Bwana, nakushukuru kwa kunipa asubuhi nyingine.
Kabla sijaanza kuhofia mambo ya leo, nisaidie kukumbuka kuwa wewe tayari upo nami.
Nipe nguvu kwa ajili ya mambo ninayopaswa kufanya.
Nipe uvumilivu kwa watu nitakaokutana nao.
Nikinge nisipoteze muda wangu kwa mambo yasiyo na mana.
Maombi ya asubuhi ni njia ya kumkaribisha Mungu katika mambo yote yaliyo mbele yetu. Mkabidhi yeye mahangaiko yako, omba hekima na umshukuru kwa siku nyingine. Huenda yasifanye siku hiyo kuwa rahisi, lakini yanakukumbusha kuwa huhitaji kuikabili peke yako.
Isaya 54:17
“Kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa; na kila ulimi utakaoshindana nawe katika hukumu utauhukumu. Hii ndiyo urithi wa watumishi wa Bwana, na haki yao inayotoka kwangu mimi, asema Bwana.”
Mpe taarifa mwenza wako mara kwa mara. Hii si sheria, bali ni lugha ya upendo. Haipaswi kwa mwenza wako kukisia mahali ulipo au kujiuliza unafanya nini. Kumpa taarifa si kitendo cha kutaka kumdhibiti.
Ni ishara ya upendo. Inamaanisha:
"Una umuhimu. Nataka uelewe hivyo."
Na unapoomba usiku wa leo, weka mbele za Mungu yale ambayo huwezi kuyatatua.
Majibu usiyo nayo, milango isiyofunguka na yaweke mikononi mwa Mungu.
Lala ukijua kuwa Mungu halali kamwe, na ukumbuke kwamba kwa kuwa rehema zake ni mpya kila asubuhi, kesho itakuwa siku njema zaidi.
Kuna mtu aliniambia nisome 𝐙𝐚𝐛𝐮𝐫𝐢 𝐲𝐚 𝟐𝟑 ninapoamka na 𝐙𝐚𝐛𝐮𝐫𝐢 𝐲𝐚 𝟗𝟏 kabla ya kulala. Kwa kweli, utaratibu huo mdogo umeleta mabadiliko makubwa sana kwangu. Kuanza siku na Mungu na kuimaliza pamoja naye ni jambo la kipekee sana.
2 Mambo ya Nyakati 7:14
“Ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekeza, na kuomba, na kuutafuta uso wangu, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, nami nitasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.”
2 Mambo ya Nyakati 20:12
“Ee Mungu wetu, je! Hutawahukumu? Kwa maana sisi hatuna uwezo wa kukabiliana na jeshi hili kubwa linalokuja juu yetu; wala hatujui tufanye nini, lakini macho yetu yako kwako.”
BWANA ni jabali langu, na boma langu, na mwokozi wangu, Mungu wangu, mwamba wangu ninayemkimbilia, Ngao yangu, na pembe ya wokovu wangu, na ngome yangu.
[Zab 18:2 SUV]
Ninakuombea katika mwezi huu mpya ili Mungu arejeshe afya yako na kuponya majeraha yako—kiroho, kifedha, katika ndoa—na kwenye nyanja yoyote ya maisha ambayo haikuenda vizuri ianze kwenda vizuri katika jina la Yesu. Heri ya mwezi mpya!
Bila shaka, mwezi huu utakuwa mwema kwako!
Karibu mwezi wa tisa, Septemba! Mwezi huu ukakamilishe mema yote ambayo Mungu ameanza maishani mwako. Maombi yako yakapate majibu, matumaini yako yakafanywe upya na muda wako wa kusubiri ukageuke kuwa ushuhuda wa furaha. Bwana akubariki, akuongoze na kukupa sababu za kushukuru.