@royalmediatz Najiuliza SANA nakosa majibu. Ikiwa Rais wetu aliye madarakani anataka Katiba Mpya na aliridhia ajenda iwekwe kwenye ilani ya CCM kwa kuwa ndilo hitaji la Watanzania wengi kwa mujibu wa utafiti uliofanyika, sasa wananchi tupambane na nani ambaye hataki Katiba Mpya?
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo September 10, 2025
Part 1
Kesi imeanza
Kasimama Wakili Nassoro Katuga anatambulisha Jopo la Mawakili wa Serikali kama kawaida yao.
Wapo mawakili sita wanaiwakilisha Jamhuri.
Katuga anasema mshitakiwa yupo.
Anaulizwa Mhe. Lissu nae anasema yupo tayari.
Majaji kama kawaida wapo wote watatu.
Katibu Mkuu wa Chama pia yupo hapa ameingia.
Kumbukeni leo tuna kesi mbili na ile ya mgawanyo wa mali za CHADEMA
Baadhi ya Mawakili wameanzia huko.
Sasa anasimama Job Mrema Wakili wa serikali.
Job Mrema: Naomba nianze kusema naunga mkono yote aliyosema Nassoro Katuga na naomba niongeze baadhi ya vitu.
Kuhusiana na Presidential Affairs Act kifungu cha 9 kinaelezea utaratibu ambao upande wowote unataka kuwaita mashahidi kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Lakini kifungu cha 9 tulichosema jana kilikuwa cha zamani lakini kwa mabadiliko ya sheria ya sasa sio kifungu cha 9 bali ni cha 10. Kwahiyo tunaomba ieleweke kuwa ni kifungu cha 10 pale kwenye tisa sio.
Kifungu cha 2 cha Sheria hii kinamtaja Rais, Makamu na Waziri Mkuu.
Hivyo kwa utaratibu ulioainishwa kwenye kifungu cha 10 unawazungumzia hawa vipngozi watatu wote.
Mashahidi hao wakihitajika utaratibu wa kufuatwa ni huo hapo.
Naomba nikisome tafadhali.
Anaanza kukisoma hicho kifungu cha 10.
Kingereza fulani cha Uyole 🤣🤣huyu sijui kama ni mchaga kweli.
Kwahiyo tumesema haya ili utaratibu ueleweke.
Compliance ya hiki kifungu haikufanyika. Na mshitakiwa alishauriwa kama anataka hao wawe mashahidi wake atakuja kuomba jambo hilo hapa mahakama kuu.
Mahakama hiyo ndio hii tuliyopo sasa anapaswa kuomba sasa kwasababu ndio inauwezo wa kusikiliza shauri.
Na kimsingi naomba kusisitiza hajaathirika na chchote kwasababu ndio kwanza mahakama inaanza.
Waheshimiwa majaji jambo kubwa tunalofahamu kwamba mahakama hii itajiuliza.
Je pingamizi lililoletwa na mtuhumiwa liko sawasawa mbele ya mahakama hii.
Lakini pia naomba kufanya marejeo ya kesi kama tatu.
1. George Aldon Kilinga and another vs Anna Joseph Riwa and another Civil appeal no. 6 2023 TZ HC 19093.
2. Joseph Mkenda vs Ladislaus PC Civil Appeal No. 132, 2023 [2024] HC 56
3. Commissioner General Tz Revenue Authority and AG vs Milambo Limited Civil appeal No. 62/2022
Anasimama Mh. Lissu anaomba wampe Nakala ya kesi wanazotaja.
Jaji anasema mpatieni sasa.
Katuga anasimama anasema jaji zipo kwenye mtandao hizi kesi.
Mh. Lissu anasema sasa niko gerezani nazipataje huko mtandaoni? Watu wanacheka🤣🤣
Jaji anasema sasa mawakili wa serikali mpo wengi sana chaguaneni mmoja akazilete hizo printed case.
Anaondoka Wakili mmoja.
Anasimama Katuga anasema naona mahakamani yupo mtoto ni kinyume na sheria kifungu cha 193 cha CPA.
Jaji anasema haya muondoeni huyo mtoto.
Ni kama watu wamesikitika fulani. 🤣 ika ndio sheria sasa.
Dogo alikuwepo ana umri kama wa miaka 13 hivi amekula suti amependeza sana na alikuwa anasikiliza kwa hisia sana.
Anaonekana ana ndoto ya kuwa Wakili pia huyu na alivyo alivyo huyu dogo ni kama anamkubali Mh. Lissu.
Ipo siku tutapata story yake bila shaka hata kama ni baada ya miaka 15. Kuna siku anaweza kuja kulielezea Taifa kuhusu kisa hiki akiwa tayari amekuwa Wakili labda enzi hizo wahenga wanasema muda ni mwalimu mzuri.
Haya anaendelea Mrema sasa.
Mleta pingamizi hakuieleza mahakama anaposema mahakama hii haina jurisdiction kwa mfano pecuniary jurisdiction au nyingine.
Alivyotaja hiyo pecuniary mawakili wamecheka.
Watakuwa wameelewa jambo ambalo sisi ma layman hatuelewi.
Mawakili wamecheka kwa dharau nahisi kutakuwa na kaujinga hapo.😂😂😂
Nitawauliza niwape mchapo baadae.
Je mahakama hii ina mamlaka au laa ndio hoja kubwa sasa mwenzetu hajasema hayo mamlaka ni yapi katika zile aina za mamlaka zinazojulikana kisheria.
Part 2 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako kwenye tweet hii.