A human rights focused Org, that works to prevent the spread of AIDS and addressing challenges that affects the vulnerable population and Gender Based Violence
Taasisi ya Community well-being foundation (CWF) inawatakia Waislamu wote na Watanzania kwa Ujumla heri ya Mfungo Mtukufu wa Ramadhani! Ramadhani Kareem!
Hii ni mikoa mitano inayoongoza kwa kiwango cha maambukizi ya VVU (HIV prevalence) nchini Tanzania kulingana na data kutoka Tanzania HIV Impact Survey - THIS 2022/2023,
1. Njombe - 12.7%
2. Iringa - 11.1%
3. Mbeya - 9.6%
4. Songwe - 7.1%
5. Ruvuma - 4.5%.
Tulipata Fursa ya Kushiriki Mafunzo ya uandishi wa Ripoti chini ya Zangof - Zanzibar! Taasisi yetu iliwakilishwa na Safia Mgeni - Mwanachama na afisa wa kujitolea kwenye Shirika letu la #CWF
Pamoja na yoote muhimu ya Huzuni na faraja, yanayoendelea nchini - Sisi #CWF tunatumia fursa hii kumtakia Mkurugenzi wetu Mtendaji siku yake ya Kuzaliwa! Heri Yako ya siku ya kuzaliwa Bi @makiyye Mkurugenzi Mtendaji wetu.
Wanawake wa Kiislamu nakuombeni muelewe HAKI zenu. Ukichangia kwenye UJENZI wa nyumba una HAKI kwa mujib wa sheria za Kiislamu kupata asilimia ya mchango wako. Nakuombeni wekeni USHAHIDI wa mchango wenu.
Mwanaume hana haki ya kuchukuwa MALI ya mke wake kwenye UISLAMU.
Bi @MakiyyeJuma Kwa Niaba ya #CWF, aliendeeana ziara yake ya Kuitambulisha Taasisi yetu kwa wadau wengine wanaojihuisha na masuala ya Utetezi wa Mwanamke - na hapa alifika Ofisi za TAMWA.
Bi @MakiyyeJuma Mkurugenzi wa Taasisi yetu ya #CWF akijitambulisha na kufungua milango ya mashirikiano baina yetu na Taasisi ya Wildaf Tanzania. Pamoja nae, alijumuika na baadhi ya Wanawake Viongozi wa Kisiasa ktk kutanua WiGo wa nafasi ya Mwanamke ktk Jamii. #HIVPrevention
BREAKING NEWS KUTOKA KWA RAIS TRUMP INAYOTUHUSU NI AFYA ZA MAMILIONI YA WATU KUWA HATARINI. Ikiwa uamuzi wake kusitisha misaada kwa mashirika ya afya duniani hasa PEPFAR na GLOBAL FUND yatatekelezwa ni kiama. Upatikanaji wa madawa ya kuongeza kinga za mwili ARVs utaathirika. Ninashauri Wizara ya Afya kuufahamisha umma wa waTanzania je ni hatua gani za haraka zinachukuliwa kutathmini jambo hili na kuchukua hatua stahiki?.
Ikibidi African Union waitishe kikao maalum kuangalia swala hili na kuweka mkakati wa pamoja. Waathirika wa gonjwa hili la UKIMWI ni waAfrika na ugonjwa haujulikani ulitoka wapi?. Tujitetee.
Aidha juhudi za kuthibiti maambukizi ya virus vya ukimwi ziwekewe nguvu mpya. Upatikanaji wa ARVs utakuwa mgumu. Na kununua ARVs kibiashara ni jambo litakalohitaji bajeti kubwa na uwezo wa taifa kwa ujumla ni mdogo. Na jambo limekuwa la ghafla. Waathirika wengi hawana uwezo kununua madawa hayo wenyewe maisha yao yote. Afya zao zikidhoofika itatumika gharama kubwa kuwauguza hivo kusababisha umaskini na vifo. Pia bila ARVs maambukizi yatashika kasi mpya. Tuwe macho
Uzinduzi Rasmi wa Mradi wa #MeettheGreat#Zanzibar ambao umejikita ktk kuwekeza kwenye Vipaji vya Vijana. Sisi #CWF tumechagua kuwaunga Mkono MEET THE GREAT ili kuongeza Kasi yamaendeleo ya Vijana Zanzibar na Tanzania.
Our Director Ms. Makiyye Juma, proudly participating in the launch of the Talent Development and Empowerment Project for Youth in Zanzibar 🌟 Our CWF, is one of the sponsors of this unique initiative, #MeetTheGreat. We look forward to seeing the talents of the youth flourish 💪
Mkurugenzi wetu, Bi Makiyye Juma, akishiriki kwa furaha katika uzinduzi wa Mradi wa Kuinua na Kuboresha Vipaji kwa Vijana #Zanzibar! Taasisi yetu ya CWF ni moja ya wadhamini wa mradi huu wa kipekee, 💪 #MeetTheGreat . Tunatarajia kuona vipaji vya vijana vikichanua! #VIPAJI#CWF
Wakati mkoa wa Njombe ukiwa na watu 66,979 wanaoishi na Virusi vya UKIMWI, mkoa huo umeendelea kusambaza kondomu ili kukabiliana na maambukizi mapya ya virusi hivyo huku vijana wakitakiwa kuendelea kuchukua tahadhali na janga hilo.