#TajiriLaKihaya
Wewe Kijana ulieajiriwa;
Achana na kufanya fadhila kwa kampuni yako, fanya kile unacholipwa na uende nyumbani.
Unapofanya kazi kwa kampuni kwa masaa 8, usiende nyumbani uangalie TV au Kucheza Game au kushinda mtandaoni…
fikiria kuanzisha biashara ili familia yako iweze kurithi,
Hawawezi Rithi kazi yako.
Kujifunza hakuishi…
“Much love, my friend—I miss you deeply. You are still one of the finest brains this country has. I’m keeping you in my prayers—may God give you the courage, strength, and resilience to rise above every challenge before you.���
As expected, this “commission” glossed over a violent crackdown and the facts. I support the administration’s bilateral review and call for sustained pressure on Tanzania, including the release of Tundu Lissu. Waiting out scrutiny with a whitewashed report is a flawed strategy; it won’t restore credibility but rather deepens long-term risk and mistrust of the ruling regime.
Kwa kweli Bongo Zozo Sisi Watanzania hatuna cha kukulipa ila tunaona juhudi zako za kusimama katika ukweli na haki, Mungu azidi kukutunza na kukufungulia milango ya mafanikio.🫡
Tume ya Jaji Chande: katika miaka 2 (2023-2025) Watanzania 245 walitekwa na hawajapatikana. Hii ni sawa na watu 2 kutekwa na kupotea kila wiki. Hali mbaya, ya kuumiza na kutia hasira sana.
Utaridhiana vipi na watu ambao njia yao ya kujadiliana ni kutekana tu?
Jana niliandika ujumbe nikikosoa kitendo cha Mzee MBOWE kumuombea msamaha SABAYA. Nimepata maoni mengi; wengine wakisema sikuwa sawa.
Ipo hivi. Kuna mambo katika siasa hayawezi kufutwa na maneno laini na mepesi ya “msamaha,” hususani msamaha usiotoka kwa mtenda dhambi mwenyewe.
Utawala wa SABAYA katika wilaya ya Hai haukuwa wa kisiasa tu; ulikuwa ni utawala wa chuma na ukatili uliopitiliza. Hata Mzee MBOWE anafahamu hilo.
Makosa ya uhujumu uchumi na unyang’anyi wa kutumia silaha (armed robbery) yaliyomfunga gerezani wakati ule, ni tone dogo sana katika bahari ya unyama wake.
Wapo watu walitekwa, kuteswa, na kuachwa na vilema vya kudumu. Kusema mtu huyu anastahili msamaha bila toba ya dhati kwa wahanga, si tu ni kosa, ni dhihaka.
Miongoni mwa wahanga wa genge la SABAYA ni ndugu yetu Simon MNYAMPANDA, aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Hai. Ndugu yetu aliteswa.
Simon Mnyampanda aliteswa kwa umeme. Ameeleza wazi kwamba, alihojiwa kuhusu mahusiano yake na Mzee MBOWE. Mwisho, alipigwa misumari ya miguu.
Huyu ni mtu aliyepata mateso hayo akimlinda Mzee MBOWE na CHADEMA. Leo Mzee MBOWE anajigeuza kadinali na kumuombea msamaha mtesaji SABAYA?
Genge hilo halikuishia hapo. Genge hilo lilikuwa kama MAHARAMIA. Walivamia nyumbani kwa mgombea udiwani wa kata ya Narumu katika jimbo la Hai.
Baada ya kumkosa, walitoa adhabu ya kinyama kwa watu waliokuwepo nyumbami kwa kuwakata masikio na sehemu nyingine. Nyumba nzima ilitapakaa damu.
Hawa ni binadamu, si takwimu za kisiasa. Hawa watu waliotendewa mambo hayo wapo. Baadhi ya ushahidi wa masuala hayo nimeambatanisha katika makala hii.
Inasikitisha kuona Mzee Mbowe anatumia mateso ya wafuasi wake kama mtaji wa kisiasa (political capital). Binafsi nimejiuliza maswali mengi tangu hiyo jana.
Je, wahanga wameombwa msamaha na kufidiwa? Je, mateso yao yamekuwa ngazi ya makubaliano ya kisiasa? Hii si dharau kwa wale walioteswa wakikupigania?
Sabaya anapaswa kuomba msamaha kwa waathirika, si kuombewa. Vinginevyo, hii ni michezo ya kumtengenezea mazingira ya kupata uteuzi katika Serikali ya CCM.
Watu wa Hai hawajasahau. Damu na machozi ya wahanga bado vinadai haki. Msamaha bila toba ni baraka kwa ukatili mwingine ujao. Haki kwanza, msamaha baadaye.
Binafsi, nilimheshimu Mzee Mbowe kiasi cha kumpa mwanangu wa tatu jina la “Freeman”. Leo hii, nahisi usaliti mkubwa moyoni mwangu kwa mambo hayo.
Kunyamaza mbele ya usaliti huu si busara, bali ni upumbavu ambao kesho utatunyong’onyesha. Nimeandika ili kulinda hadhi ya jina la mwanangu.
Siku mtoto wangu akiniuliza, nitamjibu kwa utimamu kabisa. “Nilitetea maana halisi ya ‘Freeman’ wakati jina hilo lilipotaka kuchafuliwa na siasa za kimaslahi.”
Je, wale waliopoteza viungo vyao vya mwili? Waliokatwa masikio? Waliogongwa misumari miguuni? Waliofanya ukatili wa kutisha kama kulawitiwa wakati wakimtetea Mzee MBOWE akiwa mbunge wa HAI, wamepewa faraja au kuombwa msamaha? Wengine walilazimika kutelekeza familia zao na kuwa wakimbizi kwa kuhofia usalama wao. Hali hii inajenga picha kuwa Mzee MBOWE ameweka maslahi yake binafsi mbele na kusahau gharama kubwa waliyolipa wafuasi wake. Hii ni dhihaka kwa watu wote ambao waliwahi kuamini katika njia zake. Hii inatuogopesha ambao tumewahi kumpambania hadharani. Hata hivyo, SABAYA anatakiwa kuomba msamaha mwenyewe, siyo kuombewa msamaha. Kimsingi, msamaha ni jambo la kibinafsi na la kimaadili kati ya mtu aliyekosea na yule aliyekosewa. Msamaha wa kweli unahitaji sauti ya mkosaji mwenyewe.
Hizi ni kodi na ushuru wa serikali kwa gari ndogo tu Crowne.
Fikiria kijana ambae ameanza maisha hapa Dar, kutokana na adha ya usafiri anajibana ananunua kagari ka usd 6,000 ambazo ni sawa na 14 m.
Hiyo gari ikifika inatozwa ushuru mwingine wa 14 m, yaani fikiria ushuru unalingana na ununuzi wa gari!!!
Yaani gari Machuma yote, engineering iliyopo pale kwenye gari unanunua bei sawa na ushuru wa mtu ambae amekaa ofisini tu na anakuchaji hela yote hiyo!!!!
Wakati mwingine kodi zinakua bei juu kuliko manunuzi!!!!
Huyu kijana awe mkulima au mfanyakazi, anafanya kazi ngumu sana kupata hiyo fedha, then inachukuliwa hivi…
Alafu baada ya mda CAG anasoma ripoti kwamba uwanja ulitakiwa kujengwa kwa bilioni 187 baadae ukajengwa kwa bilioni 337..
Mara umekaa unaambiwa kuna eti Waziri anatumia gari binafsi ya bilioni 2, unajiuliza mtumishi wa umma ametoa wapi bilioni 2 kununua gari na mshahara wake unafahamika, au anamiliki nyumba tano za thamani ya bilioni tatu, nne au tano… aniliki mashamba ya mabilioni, amempa mama mkwe wake nyumba ya bilioni tano na gari la kutembelea la milioni 500.
Pesa zote hizi za mlipa kodi anaeumizwa kiasi hiki na mzigo wa kodi…
Hapa nimesema magari tu, Ukienda kwenye kila kitu kinachoingizwa na kutoka Nchini ni mzigo wa kodi na maumivu kwa Mwananchi..
Na mwisho wa siku badala hizi fedha zitumike kwaajili ya maendeleo yetu zinaishia kwenye mifuko ya vibaka.
Hakuna barabara, hakuna maji, hakuna umeme.. Maisha magumu , mishahara duni hasa kwa walimu na manesi.
Hatuwezi kukubali kuwa watumishi wa vibaka wanaopora mali za umma.
Dunia ya sasa watu wana taarifa mkononi…
Mazungumzo yoyote unayofanya na Watanzania ujue sio wajinga, watafuatilia na wataringanisha taarifa hizo.
Watanzania wa sasa sio wa mwaka 47.
Nasema kwa uhakika hakuna mahali popote duniani mafuta yamefika 8,000 usd wala 6,000 Euro kwa lita.
Hakuna popote mafuta yanauzwa 400usd wala 600 Euro duniani.
USD 100 ni sawa na 260,000 Kwahiyo usd 400 ni sawa na 1,040,000.
Euro 600 ni sawa na 1,820,000
Kama ni 6,000 ni sawa na sh
18,200,000=
Kama ni usd 8,000 ni sawa na milioni 20.8 .
Lita moja ya mafuta Marekani inategemeana na state na state.
Kwa mfano Washington DC area kwa gallon 1 ambayo ina lita 3.8 ni usd 3.80 ambayo kwa pesa za Kitanzania ni 9,600, ukigawa kwa lita 3.8 ni sawa 2,526 kwa lita, ambayo hapa sisi kwa Tarime 4,020, kwa hapa Dar ni 3820.
Na kwa Marekani nzima wastani wa gallon moja ni usd 4.10.
Kwahiyo kwa wastani sana ni sh 2,600 za Kitanzania kwa lita.
Marekani ndio wako vitani na wao ndio wana uchumi mkubwa, lakini mafuta Marekani ni rahisi kwa zaidi kwa sh 1500 kwa kila lita tunayonunua huku..
Ukiwa na 10,000 ya Tanzania Marekani utanunua lita 4, na ukiwa ma hiyo hiyo hela hapa Tanzania utanunua lita 2 na point kidogo.
“Jamii inapokwepa mwanga wa kweli, macho yake huzoea giza. Na kila anayeleta mwanga huonekana kama adui, si kwa sababu amekosea, bali kwa sababu amekuja kuvunja utulivu wa uongo uliozoeleka.”
Yaani AIBU naona mimi Mtanganyika kwa kinachoendelea mahakamani kwenye kesi ya kubumba ya Lissu, na hawa mashahidi wa kificho wa kubumba…Ni kama wameokota vichaa barabarani , ni AIBU TUPU!
NB: Aliyewapa huu mchongo wa hii kesi kawaingiza chaka bovu, na pamoja na mashtaka mengine atashitakiwa kwa UHUJUMU UCHUMI, kesi hii ni ubadhirifu mkubwa wa fedha za umma. MATAKO YAKE!
Usiogope wala kuyumba moyo, kwa maana waliokuweka jela wana mashaka makubwa kuliko wewe. Wewe una dhamira, wao wana hofu, wewe una msimamo wa haki wao wana wasiwasi. Ukweli haufungwi kwa minyororo, na haki haizimiwi kwa kuta za gereza. Endelea kusimama imara, kwa sababu unachokisimamia ni kikubwa kuliko hofu zao. Unapaswa kuwa na familia yako lakini huko jela kwa ajili ya watu na Nchi. Kusudi jema sana hili. Hauoni ujumbe huu lakini angalau ndugu na watoto wako wataona na kupata nguvu wakati wakitafakari.
Religious freedom is a fundamental American value. Today, CDA Lentz convened interfaith leaders in Dar es Salaam to discuss shared values of religious freedom, inter-faith peace, and mutual respect.
Wabunge kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Joseph Musukuma wa Jimbo la Geita na Mhandisi Kija Ntemi wa Jimbo la Katoro wamesema Mwekezaji anayetuhumiwa kubomoa bila kibali majengo ya Serikali katika Kitongoji cha Katoro Center anatakiwa kuchukuliwa hatua.
Wabunge hao wamewasilisha malalamiko yao baada ya Kamati ya Uchumi na Fedha ya Halmashauri kutembelea eneo hilo linalolalamikiwa ambapo kulitokea mvutano kati ya mtu aliyejitambulisha kuwa Mwekezaji na Musukuma.
Zaidi tembelea JamiiForums.
#JamiiForums #JFMatukio #JFUwajibikaji #Governance
Video: Daily News Digital
Hii ni jana mbunge wa mchongo Joseph Msukuma kamchapa kibao muwekezaji.
Soon wauwaji wote watachanganyikiwa maana damu za Watanganyika zaidi ya elfu kumi hazitawaacha salama.