"Serikali ituambie na kutuhakikishia wananchi ni kwa kiwango kipi vipimo vyetu ni sahihi na thabiti(robust) kwa maana ya kutoa majibu sahihi ya uwepo wa virusi kwa mgonjwa husika na hasa kwa kuzingatia angalizo liliotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa @WHO." @ceciliaparesso
"Serikali ifanye jitihada za lazima na ziada Kuhakikisha kuwa kunakuwepo na maabara ya kupima sampuli za virusi katika hospitali zetu za mikoa na si utaratibu wa sasa wa kupeleka sampuli hizo kwenye maabara moja tu jijini Dar es Salaam."
Mhe. @ceciliaparesso (MB)
"Pale inapobidi wageni kuingia basi Serikali iwaweke kwenye karantini wageni hao kwa gharama zao kwa siku kumi na nne kama ambavyo taratibu za kitabibu zinavyoelekeza. Hii ni kwasababu wagonjwa wote waliothibitika mpaka sasa ni waliotoka nje ya nchi." Mhe. @ceciliaparesso
"Tumeshangaa kupitia vyombo vya habari kumemsikia Mkuu wa Mkoa wa Arusha akieleza umma kuwa dereva aliyemwendesha mtanzania wa kwanza aliyegundulika na virusi vya corona kuwa hana maambukizi yeyote, jambo la kujiuliza hapa je siku 14 zimetimia?"
Mhe. @ceciliaparesso (MB)
Kikao cha halmashauri ni bunge la halmashauri.. Mwenyekiti ndio boss kwenye kikao hicho. Dc kwenye kikao hicho ni mualikwa hata kuzungumza yeye lazima aruhusiwe na mkt wa kikao. Kama kuna fujo kwenye kikao kuna kanuni na kamati ya maadili. Kwanini awamu hii wanavunja sheria hivi!
Huyu ndio Dr Slaa anaetuambia tukilalamikia uonevu, mauaji, utekaji. Ukosefu wa demokrasia ni kuchafua nchi. Baba ulitufundisha kupigania haya na sisi bado tunaamini katika kupigania hayo.
Wazee/malaigwanan/machifu/na madiwani wa Ngorongoro wakiambatana na wawakilishi wa makabila ya wamaasai, wabarbaig, wambulu na wahadzabe, walinitembelea kuja kunipa pole, supu ya mbuzi na dawa za jadi za kuponya mifupa na joint haraka!