Mnakumbuka mnavyo tutesa, ndivyo mtakavyo teseka, mnaona mlivyo tudharau , ndivyo mtakavyo dharauliana, mnakumbuka mnavyo tuweka jela kwa ushahidi na kesi za uongo , ndivyo mtakavyo pelekana magereza, mnajua tunavyoishi kwa hofu ? sasa ni zamu yenu.
Mnakumbuka mlivyoteka na kuua watu , sasa ile mbegu imeota kwenu. Hali yenu itakuwa mbaya sana, kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti. Bahati mbaya Nchi pia inaharibika.
Leo 29 Mei 2026, ni siku 212 zimepita tangu damu ya watanzania wasio na hatia imwagike kwa risasi za moto 29 Oktoba 2025. Serikali ya CCM inaweza kudhani labda muda umefuta machozi yetu, na ndio maana wanacheka na kupongezana badala ya kuwajibishana. Lakini wamefeli. Jeraha hili liko hai, na mioyo ya wananchi haitasahau kamwe. Hatupigani kwa nguvu zetu wenyewe; tunasimama na haki thabiti ya Mungu ambayo haijawahi kushindwa. Jasho na damu ya raia wenzetu inaililia dunia, na amini nawaambia, dhoruba ya haki inakuja. Kila mkono uliomwaga damu utawajibika. Dunia imesimama nasi, na sauti ya wanyonge haitanyamazishwa tena! #MO29
Samia anatuona sisi ni wapumbavu kama yeye kwamba tangu Oktoba 29, hakuna aliyeshitakiwa kutokana na mauwajivya kihistoria; aliyejiuzulu au kuwajibika kisiasa!
Kibri hiki tunakiona; acha tuone kitamfikisha wapi.
RIP to the Fallen Heroes! Tutawakumbuka daima!
Umeshawahi kukutana na binadamu ambaye amemwaga damu za watu na hajutii kabisa matendo aliyofanya?
Ndo huyu shetani sasa.
Yaani, anashangilia tu, ni kama aliua Panya wasumbufu shambani kwake Kizimkazi huko kumbe ni damu za watoto wa wanawake wenzake zinalia aridhini.
Ila, Mungu yupo.
Tundu Lissu ni mzalendo anayepigania Tanzania anayoamini. Wanaofurahia au kusimamia kuendelea kwake kuwa gerezani wajue kuwa mamlaka ni ya muda, lakini hukumu ya historia ni ya milele. #FreeTunduLissu
Leo imetimia miezi saba tangu Nduli Idd Amin Mama auwe kwa risasi Watanganyika zaidi ya elfu kumi.
Tunamuomba Mungu aendelee kuwapa pumzika la milele mashujaa wetu wote.🙏💔
Hili nalo ni kosa ambalo natuhumiwa kulifanya kwa mujibu wa Msajili. Sasa narudia tena kusisitiza, ofisi za Serikali si duka la wazazi wenu wala mali ya familia zenu. Mkipewa mamlaka ya umma, mnapaswa kuvumilia kukosolewa, kuulizwa maswali na kuwajibika kwa maamuzi yenu. Kama hamtaki kusemwa, kuhojiwa au kuwajibika, acheni hizo ofisi mrudi mkakae na wake zenu, waume zenu na familia zenu. Mamlaka si kinga dhidi ya uwajibikaji. Na hili linamhusu kila mmoja wenu, hususani pia na wewe Msajili
Ni muhimu kumtaja Samia Suluhu kama mwandishi mkuu wa mauwaji ya tangu Okt 29.
(W)amekiri mara kadhaa kuwa aliamuru majeshi kuuwa ili kulinda urais wake batili.
Mauwaji yale yasingefanywa bila sanction yake, na amesikika akijivunia suala hilo!
Lazima awajibike! #MO29
Shangazi @MariaSTsehai nimeona leo nikupe MAUA yako. Najua utamaduni wetu unatufunza kumpa mtu maua yake akifa, kitu ambacho si kizuri. Mi napenda ku celebrates watu wakifanya vizuri. Nimejijengea hiyo culture.
Unafanya kazi kubwa sana, unaipenda sana nchi yako, unalipa gharama kubwa juu ya haya mapambano. Mashangazi wengi tulikuwa nao humu, wameyaaga mashindano. But you're still here, madame. Una kila sababu ya kuweza kuendelea na mishe zako. Given that you're an African woman, family responsibilities etc zingeweza kukufanya useme sina muda. Lakini uko hapa, kueleimisha, kuencourage, kushawishi na kupambana. Hata pale ulipokuwa so down, kwa kusemwa, kutukanwa, kupigwa propaganda na kusingiziwa. Ulisimama kidete kuendelea mbele, na kufocus. Na zuri zaidi, in the mid of that unaweza hata ku encourage wengine 😭. Maombi yangu, ni Mungu akutunze na kizazi chako, uone na kufarahia matunda ya unachokipigania. Amen.
Pokea maua yako, Shangazi
@AbroadTanzania Na maccm yamekaa kimya. Kinachoniumiza zaidi ni sisi UMMA million 65 tumekaa kimya pamoja na jeshi la Wananchi. Mungu hawezi kutusamehe
@AbroadTanzania Kunawatu waliniumasana kupotea kwao, Polepole alikuwa nyumbani akachukuliwa na Mdude alikuwa nyumbani akachukuliwa mbele ya mke wake, halafu kunamijitu unasema imeheal the national ya nyoko.
Hakuna kosa Kubwa alifanya Polepole Kama kutoa siri akiwa nchini alafu alikuwa kagusia kurasa 5 tu kati ya 38 alizokuwa anatakiwa kuweka wazi! Alitakiwa awe nje ya Tanzania,
Kuna mengi sana
Abdul,
Pengine mengi yanayosemwa mitandaoni na mitaani dhidi yako si ya kweli. Lakini ikiwa hata asilimia ndogo tu ya yanayosemwa yana ukweli ndani yake, nakusihi uyatafakari kwa makini na kuchukua hatua mapema.
Historia inatufundisha kuwa wale wanaoshangilia na kupiga makofi juu yetu leo wanaweza kuwa mashahidi wa kwanza kesho mambo yanapobadilika. Nguvu, umaarufu na ushawishi ni vitu vya muda, havidumu milele.
Kumbuka pia kwamba nafasi na mamlaka ya wazazi wetu si ya milele, na wewe bado una safari ndefu sana mbele yako kama kijana. Hekima kubwa ni kujenga heshima, uadilifu na jina jema mapema kabla ya mazingira kubadilika.
Mungu huchelewa wakati mwingine, lakini haki yake haipotei. Ikiwa kuna jambo lolote lisilo sahihi, kurekebisha njia mapema ni busara kuliko kusubiri wakati ambao marekebisho yatakuwa magumu zaidi.
Huu ni ukumbusho wa KIMUNGU, kwa nia njema. Sijui hata kwa nini nimeandika. Lakini kesho huwa inafika.
Baada ya CHADEMA kujibu barua ya kwanza ya MSAJILI wa VYAMA vya SIASA katika barua ya majibu ya kurasa 29, MSAJILI (aliyeongezewa mkataba wa kusalia ofisini baada ya kustaafu) ameshindwa kujishikilia, ametuandikia barua nyingine ametupa siku 10 za kujieleza kwanini CHADEMA isifutiwe USAJILI au kutozwa FAINI. Huu ni mwendelezo wa mbinu MUFILISI za DOLA KATILI ya CCM kupitia VIBARAKA wao. Tunamueleza Msajili: Asithubutu kutingisha dishi lililokaa tenge. NGUVU ya UMMA haizuiliki. #PeoplesPower ✊🏾
CHADEMA Youth Council (@bavicha_taifa) is a seedbed of leaders in Tanzania.
It's great to see the council gathering for its constitutional meeting despite the hostile political environment in the country.
Ofcourse, classy is our tradition!