@JamiiForums Kuna maswali ya kujiuliza hili jina ni jina ambalo alipewa na wazazi wake? Ni kweli alifungiwa na timu ndio akaamua kubadilisha jina? Kwa hiyo badala ya kumhoji yeye tu, unatakiwa kufanya triangulation
Jumuiya ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDASA), imetoa tamko la kishujaa na la kihistoria ikisema kuwa mchanganyiko wa ubadhirifu wa mali za umma, uongo wa viongozi, na vitendo vya utekaji ndivyo vilivyolipua bomu la machafuko ya Oktoba 2025 nchini Tanzania. Katika kile kinachoitwa "Jicho la UDASA," wasomi hao wamechambua wasilisho la Tume ya Jaji Chande na kubainisha kero 53 ambazo zimejenga chuki iliyopitiliza kati ya Serikali na wananchi, wakisisitiza kuwa amani haiwezi kurejeshwa kwa nguvu ya silaha ikiwa viongozi wanaendelea "kuiba" huku raia wakitekwa na kupotezwa.
UDASA imepasua mbarika kwa kusema kuwa imani ya wananchi kwa Serikali imeporomoka kutokana na wizi wa kimfumo, ambapo viongozi na watumishi wa umma wamegeuka kuwa wezi wa mali za serikali na kuishi maisha ya anasa ya kufuru huku wananchi wakikosa huduma za msingi na ajira. Wasomi hao wamebainisha kuwa mmomonyoko wa maadili umefika hatua ambapo viongozi wanatoa taarifa za uongo mbele ya umma na kuonyesha kiburi dhidi ya raia, huku mifumo ya huduma kama hospitali, zimamoto, na ajira ikishindwa kufanya kazi kutokana na ubadhirifu na upendeleo uliokithiri.
Kuhusu hali ya usalama, UDASA imeweka wazi kuwa majeraha ya Oktoba yalisababishwa na ongezeko la kutisha la vitendo vya watu kutekwa na kupotezwa huku vyombo vya usalama vikishindwa kutoa majibu ya kuridhisha, jambo lililozua hofu na hasira kubwa. Jeshi la Polisi limetuhumiwa kutumia nguvu kupita kiasi dhidi ya raia na kutotenda haki, hali iliyofanya wananchi kuliona chombo hicho kama tishio badala ya mlinzi, huku Tume ya Uchaguzi na Mahakama zikitajwa kukosa uhuru na kuwafanya wananchi wahisi nguvu yao ya kuchagua viongozi kwa kura imepokwa na "wezi wa kura."
Mwenyekiti wa UDASA, Dkt. Elgidius Ichumbaki, amesisitiza kuwa Serikali lazima ijishushe na ikiri makosa yake ili kurejesha amani ya kweli nchini. UDASA imetoa wito wa kuanzishwa mara moja kwa mchakato wa Katiba Mpya itakayozuia ubadhirifu na kulinda haki za raia, kuwashitaki viongozi wabadhirifu, na kutoa maelezo ya kweli kuhusu watu waliopotea.
Tamko hilo limehitimisha kwa kuonya kuwa amani ni tunda la haki, na bila kushughulikia wizi na utekaji, maumivu ya wananchi yataendelea kuwa bomu linalosubiri kulipuka wakati wowote.
@CloudsMediaLive@FKihamu Semeni tatizo kubwa ni kukosa maadili, uwajibikaji na uzalendo. Pia ubinafsi umeshamiri kwa sababu ya kukosa maadili na uwajibikaji