Mapokezi ya JOHN HECHE Shinyanga sio poa Bro.
Hapa watu wanasherekea mengi. Lakini kikubwa ni kwamba wanafurahia CHADEMA ikiongozwa na LISSU akiwa Gerezani na Heche akiwa nje bado wapo imara hawajawasaliti watanzania.
Madai yetu watanzania YANAJULIKA, TUMEKATAA SIASA ZA MASAJI.
Repost 200
@YerickoNyerereT We choko tusaidie kumuuliza bahsha wenu abdul hela za kununuu rolls royce kapata kwenye matairi yapi aliyouza kariakoo akapata hizo hela za rolls royce ,ukishakuja na majibu tutakujibu
Kuna andiko la Aloyce Nyanda kuhoji kwanini CHADEMA hatujaenda kizimkazi kutoa pole kwa SAMIA kufiwa.
Anaandika andiko lake hili la kuonyesha anajali sana na huku anasahau NCHIMBI nae hajaenda kizimkazi kutoa pole kwa SAMIA.
Lissu alikuachia chama HUJAMUANGUSHA.
Lissu alikuweka kama shahidi wake HUJAMUANGUSHA.
Kipindi chote zaidi ya siku 600 umeongoza CHAMA kwa shida sana ila umebaki imara, tunaomba usikate tamaa sisi TUNAKUAMINI shikilia hapo hapo.
HIKI CHAMA NI MPANGO WA MUNGU NA WEWE MAKAMU HECHE NA LISSU NDIO MARUBANI WETU.
TUTAVUKA HAPA NA HAYA YOTE YATABAKI STORY, PIGA KAZI MAKAMU.
Mbogamboga mnaona tunavyopasuana? Sisi hatuna cha ndio mzee. Tulipasua Mbowe tukamstaafisha siasa za udalali. Mimi nikizingua nitakaangwa ipasavyo. No one is above the program. Lissu atatoka jela ila sio kwa kumpigia magoti au kumpakaa rangi Samia muuwaji. Hatutarudi tulikotoka.
Nimeona matusi na sintofahamu nyingi mtandaoni baada ya kuchapisha ujumbe wa kutoa pole kwa Mama Samia, hasa niliponukuu salamu za pole za Mwenyekiti Lissu kutoka gerezani.
Kwa sisi jamii tunaodai kupigania uhuru wa maoni na demokrasia, hili linapaswa kutufikirisha. Kutofautiana kwa hoja hakuhitaji matusi, dhihaka wala chuki.
Lissu amekaa gerezani takribani mwaka mmoja na miezi sita, akikabiliwa na kesi ambayo sisi tunaamini ni ya kisiasa na isiyo na haki. Anafahamu yaliyompata na serikali iliyomweka mahabusu. Lakini alipofahamishwa kuhusu msiba wa mume wa Mama Samia, akiwa mbele ya mahakama, alitoa salamu zake za pole kwa wafiwa mara mbili.
Huu si unyonge. Hii ni hekima, utu na ukomavu wa kiwango cha juu.
Na si mara ya kwanza. Aliwahi pia kumtetea Sabaya katika kesi yake Moshi. Wengi tulishangaa, nami nilishangaa. Lakini nilipomuuliza baadaye, nilielewa kwamba kwake haki haichagui upande.
Hilo ndilo fundisho kubwa tunalopaswa kulibeba. Tunaweza kupinga serikali, kudai haki na kupigania demokrasia bila kujenga harakati zetu juu ya chuki na kisasi.
Lakini kama tunasema tunampenda Lissu, basi pale anaposema ana pumzi ya kuvumilia mateso na kukaa gerezani, sisi tunapaswa kuchukua kauli hiyo kama mwito wa ujasiri, si ruhusa ya kukaa kimya.
Kama tunaamini kesi hii si ya haki, basi viongozi tunanapaswa kuwaongoza wananchi katika hatua za amani, kisheria na kidemokrasia za kudai haki, pengine kwa njia ya maandamano. Sio kwenye keyboard tu na microphone.
Demokrasia inahitaji wananchi wanaothubutu kusimama kwa kile wanachoamini. Na kama siku moja tutapata nafasi ya kuongoza nchi hii, tusije tukarudia makosa tunayoyapinga leo. Lazima tutawala kwa haki, utu na dhamira njema.
Mimi nitasimama kwenye upendo, utu na haki siku zote ktk kazi hii. Anyway , hekima ya Lissu kutoa pole kwa Mama Samia was a top-class thinking. Inaonyesha kwamba hata unapoteseka, unaweza kuchagua utu, hata unapopinga, unaweza kukataa kisasi.
Wakati mwingine Mungu hataki umshinde adui yako kwa chuki, bali kwa upendo, hekima na maisha yenye ushuhuda kwamba uovu wake haukukushinda.
Mimi niko tayari kusimama kwa amani na kwa ujasiri. Katika hatua ya kupigania uhuru wa Lissu kuwa nje ya kuta za gereza na sio kusema ana pumzi ya kukaa jela hata maisha. Tuna watu wengi sana Chama hiki , pumzi yetu itoke mtandaoni , fikeni tu hata mahakamani kwa sasa na huku viongozi wakuu watusaidie kutafakari jambo muhimu la haki , sheria na amani.
“You don’t have to hate those who hurt you. Sometimes the greatest revenge is to rise above them with peace, dignity, and success.”
Thank you !!
Muda huu mahakamani
Wakili Tundu Lissu anamhoji shahidi wake John Heche 🔥👊🏽
Inside the courtroom - Tundu Lissu the advocate questioning his witness John Heche
For transcript in Kiswahili follow @HildaNewton21#FreeTunduLissu