C&p kutoka kwa @ExMayorUbungo MUHIMU SANA hii.🤝
MAMBO 10 YA KUZINGATIA WAKATI WA MAANDAMANO.
Leo ni siku ya mwisho ya maandalizi ya maandamano ya amani jijini Dar es Salaam.
1.Andaa viatu vyako vyepesi kwa mfano raba na epuka aina ya viatu vya mchuchumio au moka.
2.Hakikisha nguo zako ni nyepesi kwa mfano Suruali na T shirt epuka kuvaa vazi zito au nguo nyingi mwilini.
3.Jitahidi uwe japo na chupa ya maji mikononi yatakusaidia Juani
au beba soda aina ya fanta au mirinda kukuongezea nguvu
4.Andaa bango lako lenye Ujumbe maalum wa kufikisha kwa Watawala au beba Kipeperushi au bendera inayoendana na maandamano
5.kwa sababu ya matembezi ya umbali mrefu epuka kubeba mzigo wa aina yoyote kama vile pochi na vitu vinginevyo.
6.kwa sababu ya msongamano mkubwa wa watu,epuka kuvaa vitu vya thamani kama cheni,hereni na kutembea na kiasi kikubwa cha pesa mfukoni.
(simu yako usiache nyumbani ni muhimu sana)
7.Epuka kutumia nguvu kubwa wakati wa maandamano kama vile kukimbia au kurukaruka wakati wa maandamano.
8.Muda wote wa maandamano sikiliza maelekezo ya Viongozi au waratibu wa maandamano kuepuka ajali au kulinda usalama wa watumiaji wengine wa barabara.
Ukiona mtu anatenda uhalifu wakati wa maandamano,mripoti kwa Viongozi haraka sana.(katika msafara wa Mamba kenge hawakosekani)
9.Ukichoka Kutembea au ukihisi dalili ya kuishiwa nguvu usikae kimya waambie Viongozi au waratibu wa maandamano watakupa njia mbadala wa kupumzika katika magari maalum yanayotufuata nyuma ya maandamano.
10.Baada ya Kufika mwisho wa maandamano usiondoke kimya kimya,
wataarifu Viongozi au watu uliokuwa nao kuwa umefika salama na unarudi nyumbani kwako (kuhakikisha wote tunamliza salama)
Imeandaliwa Na
Boniface Jacob
Mwandamanaji mzoefu
Share na wana kila kona ujumbe uwafikie.
Repost 200 za kuanzia.🫡
Haki,Amani na Utulivu katika Taifa itashamiri zaidi pale tutakapotambua kwamba Uhuru tulio nao tuliupata kwa jasho na damu la Babu zetu.
Kamwe hatuna sababu yeyote halali ya kujirudisha Utumwani kwa hiyari
Haki ya Kuishi,Kumiliki Mali na Kulindwa kwa uhai ni Msingi wa Uhuru wetu
Nyie mliopo CCM, TISS, Polisi, JWTZ na vyombo vingine - hivi mmekosa uzalendo na uwezo wa kudadavua na kupigania rasilimali zetu na watu wenu wa Tanganyika?
Leo Zanzibari wana serikali yao na ardhi yao hawezi kugawa Rais wa Muungano - nyie mko bize kupigania Tanganyika ife?
Eti changu changu, chako chetu?!
Nyie mmekaa mnachekelea ardhi ya wamaasai anaigawa @SuluhuSamia anawanyima huduma ndugu zenu wamaasai, ameuza bandari zetu alafu anarudi Zanzibar anatuita MBWA wapumbavu na wenzake wanatucheka na kupiga makofi huko Makunduchi!
Nyie mpo tu mnaimba “Mama! Mama!” 🙄
Mnateka na kupoteza vijana wetu kwa kulinda nini au nani?
Nchi iko kama Afghanistan mmekaa mnatetea uozo huu?
Mababa na mababu zetu walipigania uhuru huu wa wakoloni mweusi?
Mnatia hasira! Hebu kuweni majasiri kama mnavyojitamba mtaani eti chama dume and STAND UP for your country!
Kama vipi Bi Kizimkazi akae kwao, sisi mtuache tupate #KatibaMpya ya serikali tatu - Muungano iwe bare minimum - changu changu, chako chako, chetu chetu!
Ila the centre no longer holds - mambo mkiacha yabumbuluke zaidi we may never pick up the pieces!
#TutaelewanaTu #ChangeTanzania
Waziri wa TAMISEMI hana mamlaka ya kufuta vijiji na Vitongoji nchini. Si Katiba wala sheria zetu zinazompa mamlaka hayo. Pole kwa umma kutokana na taharuki hii ambayo haina msingi wowote wa kisheria. Mahakama itaondoa/ futa Amri hii.
Stay tuned!!
Mainstream media takataka sana. Siku tano ambazo Maasai wamekusanyika na kuamdamana kudai haki zao hawakuwahi kufika hata kuwasikiliza. Leo, media zote za kimkakati zinapeperusha taarifa za Serikali kurudisha huduma Ngorongoro. Kama lipo tatizo nchi hii, ni tasnia ya habari.
Tulipo sipo na Tuendako siko.Tunahitaji muafaka wa Kitaifa kuondoka katika Mkwamo huu.Huu ni wakati wa Hekima na Busara kufanya kazi yake.
Hatuwezi kuendelea kufagilia uchafu chini ya Kapeti na kudanganya dhamiri zetu kwamba Nyumba yetu ni Safi. Ukifuka Moshi jua Pana Moto.
@LuhagaMpina Uhai ni kitu valuable sana, uwe wa mlengo tofaut, uhai ni muhimu sana.
Haki ya kuishi ndio haki yenye thamani kubwa kuliko zote.
Kama mtu aliyepewa wajibu wa kuhakikisha usalama wa maisha ya wananchi ndio anakuwa wakwanza kuhatarisha huyo sio kiongozi.
Atolewe ahukumiwe
Oust her.
Kijana wa miaka 20 Simiyu amekatishwa maisha yake na ndoto zake kikatili na risasi ya polisi. Huku Ngorongoro wanalia, huku askari wanaua watu, huku watu wanabakwa, huku watu wanapotezwa, huku maiti zinaokotwa hovyo kama njugu. IGP na Masauni wanangoja nini ofisini?