Good Job Watanzania, wow wow wow.
Hongereni Watanzania maana zamani hata kuwazomea hivi CCM tulikuwa tunaogopa ila sasa hivi hatuwaogopi tena hawa wauwaji na machawa wao.
Watanzania, video kama hizi zinatutia moyo wanaharakati wenu tuendelee kupambana kwa niaba yenu. Yani mimi personally nimeangalia video hii nikajiambia, it’s worth it kupigania nchi yangu, Acha ma cartel waje kuniua ila napigania watu ambao wako tayari kujipigania…..,
Mmejua kunipa raha mchana huu.
@tedcruz@SenatorShaheen@Europarl_EN This is the reality in Tanzania: the people have rejected Samia Suluhu and her regime. The moment her government was mentioned, the crowd erupted in boos. The minister wasn’t even given the chance to finish his sentence.
The only reason CCM remains in power is through killings, fear and force. Tanzanians are being held hostage at gunpoint, not governed with the consent of the people.
Arusha, asanteni sana. Baada ya muda mrefu bila kukutana, leo mmekuwa mashuhuda wa upendo wa demokrasia na haki katika nchi yetu. Pamoja na hofu iliyojengwa juu ya maumivu makali, mateso na mauaji, bado mmejitokeza kwa matumaini makubwa.
Mungu awabariki . Love you sana.
MaCCM msipotoshe NO REFORMS; NO ELECTION.
Kuna namna msimamo wa kamati kuu ya CHADEMA umeanza kupotoshwa usieleweke.
Unapotoshwa kwa makusudi na MaCCM. Hofu yao ni CHADEMA kutoshiriki ‘uchafuzi’ huo.
MaCCM wanamiliki vyama 19 mfukoni lakini hawaridhiki kuona CHADEMA hawashiriki.
Namna msimamo unavyopotoshwa unaelekea kugeuzwa kuwa maneno ya kwenye khanga.
Msimamo si kutoshiriki uchaguzi, ni ama reforms zifanyike au uchaguzi usifanyike.
Kwamba, hata MaCCM na wenzao wasiwe na ‘uchafuzi’ wa kushiriki kama hakuna reforms.
CHADEMA ikishindwa kushinikiza reforms, haipaswi kushindwa kuzuia uchaguzi kufanyika
Hakuna marekebisho ya sheria na kanuni za uchaguzi, hakuna uchaguzi wowote kufanyika.
Hivi ndivyo ambavyo nilielewa azimio la kamati kuu ya CHADEMA na limerejewa mara kadhaa.
Msimamo wa CHADEMA upo namna hiyo na usitafsiriwe vinginevyo. No reforms, no election
Msimamo huo wa chama uwekwe katika fremu na uning’inizwe katika kuta za ofisi zetu zote.
Pia, msimamo huo wa chama uwekwe katika kuta za sebule za viongozi wakuu wa chama.
Kwanini, ili wasije wakasahau na kutupeleka katika ‘uchafuzi’ kwenda kuporwa na kuuwawa.
Uchaguzi wetu umemalizika, na sasa tunajenga taasisi yetu. Baada ya uchaguzi mshindi ni CHADEMA. Tujivunie tulivyowafundisha demokrasia wengine.
Viongozi wataondoka, CHADEMA itabaki. Muhimu kuilinda CHADEMA kwa wivu mkubwa. Waliochaguliwa ni wanachama wa CHADEMA. Wanastahili kuongoza.
Maturity is knowing that in life you will loose some and you will win some. You’ve got to live with it. You might have lost this battle but you’ve not lost the war.
Vita yetu ni dhidi ya MaCCM na sio vita against each other. Do not loose your eyes on the prize. Stay focused on your goal and not get distracted by anything else.
Hakuna sababu ya kupambana wenyewe na kuzodoana. Tunayapa haya majitu - MaCCM sababu ya kupumzika na kuchekea chooni. MaCCM yanatushangaa.
MaCCM yanatakiwa kupumzika motoni tu. MaCCM ndiyo adui zetu. MaCCM hayatakiwi kuwa na amani. Tumemaliza uchaguzi. Tusimame, tuelekee mbele.
Tuondoke katika 'mode za uchaguzi', twende katika 'mode za ujenzi wa chama'. Kuna majukumu mengi ya kufanya kwa wanachama na viongozi wa chama.
Let's stay focused. Run, go! Get the chopper!
Freeman Aikaeli Mbowe
Kwangu umekuwa siyo tu kiongozi wangu wa chama bali ni mwalimu, mwanafalsafa,mkufunzi,mzazi,mlezi na rafiki wa kweli. Wewe ni mfano wa kuigwa
Nashukuru kwa kuniamini na kunipa jukumu la kuwa Mwenyekiti wa kampeni zako katika uchaguzi mkuu wa chama January 2025.
Unajua,umeona, umesikia na umeshuhudia hadi sekunde ya mwisho nilivyo simama na wewe na nilivyojitoa kwa hali na mali kufanya jukumu lile zito lililokuwa mbele yetu lakini bahati haikuwa upande wetu.
Sikuwahi kufikiri au kudhani ipo siku mwalimu wangu wa siasa atanipa mimi mwanafunzi wake kazi ya kusimamia kazi yake ya siasa
Hata hivyo nachezwa na machale, ninavyokufahamu itakuwa ulikuwa kuna kitu ulitaka nijifunze kwenye majukumu yangu ya kusimamia kampeni zako.
Moja ya funzo kubwa na la ajabu nitalikumbuka daima katika uchaguzi huu ni pale uliponieleza
"Watu wako rasmi uliowapa jukumu la kufanya kampeni wasifanye Jambo lolote bila idhini yako, na pia katika kila jambo tutakalofanya tusikiumize chama kwa namna yoyote ile au kwa kisingizio chochote kile"
Mapenzi yako kwa CHADEMA na wanachama wa CHADEMA ndiyo yalinifanya nikubali kubeba Jukumu hili zito,ulistahili "support" yangu hata kama Dunia nzima ingekusaliti kisiasa na kukugeuka bado mimi ningebakia peke yangu kuwa pembeni yako.
Ndiyo maana nilipoona kura zetu hazijatosha sikuhitaji ruhusa yako kusaini fomu ya matokeo kuwa Mheshimiwa Tundu Lissu ni mshindi
Na nilipokujulisha matokeo ya uchaguzi kuwa wajumbe 482 walihitaji uwe Mwenyekiti wao na wajumbe 513 wameamua ukapumzike, watu wengine uliokuwa nao chumba cha VIP wakiwa wanalia wewe ulinyanyuka ukanikumbatia kisha ukachukua simu yako ili kupongeza na kukubali matokeo kupitia ukurasa wako wa X na kuanza kujadili swala la kurudi ukumbini tayari kupokea matokeo rasmi.
Hili ni somo kubwa sana kwangu.
Wewe utabakia kuwa Jenerali wangu wa kweli na kiongozi wangu siku zote. Nitakuwa tayari siku yoyote na mahala popote kutumwa au kupokea majukumu kutoka kwako hata nje ya siasa.
Nakutakia maisha mapya nje ya majukumu makubwa ya kisiasa.
"We protect the Purpose and not a person"
Boniface Jacob (Boni Yai)
Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Pwani
Thursaday, Jan 23, 2025.
Nimesoma neno la leo katika Kalenda ya KKKT kwenye Biblia kutoka Kitabu cha Yakobo 3 : 13 - 18. Limenirutubisha. Natamani nanyi mrutubishwe nalo.
"Je, ni nani mwenye hekima na akili miongoni mwenu? Basi, aoneshe jambo hilo kwa mwenendo wake mzuri na kwa matendo yake mema yanayofanyika kwa unyenyekevu na hekima. Lakini ikiwa mioyo yenu imejaa wivu, chuki na ubinafsi, basi, msijisifu na kusema uongo dhidi ya ukweli. Hekima ya namna hiyo haitoki juu mbinguni; hekima hiyo ni ya ulimwengu, na ya kidunia, tena ni ya kishetani. Maana popote palipo na wivu na ubinafsi, hapo pana fujo na kila aina ya uovu. Lakini hekima itokayo juu mbinguni, kwanza ni safi; inapenda amani, upole na huwajali watu; imejaa huruma na huzaa matunda ya matendo mema; haina ubaguzi wala unafiki. Uadilifu ni mazao ya mbegu ambazo wapenda amani hupanda katika amani."
Nimeyashuhudia matokeo, Wanachadema mmeamua kwa kura, Niwapongeze Mwenyekiti Mpya Mh Tundu Lissu, na Makamu Mwenyekiti Mh John Heche kwa ushindi huu. Niwatakie utumishi mwema wa Chama chetu.
Na Yericko Nyerere
Kwa kuwa nilitangaza kumuunga mkono @freemanmbowetz katika uchaguzi wa chama chetu hadharani, ndivyo nampongeza @TunduALissu kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA katika uchaguzi huru na haki. Binafsi, namtakia heri katika uongozi wake. CHADEMA tumetoa darasa la demokrasia. ✌🏾
Nimepokea kwa mikono miwili maamuzi ya uchaguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama chetu CHADEMA uliohitimishwa leo asubuhi 22 Januari 2025. Nampongeza Mhe. Tundu Lissu na wenzake kwa kuaminiwa kutwikwa jukumu la Uongozi wa Chama. Nawatakia kila la kheri katika kukipeleka mbele Chama chetu.
VIDEO:
"Mheshimiwa Mwenyekiti (Freeman Mbowe) nakushukuru sana, na naomba niseme hii hapa kwamba nimekaa pembeni ya Mwenyekiti wetu wa chama kwa miaka zaidi ya 20 na katika kipindi chote hicho hatujawahi kugombana, hatujawahi kuvutana mimi na yeye binafsi, ndio tumetofautiana kimisimamo lakini hatujawahi kugombana, sijawahi kuwa na ugomvi na Mwenyekiti na natumaini hili litaendelea baada ya leo Mheshimwa Mwenyekiti" -Lissu
Mgombea Uenyekiti wa CHADEMA taifa Tundu Lissu akizungumza siku ya Jumanne Januari 21, 2025 katika Mkutano Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) unaofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City mkoani Dar es Salaam.
“Sijawahi kugombana na Mwenyekiti wangu Mbowe kwa miaka yote ambayo nimefanya nae kazi, na hatutagombana hata mara baada ya uchaguzi huu, na kivyovyote vile itakavyokuwa leo tutabaki kujenga chama chetu” - @TunduALissu