza kukupa picha kuwa Geopoligical Diplomacy ndio msingi wa kwanza wenye kuweza kulinda maslahi ya Nchi yoyote ile duniani.
Nchi majirani na Iran(Middle East) ziliamua "kumaintain" ALLIANCE na jirani Iran kuliko kuungana kumpiga Tehran na hapa lengo lilikuwa ni kulinda maslahi yao kwanza ya Kiulinzi na Usalama wa kikanda (Geopolitical Security & Soverignity).
HITIMISHO.
Katika mfumo huu mpya wa Mahusiano ya Kimataifa-Mkakati(Geopolitical Diplomacy),Nchi yoyote kwanza inapaswa kulinda UHURU wake kabla ya kulinda Maslahi yake ya kiuchumi.
Planners wa ziara hii ya Mh Rais Samia URUSI wamekuwa na "akili mingi" sana na automatically inazima matishio ya awali dhidi ya Uhuru wa Nchi yangu Tanzania.
Tanzania Kwanza.๐น๐ฟ๐น๐ฟ๐น๐ฟ
#UkweliNaUwajibikaji
#TumeYaUchunguziReport
#TanzaniaYetu
KUONDOKA KWA MCHUNGAJI MSIGWA CCM:NI OCT 29 KWELI?
Moja ya sababu Kuu ambayo Mchungaji Peter Msigwa ameitaja kupelekea kuondoka kwake ndani ya CCM anasema ni matukio ya Oct 29,2025.HAUWEZI kubishana na Mdomo wake lakini ukweli anaujua yeye mwenyewe.
Hata nyakati zile alipokuwa anatoka Chadema kuja CCM mwaka jana baada ya kukosa Cheo cha Mwenyekiti wa Chadema kanda ya Nyasa dhidi ya SUGU,Peter Msigwa tena hakuwa mkweli mbele ya Umma ALIDANGANYA KAMA ANAVYODANGANYA SASA.
Ni miezi kama SABA HIVI TANGU Oct 29,2025 mpaka sasa May 24,2026 lakini Mchungaji Peter Msigwa akaendelea kusikilizia muda wote huu wa miezi saba akiendelea kula mshahara na posho pale Ofisi ya ITIKADI NA UENEZI kwa ndugu yangu KINANI KIHONGOSI.
YAPO MAMBO MAKUBWA MATATU HIVI AMBAYO YANAMUONDOA LEO CHAMA CHA MAPINDUZI.
I.MATARAJIO ya kupata CHEO/UTEUZI ndani ya Chama na Serikali hayapo tena.Hesabu za Mchungaji zilikuwa cleary kabisa kwani aliamini kuwa ujio wake ndani ya CCM ungempa uteuzi kama.ilivyokuws kwa wanachadema wengine ambao walikuja ndani ya Chama na kupata teuzi.
Kumbuka kuwa Msigwa angepata CHEO cha Mwenyekiti wa kanda ya Nyasa asingekuja CCM kamwe kwahiyo Msigwa alikuja CCM kwa hasira na bahati nzuri CCM walilijua hilo.
II.Kuundwa kwa TUME-JINAI kutokana na Matukio ya Oct 29
Kama.una akili nzuri ni rahisi kujua kuwa Msigwa alikuja CCM kwa missions kuu mbili hizi hapa(I)kutafuta Cheo na kuikomoa Chadema lakini bado moyo wake ulikuwa Chadema,CCM walikuwa wanafahamu hilo haswa.
Pili(II)Msigwa alikuja Chadema kufanya UKACHERO wa Kisiasa then badae arudi https://t.co/Ee2leM9OzQ kwamba pamoja na kuwekwa idara ya Uenezi,Msigwa alikuwa chini ya "ukachero" mkubwa wa CCM akisomwa nyendo zake usiku mchana asubuhi.
Mchungaji inawezekana sana alikuwa sehemu ya Mpango wa NO REFORMS NO ELECTION ambao ndio ulizaa matukio ya Oct 29.
Ilibidi atafutwe mtu wa kumwingiza ndani ya mifumo ya CCM kuweza kuratibu mipango hiyo ya Chadema akiwa ndani ya CCM.KUMBUKA TUNDU lissu na Msigwa ni damu damu.Inawezekana sana Tundu Lissu alitaka kumtumia Peter Msigwa kutekeleza waliyotekeleza Oct 29.
USIJE ukashangaa Peter Msigwa akija kutajwa kwenye REPOTI YA TUME JINAI na kutiwa nguvuni mbeleni.Njia pekee sasa ni kuondoka CCM na kwenda kuungana na wana Oct 29 wenzake huko Chadema.
III.Sababu ya Tatu kubwa ni URAFIKI uliopo wa kufa na kuzikana wa ndugu Tundu Lissu na Mchungaji Peter Msigwa ambao unamfanya MSIGWA AJIONE NI MSALITI mbele ya jamaa yake Tundu kwa kuendelea kula mshahara wa CCM pale Dodoma.
Mtarajiio ya Msigwa yalikuwa ni kwamba uenda SERIKALI mbeleni ingemtema(Gerezani) Tundu Lissu baada ya Uchaguzi Mkuu kumalizika lakini anaona Serikali(Mahakama) IMEKAZA.HAINA MCHEZO KABISA NA ISHU YA LISSU.
JAPO watu wengi wanataka kuaminishwa kwamba Tundu Lissu yupo Magereza Ukonga KISIASA lakini ukweli unabaki kuwa jamaa ameshiriki kwa 70% kuratibu yale ya Oct 29 hata akiwa huko huko mahabusu..
Hii sio ishu kabisa kwani hata Muuza madawa ya kulevya wa MeXICO Olechampo aliweza kuratibu biashara zake za kuuza dawa za kulevya hata alipokuwa gerezani na baade akafanikiwa kutoroshwa na kundi lake hatari.
Tundu Lissu ni wazi alikuwa na mkono wake mkubwa tu kwenye Oct 29,niaminini.
Kama mnabisha nadhani tusubilie majibu ya Tume- Jinai,itasema ukweli kuhusu haya nisemayo.
Infact,Oct 29 kulikuwa na elements zote za UHAINI/MAPINDUZI NA BAHATI MBAYA SANA wapo hata wanaccm wanatajwa nao kushiriki kuwezesha matukio yale ya hovyo.
Ila tu cha kushangaza hata report ya Tume JINAI ambayo itakuja na purely ushahidi nayo wataipinga tena kwa nguvu kubwa zaidi.NASUBILIA KUONA WATAWEZAJE KUPINGA FACTS?,HUU ni Uchunguzi wa KIJAJI na sio bla bla tena.
Katika mazingira kama hayo Msigwa anabakije CCM?
TUNAPOSEMA WATU WANAJITEKA MUWE MNAELEWA...
Tumekuwa kila siku tunasema na kuwaambia watu hasa CHADEMA wanatengeneza matukio ya kujiteka mkawa hakuelewi.
Haya leo Waziri Mkuu kawasaidia kuelewa na kuwajulisha nini huwa kinafanyika na wanaotunga michezo ya kujiteka ndani ya nchi hii hasa huko CHADEMA..
Anayejiita msaidizi wa Chiba eti katekwa halafu mtu aliyekuwa naye kwenye gari akapanda bodaboda akaanza kufukuza gari lililomteka baadaye wakaanza kupigwa risasi halafu hakuna aliyejeruhiwa! Hivi nyie watu mbona hamnaga akili kiasi hiki? Sawa tunajua ni wajinga lakini mbona kama mmezidisha ujinga sasa.!
Naye mtekwaji eti karuka toka kwenye buti ya gari mpaka vitu vya kati na kufungua mlango na kuingia porini ๐๐ akajikuta suruwali imenasa kwenye miiba ghafla kaibuka kavaa kanga na pingu zimemkamata kweli kweli ikabidi aende polisi kuomba afungukiwe pingu!.. mwandishi wenu wa hizi script ni mjinga sana.
Nadhani leo mmeeleweshwa nani anafanya hii michezo na huwa inafanywa kwa lengo gani na kwa wakati gani!..
UFIPA tafuteni mbinu mpya hii ya kujiteka kuuwa watu wenu ilishafeli toka wakati wa Chacha Wangwe๐
#KigogoMediaUpdates