Nikisikia hizi habari za watu kutekwa najisikia vibaya sana. Watu zaidi ya saba mnakwenda kumteka kijana asiyekuwa hatari kwa usalama wa nchi nyumbani kwao mbele ya familia yake? Mnaelewa kweli trauma mnayotengeneza kwa hizi familia? Mnajua chuki mnayoipandikiza kwa jamii? Watu waliomteka Damour Nyakairo, @Ninja_Damour muachieni huko mafichoni aendelee na maisha yake. Hatutaki kuona kijana mwingine anatekwa na kupotezwa. Hatuwezi wote kufikiri na kuwaza sawa. Taifa letu litajengwa kwa msigano wa mawazo. #FreeNinjaDamour
Kitendo cha Magereza na Mahakama kumpeleka Mwenyekiti wetu mahakamani bila taarifa ya mawakili wa chama na chama ni aibu na kutia mashaka sana .
Tumezuiliwa kumuona kiongozi wetu kwa miezi Karibia sita kinyume cha sheria..
Sasa anapelekwa mahakamani kwa siri na kificho nia yenu ni ipi?
Lissu ni kiongozi wa umma haiwezekani kumfanyia mambo ya ajabu kama haya.
Kwa yeyote amjuae huyu mama au ana mawasiliano yake au watu wa karibu wanaoweza kumpata naomba utusaidie. Mtoto wake aliuawa October 29, mama alihudhuria graduation ya mtoto na hiyo picha. Wapo wanaopendezwa kumjulia hali na kusaidia na kuwa wanae wapya. Tafadhali Retweet 🙏🏽
@Mwinshehe07 Dalili ya mvua ni Yale madude yanayoelea soma nyakati kwanini kuchoka kuwe Leo andaa mpango wa scania boss hii scania inaelekea mwisho mwsho
@bonifacejoseph_ Pole sana boss najua tunalindwa na Mwenyezi Mungu lkn nakushauri utafute hizo dude ziwe 3 uwe unaweka kwenye mfuko wa nyuma au kale kadogo itakuepeusha na mengi sana kuhusu ajali ajali kwa maderva muda mwingi mpo road nzuri sana hiyo
Tundu A.M Lissu, kiunoni ana risasi ambayo madaktari wameshauri, isiondolewe. Mwili wake una makovu ya risasi na makovu ya visu, oparesheni zaidi ya 22. Mguu wake mmoja ni mfupi kutokana na oparesheni hizo.
Tundu A.M Lissu ni mlemavu wa kudumu sasa kutokana na madhila ambayo amepitishwa na wahuni ambao walipanga njamaa za kumuua ili waendelee kusalia madarakani. Walihofia, akiwa hai, atawasumbua.
Tundu A.M Lissu anatakiwa kuonana na madaktari wake kila anapohudhuria kliniki nchini Belgium. Amezuiwa. Hakuna kliniki. Lakini, TAL akifikishwa Mahakamani ana furaha kuliko watu wengine wote walio huru uraini.
Tundu A.M Lissu amekaa gerezani (mahabusu katika gereza la Keko na gereza la Ukonga, Dar es Salaam) kuanzia alipokamatwa akiwa Mbinga, Songea April 9, 2025 hadi leo April 9, 2026, ni takribani siku 365.
Tangu upande wa mashtaka walipokimbilia Mahakama ya Rufani kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu uliompa ushindi Tundu Lissu ni mwezi sasa umepita, Jaji hajapangwa na tarehe ya shauri haijapangwa…
Viumbe waliomtungia mashtaka ya uongo ya uhaini ili akae gerezani na wakajichagua kwa kishindo na kujitangaza kibabe, wakaingia Serikalini na bungeni, wao wanaanguka na kuondoka kama mshumaa.
Wakati mwingine, Mungu hatumii radi kuwaangamiza watu ambao ni wadhalimu; anatumia tu muda na ustahimilivu wa yule anayeteswa kuwaonyesha kuwa ndiye Mwenye Mamlaka ya mwisho. Takbīr.
@HecheJohn Kwa kifupi tusipangiane furaha ndio maana Kuna mtu akila wali nyama anafurahi ,mwingine akila ugali dagaa anafurahi ,mwingine akila ugali mchicha anafurahi na hata mwngine akinywa maj akalala anafrahi kama ambavy mbuz hula kw kamba Yake na furaha Kila mtu afurahi kwa uref wake