Mtuacheni tuichangie Chadema acheni wivu maneno ya mwananchi.
CHANGIA SASA
M-Pesa
Namba: 0744446969
Jina: CHADEMA HQ
NMB Bank
Namba ya Akaunti: 22606600140
Jina la Akaunti: Chama cha Demokrasia na Maendeleo
Agenda ya kufunika wizi mkubwa kwenye sketa ya mafuta.. Watanzania msikubali.
Tunataka kujua kwanini Vitol ametuuzia mafuta kwa usd 260 sawa sh 689,000.
Wakati huo huo anawauzia Uganda mafuta hayo hayo kwa USD 83 sawa na sh 212,000
Msumbiji usd 90 sawa na 238,500.
Hawa watu wanaoitwa NAMARO na TPDC wamehusikaje kwenye huu ufisadi wa kufilisi Nchi.
Huu ni uhujumu uchumi mkubwa kuwahi kutokea katika Nchi hii.
Kuna zaidi ya 1.2 trilioni imeibiwa katika mafuta.
Katibu mkuu wa Nishati bwana Mataragio alisema tuna mafuta ya kutumia miezi mitatu.
Watanzania tusikubali huu wizi.
#TANZANIA: CHADEMA, ACT WAZALENDO, KATAMBI, IGP WASHITAKIWA, WAKILI AFUNGUKA
Wakili Msomi, Jebra Kambole leo Julai 16, 2026 akizungumza na Wanahabari amesema Waziri wa Mambo ya Nadani, Patrobas Katambi ameshitakiwa kutokana na tamko lake la kufungia mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa alilolitoa bungeni kwa kile kilichoelezwa kuwa kuna tishio la usalama, wakati huo huo wakiwaruhusu klabu za Yanga na Simba kufanya mikusanyiko mikubwa huku viongozi wengine wa serikali wakiendelea na mikutano, jambo hilo amelitafsiri kuwa ni uvunjifu wa katiba.
Aidha, Wakili Jebra amesema wamewashitaki chama cha CHADEMA pamoja na chama cha ACT Wazalendo kwa sababu wanataka wakaieleze mahakama namna walivyoathirika na zuio hilo.
Zaidi: https://t.co/VnfpkMMDdt
TAARIFA MBAYA
Usiku wa leo, majira ya saa kumi, watu wanne waliokuwa na silaha za moto na vifaa vinavyodaiwa kutumika kuvunja mlango, huku wakiwa wameficha nyuso zao kwa vitambaa na bila kujitambulisha, wanaripotiwa kuvamia nyumbani kwa Katibu wa Wilaya ya Shinyanga wa BAVICHA, Alfred Masanja, na kuondoka naye.
Hadi sasa, haijafahamika alipelekwa wapi wala ni akina nani waliohusika na tukio hilo.
Tunafuatilia kwa karibu taarifa za tukio hili na tutatoa taarifa kamili leo Asubuhi
Jackson Mnyawami
Katibu wa Kanda ya Serengeti
VIDEO:
Katibu wa Shurah ya Maimamu Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda ameungana na wote 'wanaopiga kelele' kuhusiana na kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa Tundu Lissu, akitoa rai kwa muhimili wa Mahakama kuharakisha uendeshaji wa kesi hiyo ili haki iweze kutendeka
Sambamba na hilo, Sheikh Ponda amegusia kile alichodai kuwa ni kudorora kwa hali ya kisiasa Nchini akitoa wito kwa mamlaka za kiserikali na wadau wengine husika kuhakikisha wanairejesha nchi kwenye misingi ya 'kutabasamu'
Sheikh Ponda amezungumza hayo alipokuwa kwenye mahojiano maalum na Mwanahalisi Digital, ambapo kupitia mahojiano hayo masuala mbalimbali amegusia ikiwemo mchakato wa maridhiano uliofikiwa Zanzibar ukihusisha vyama vya CCM na ACT Wazalendo
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche amesema hatetereki kwa maneno au propaganda zinazoelekezwa kwake, akisisitiza kuwa mashambulizi hayo hayawezi kubadili msimamo wake.
Akizungumza leo Julai 15, 2026 nyumbani kwake Tarime, Mkoani Mara alipokuwa akiongea na Wanawake wa BAWACHA waliomtembelea kumfariji kufuatia kifo cha dereva wake, Suez Dani Maradufu, Heche amesema anayeshambuliwa ni yule mwenye ushawishi.
“Mchezaji mwenye mpira ndiye anakabwa, mnayoyaona mashambulizi dhidi yangu ni kwa sababu mpira uko hapa, hivyo msiwe na wasiwasi, sina muda wa kujibizana na Mtu, huwezi kuniyumbisha kwa maneno ya mtaani, ya kwenye khanga? Mimi nasonga mbele,” amesema Heche.
#MillardAyoUDATES
Aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Nigeria, Dkt. Benson Bana, amesema hayo kwenye mahojiano ya njia ya Simu yaliyorushwa Julai 15, 2026 na Saut Digital.
Fuatilia zaidi https://t.co/T7ylDFpYyk
#JamiiForums#Demokrasia#Sheria#Utawala
#TANZANIA: WATANZANIA WAWAUNGE MKONO JUMUIYA YA MADOLA ILI KULIEPUSHA TAIFA LETU NA UTAWALA USIOZINGATIA HAKI ZA BINADAMU - DKT. LWAITAMA
Dkt. Azaveli Lwaitama, mshauri wa masuala ya siasa leo Julai 16, 2026 akizungumza na Wanahabari amewataka Wanzania wote wenye kupenda haki na Demokrasia kuiunga mkono Jumuiya ya Madola iliyotoa tamko la kuitaka serikali kufuata misingi ya demokrasia katika utawala wake na kwa kuanza waanze na kumuachia huru Tundu Lissu na kuhakikisha serikali inafuata utawala wa sheria.
Aidha, Dkt. Lwaitama amesema Jumuiya ya Madola ina lengo la kuliepusha taifa juu ya utawala usiofuata haki za binadamu.
Zaidi: https://t.co/lHqBMW22UG
ASANTENI WATANZANIA! MPAKA ASUBUHI HII TUMEFIKISHA TSH. MILIONI 53.5 ✌️
Safari inaendelea.
CHANGIA SASA
M-Pesa
Namba: 0744446969
Jina: CHADEMA HQ
NMB Bank
Namba ya Akaunti: 22606600140
Jina la Akaunti: Chama cha Demokrasia na Maendeleo
100%. Hatuwezi kusapoti Chadema kwa maneno tu, lazma tutoe pesa.
Ngoja niwaambie kitu Watanzania, Chadema kukosa pesa ndio moja ya sababu kuu CCM wanawapata watu wa kufanya hizi press za kumchafua Heche.
Watanzania, hatutafika popote kama Chadema haina pesa .
Ni aibu kubwa sana nchi inayolilia haki leo ni siku ya 3 tumekusanya 50 million tu, ni aibu. Mtu ananunua bando ili aingie insta asome umbea wa nani kaachana na nani? Hizo buku 5 za bando la kufatilia umbea si ungetuma Chadema?
Reality is bila Chadema kuwa na pesa hakuna msaada mkubwa wataweza kutupa…….. Watu wanatupigania ila hata kuwasapoti na kufanikisha kazi zao kwa kutoa pesa tunashindwa??? Hii haki tunayoidai itakuja kimiujiza bila pesa kuwepo za kufanya movement ????
Kama unakubaliana na nilichosema basi, kabla huja Like hii posti, kabla hujareposti, kabla huja comment kabla hujamforwadia mtu hii link tuma pesa kwenye hii number.
vodacom: 0744 446969
Jina: Chadema HQ
Kingine nna swali kwa Chadema hawa wanachama wenu mamilioni, mna namba zao simu? Yani mna database ya wanachama. Je mnatuma messages kwa wanachama kuwakumbusha kuchangia? Mimi personally hapa Marekani huwa nasumbuliwa na message za chama mpaka natuma mwenyewe pesa. Maana message inakuja na link kabisa ya kutuma pesa, tena wanani address kwa jina.
‼️TUMENASA MAZUNGUMZO YA MADALALI WA PROJECT YA KUMSHAMBULIA MHE. HECHE‼️
Huyu anaitwa Shaban Mikongoro ni mpambe wa Susan Kiwanga na ni Kiongozi wa CHAUMA Mkoa wa Morogoro.
Hii Sauti inayosikika hapa ni majibizano kati ya Mikongoro na Kiongozi wa BAWACHA Kanda ya Kati ambapo Mikongoro anasikika akimshawishi Kiongozi huyo akubali kufanya press ya kumtukana Mhe. @HecheJohn kwa ahadi ya ujira wa milioni moja.😂😂😂
Nduli Idd Amin Mama na mwanae Abdul wanachezea kodi zetu kwa kuliipa hawa vibaraka wao ili wamshambulie Mhe. Heche kwasababu hataki kuimba wimbo wa Maridhiano.
Sikiliza mazungumzo haya kwa makini mwanzo hadi mwisho ili uone hawa vibaraka wa CCM walivo na akili ndogo.🚮
Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Mwanza, Mhashamu Renatus Nkwande amewataka Watanzania hususani vijana kujenga taifa kwa misingi ya unyenyekevu, uadilifu na haki badala ya kutumia nguvu au ubabe, akisema hiyo ndiyo njia sahihi ya kuleta ukombozi wa kweli wa nchi.
Askofu Nkwande amesema hayo wakati akihubiri katika Adhimisho la Misa Takatifu ya kumbukumbu ya Mtakatifu Agustino wa Hippo, mlinzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino Tanzania (SAUT) kilichofanyika jijini Mwanza.
Akizungumza na waumini na wanafunzi waliohudhuria ibada hiyo amesema vijana ndio tegemeo la taifa hivyo wanapaswa kujenga maadili na kuwa mstari wa mbele katika kusimamia haki na ukweli.
"Vijana daima huwa ni tegemeo la popote pale mkikosa uadilifu ulimwengu na nchi yetu hatujui itaishia wapi? Fuatilieni na myaelewe yote yanayotokea lakini muweke mikakati ya kweli na ya kuja kukomboa nchi yetu, hatuwezi kuikomboa nchi yetu kwa nguvu kwa sababu hata Bwana Yesu Kristo wakati anawakomboa wana wa Israel hakutumia nguvu," amesema Askofu Nkwande
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Falsafa na Maadili chuoni hapo, Padre Innocent Sanga amewataka vijana kuyaiga na kuyaishi maisha ya mtakatifu Agustino huku wakiamini kuwa wanaweza kubadilisha mienendo yao mibaya kuwa mizuri.
ASANTENI WATANZANIA!
TUMEFIKISHA TSH. MILIONI 50 ✌️
Ndani ya saa 96 sawa na siku 4.
Asanteni kwa mwitikio wenu mkubwa. Mpaka sasa, tumefanikiwa kukusanya TSh. Milioni 50 katika Marathon ya kufikia TSh. Milioni 334 kwa ajili ya kufanikisha Baraza Kuu la Umma.
Huu ni ushahidi kwamba Watanzania wanaweza. Safari inaendelea. Kila mchango una thamani. Tuendelee kuchangia hadi tufikie lengo letu la TSh. Milioni 334.