Mtafaruku wa kisiasa unaoendelea ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) @ChademaTZ2 umechukua sura mpya baada ya Ofisi ya CHADEMA Kanda ya Kati kumsimamisha uongozi rasmi Katibu wake Mkoa wa Morogoro, Barnabas Okola, kwa kosa la kukiuka maadili na kutoa shutuma nzito hadharani dhidi ya Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Wegesa Heche @HecheJohn .
Taarifa rasmi iliyotolewa leo Alhamisi, Julai 9, 2026, na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Kati, Ashura Mashaka Masoud imeeleza kuwa hatua hiyo ya dharura imechukuliwa ili kulinda nidhamu ya taasisi hiyo baada ya Okola kuitisha mkutano wa waandishi wa habari usiku wa kuamkia leo na kushusha makombora dhidi ya Heche kinyume cha kanuni za chama.
“Maamuzi haya yamechukuliwa kutokana na kitendo cha ndugu Barnabas Okola kukiuka sheria za maadili ya kiuongozi wa CHADEMA ya katiba ya chama ya mwaka 2006 toleo la mwaka 2019 kwa kuita mkutano wa waandishi wa habari na kutoa matamko na shutuma dhidi ya Makamu Mwenyekiti wa Chama Bara Mh. John Wegesa Heche kinyume na kanuni za maadili ya viongozi wa CHADEMA kanuni ya 10.1 (ix) na 10.1(x)”, imesomeka taarifa rasmi ya Ashura Mashaka Masoud.
Kanda ya Kati imempa Okola masharti ikimtaka kuwasilisha uthibitisho wa tuhuma zote alizozitoa dhidi ya Heche ndani ya siku 14, huku akipigwa marufuku kujihusisha na shughuli yoyote ya kichama kama kiongozi katika kipindi hiki.
@BrendaRupia The moment mtakapoingiza ajenda ya maridhiano ndio siku vijana wataachana na Chadema,mkimgusa Mh Heche mtabaki na vumbi......heshima yenu ndugu sugu na lema itaporomoka kwa spidi mtoroko..hamtakaa muinuke tena...Tupo na HECHE na mh LISSU kama kopo na mfuniko wake.
@AmaniHemedi@BrendaRupia Maandamano sio ya chadema ni ya watanganyika....na watanganyika walibadili mbinu wakawaacha vilaza wa intelgensia wawe wanazurura mitaani kama mazuzu,huku biashara na kazi zikisimama.
Bila kuathiri maazimio ya Kamati Kuu yatakayotolewa na Viongozi Wakuu wa Chama napenda kuwahakikishia Watanzania wote kuwa CHADEMA ni imara sana leo. Ni chama kilichojitoa kuikomboa Tanzania kutoka mikononi mwa Mamumiani wa CCM.
@Ntobi_ Kama mnakisaliti chama na uongozi wake....ni heri tu Mungu aingilie kati .mnasaliti mapambano kwa vipande vya fedha....Mungu awahukumu mwenyewe.