@InnocentJLS Elimu Form 4 failure atakuw na jambo gani la msingi la kuzungumz na akalitekeleza kama sio ujinga tu. @01MWANASHERIA na boss wao form 4 failure @SuluhuSamia ni wanaropoka tu
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Heche, amesema awamu ya pili ya kampeni ya uhamasishaji wa Tonetone imeendelea leo kwa kufanya ziara ya mtaa kwa mtaa, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kukamilisha lengo la kukusanya shilingi milioni 334.
Kwa mujibu wa Heche, mwitikio wa wananchi umekuwa mkubwa, huku wengi wakijitokeza kuchangia papo kwa hapo katika maeneo yaliyofikiwa na viongozi wa chama.
Akizungumza kupitia ujumbe wake aliouchapisha leo Jumanne, Julai 28, 2026, Heche alisema:
"Awamu ya pili ya kuhamasisha Tonetone leo tumeingia mtaa kwa mtaa kuhamasisha uchangiaji ili kukamilisha milioni 334. Kila tulikopita wananchi wametupokea kwa furaha na kuchangia papo kwa hapo." Amesema.
Aidha, amewahimiza wanachama, wafuasi na wananchi kuendelea kuchangia Chadema kupitia njia mbalimbali za malipo.
"Tuendelee kuchangia chama kwa namba M-Pesa: Namba 0744446969, Jina: CHADEMA HQ. NMB Bank, Namba ya Akaunti: 22606600140, Jina la Akaunti: Chama cha Demokrasia na Maendeleo."
CHADEMA inaendelea na kampeni hiyo ya Tonetone ikiwa ni sehemu ya jitihada za kukusanya fedha za kuendesha shughuli za chama kupitia michango ya wanachama, wafuasi na wadau wake.
Haya ndio mavazi rasmi ya MARATHON kote Duniani.
Ukiona kuna mtu alienda DODOMA kwenye MARATHON na alivaa CHUPI ama TAITI na juu akavaaa SHARTI ama TISHERT ama JERSEY huyo hakwenda MARATHON alienda kwenye MRADI wa MaCCM
KATAENI miradi ya kihuni ya CCM
Mwandishi mkongwe wa habari na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile, amesema kauli ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, kuhusu umuhimu wa Watanzania kupata Katiba Mpya, imeonyesha ujasiri wa kisiasa na uzalendo, akisisitiza kuwa "huyu ndiye Nchimbi ninayemjua, hutamka lililo bora kwa taifa."
Balile ametoa kauli hiyo katika makala yake iliyochapishwa leo Jumanne, Julai 28, 2026, akieleza kuwa kauli ya Dkt. Nchimbi inapaswa kuungwa mkono kwa hoja kwa kuwa inalenga kujenga misingi imara ya utawala bora na maendeleo ya taifa.
"Ndiye Dkt. Nchimbi nimjuaye. Anatamka lililo bora kwa taifa, si kwa masilahi yake binafsi. Taifa linapopata Katiba nzuri, halijengi tu sheria ya leo; linajenga kinga ya haki, amani, demokrasia na maendeleo kwa vizazi vijavyo," ameandika Balile.
Katika makala hiyo, Balile amerejea hotuba ya Makamu wa Rais aliyotoa wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 15 wa Mwaka wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), uliofanyika Julai 24, 2026, katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Balile, Dkt. Nchimbi alisema iwapo angepewa nafasi ya kutoa ujumbe mmoja tu kwa Watanzania, angesema: "Pambaneni mpate Katiba Mpya."
Balile amesema Makamu wa Rais alisisitiza kuwa Katiba ndiyo sheria mama na kwamba kupatikana kwa Katiba Mpya yenye misingi bora kutasaidia kuondoa changamoto zinazotokana na sheria nyingine zinazokwenda kinyume na haki na misingi ya utawala bora.
Aidha, amesema Dkt. Nchimbi alikumbusha kuwa mchakato wa Katiba Mpya umekuwa ukizungumzwa kwa zaidi ya miaka 40 na kwamba jitihada zilizowahi kuanzishwa na Serikali ya Awamu ya Nne zilikwama, hivyo kuna umuhimu wa kuufufua na kuukamilisha.
Balile pia amegusia pongezi zilizotolewa na Askofu Dkt. Benson Bagonza kwa kauli ya Makamu wa Rais, akieleza kuwa ni jambo la kupongezwa viongozi wanapopewa sifa wanapozungumza mambo yenye masilahi ya taifa, kama ambavyo hukosolewa wanapokosea.
Katika uchambuzi wake, Balile amesema Katiba Mpya si ajenda ya chama cha siasa wala kundi fulani, bali ni ajenda ya Watanzania wote kwa kuwa ndiyo msingi wa sheria zote za nchi.
Amenukuu Ibara ya 64(5) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inayotamka kuwa Katiba ndiyo sheria kuu ya nchi na kwamba sheria yoyote inayokiuka masharti yake huwa batili kwa kiwango cha ukiukwaji huo.
Kwa mujibu wa Balile, Katiba Mpya inaweza kuimarisha ulinzi wa haki za binadamu, utawala wa sheria, uwajibikaji wa viongozi, mgawanyo wa madaraka, uhuru wa taasisi pamoja na uchaguzi unaoaminika.
Amesema faida kubwa ya Katiba imara ni kwamba hulinda taifa dhidi ya kutegemea ubora au udhaifu wa viongozi binafsi, kwa kuweka kanuni zinazopaswa kuheshimiwa na kila anayeshika madaraka.
Balile amebainisha kuwa Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akisisitiza dhamira ya kukamilisha mchakato wa Katiba Mpya, huku Ilani ya CCM ya mwaka 2025–2030 pia ikiahidi kuhuisha na kukamilisha mchakato huo.
Amehitimisha kwa kuwataka Watanzania kuendelea kudai Katiba Mpya kwa njia za kikatiba, kupitia majadiliano na maridhiano, huku akihoji ni nani anayekwamisha utekelezaji wa ahadi hiyo wakati viongozi wakuu wa nchi na chama tawala wameonyesha kuunga mkono mchakato huo.
"Muda umefika nchi yetu ipate Katiba Mpya. Rais anaipenda Katiba Mpya, Ilani ya CCM imeahidi Katiba Mpya, viongozi wengi wanaitaka Katiba Mpya. Swali linabaki moja; nani anayekwamisha Katiba Mpya isije?" amehoji Balile.
Leo Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, Mhe. @HecheJohn, ametembelea Kijiwe Maarufu cha Mbao, Sabasaba jijini Mwanza na kuzungumza na wananchi, huku akihamasisha uchangiaji wa Tone kwa Tone. Baada ya hapo ameendelea na ziara yake kuelekea Mwaro wa Kirumba, Ilemela.
Hebu fikiria hizo media zote zinataka umbea tu ila ikitokea mambo ya maana ya kuhoji kama media zinaigia mitini hili taifa letu ila umbea ruksa chochote sijui tuna taifa ngani leo wanajazana kujua mtu ana ukimwi