Uhuru Kenyatta: Mimi hakuna kitu natafuta, nimetosheka na yale nilifanya. Hata wakinitukana, waniite sponsor, rebel leader, mlevi... nawaangalia tu na kucheka kwa sababu they’re wasting their time. I only want Kenya to move forward as one
HATUTAENDELEA KUKAA KIMYA DHIDI YA UOVU.
Hii ni project yenye sessions 27 mpaka sasa zimefika tano. Nadhani huu siyo uchokozi dhidi ya TEC ,Father Charles Kitima, Mapadre wala Watawa na Wakatoliki wa kweli wenye mapenzi mema. Ni shambulio dhalimu dhidi ya Kanisa na Wapenda haki.
Kuruhusu TEC, Father Charles Kitima, Mapadre na Watawa wakatoliki kushambuliwa na kubagazwa ni kuruhusu watekeji ,utekaji na udhalimu kutamalaki.
Kama TEC ilisimama na UMMA wa Watanganyika hakutakuwa na kosa lolote sasa Watanganyika kwa umoja wetu kusimama na TEC kuukabili uovu na Wapangao Maovu.
Na umma huo wa watanganyika utakuwa na haki ya kutumia njia hizo hizo zinazotumiwa na udhalimu( reciprocity) kuukabili udhalimu huu.
Hili ni shambulio dhidi ya Kanisa,Nishambulio dhidi ya watetezi wa Haki za Binadamu na Nishambulio dhidi ya Katiba na Uhuru wa Kuabudu.
BAK MWABUKUSI.
Mtoto Khairath Salum (05) mkazi wa Chanika jijini DSM, alizaliwa na tatizo liitwalo "Congenital Pseudarthrosis" ambalo hupelekea kuvunjika kirahisi. Kutokana na tatizo hilo, mwaka 2023 alivunjika mguu wake wa kulia akiwa anacheza. Alipelekwa Hospitali ya Nguvukazi (Chanika) na kufungwa P.O.P lakini hata baada ya kutolewa P.O.P mfupa haukufanikiwa kuunga.
Baada hapo alipelekwa CCBRT na kufanyiwa upasuaji na kuwekewa chuma (K-Wire). Alikaa na chuma hicho kwa muda wa miezi 3 lakini chuma kililegea na hivyo kupelekea mtoto Khairath kuvunjika tena sehemu hiyohiyo ya mguu.
Alifanyiwa tena upasujia kwa mara nyingine na kuwekewa tena chuma ambacho alikaa nacho kwa muda wa miezi 9 lakini kwa bahati mbaya kilivunjika. Aliporejea tena CCBRT mpango ulikuwa ni kufanya "ORIF" kisha kufunga kwa 'Flexible Nail' lakini mpango huo haukufaulu hivyo akafungwa tena POP.
Baada ya miezi mitatu aliondolewa P.OP lakini bado alishindwa kutembea kutokana na maumivu ya kisigino. Iligundulika kuwa chuma alichowekewa (K-Wire) kililegea na kuchomoza kweye kisigino. Ilibidi aondolewe kifaa hicho ili kumpunguzia maumivu.
Hivyo kwasasa Khairath anahitaji kufanyiwa upasuaji mwingine ili kuweza kuunga mguu wake. Huu utakua upasuaji wa 4 tangu alipovunjika mwaka 2023. Kwa bahati mbaya Khairath ni yatima, aliyempoteza baba yake akiwa na umri wa miaka miwili tu. Yeye na ndugu zake wawili wanalelewa na mama yao ambaye ni mchuuzi wa mbogamboga sokoni Chanika.
Mama hana uwezo wa kugharamia matibabu, hivyo anaomba msaada ili mwanae aweze kufanyiwa upasuaji na kupona. Hii itamsaidia Khairath kuanza shule, kwani changamoto hiyo imemfanya ashindwe kuanza shule hadi sasa. Jumla ya gharama za matibabu ni TZS 3M tu.
Ikiwa utaguswa kuokoa miasha ya malaika huyu tuma sadaka yako kupitia M‑PESA: #0752581983 Tigo Pesa: #0719744954 CRDB: #0150633516500 NMB: #24110012109 Gifted Hearts Foundation, RudishaTabasamu, LetLoveLead.!