War does not resolve any problem. It only sows death
and destruction, increases hate, multiplies vengeance. War erases the future. I exhort believers to to take only one side in this conflict: the side of peace -- not in word, but in prayer. Let the weapons be
silenced.
Nitumie nafasi hii kuishukuru Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM chini ya Mwenyekiti wake na Rais wetu Mpendwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuniteua kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania ngazi ya Taifa. Ni heshima kubwa kuona Chama changu kikiendelea kutuamini Vijana na kutupa majukukumu makubwa ya kukitumikia Chama na Taifa. Naamini uteuzi huu utakuwa chachu kwa Mabinti wadogo Chipukizi wa Chama kupambania ndoto zao wakiamini wanacho Chama ambacho kinawajali na kuwaamini watu wote wenye uwezo na dhamira ya kweli ya kuleta mageuzi ya kweli na maendeleo ya Chama na Taifa letu.
Nimeupokea uteuzi huu kwa unyenyekevu mkubwa na furaha kubwa. Namshukuru sana Mwenyezi Mungu bila kuisahau Familia yangu, Chama changu, Wananchi wa Korogwe niliokuwa nawatumikia kwenye nafasi ya Ukuu wa Wilaya, Ndugu, Jamaa na Marafiki wote mnaoendelea kuniombea na kunishika mkono. Nimepokea meseji na simu nyingi za pongezi, nimezisoma pia comments zenu nzuri mitandaoni, nawashukuru sana.
Nimejipanga kushirikiana na Viongozi na Wanachama wenzangu wote wa UWT kote nchini kwa uadilifu, ueledi, ubunifu, ustadi, uzalendo, umakini nikitanguliza mbele maslahi mapana ya Chama na Taifa ili kuendelea kuiimarisha Jumuiya yetu na kukijenga Chama chetu.
Aidha, nipo tayari kushirikiana na Wadau wote wanaopigania Maendeleo na Ustawi Wanawake kote Duniani bila kujali tofauti zetu za Itikadi za Vyama, Dini, Utaifa, Kabila.
@SuluhuSamia

Mwaka 2005, nilijiunga na Chuo Kikuu Bangalore India kwa degree yangu ya kwanza katika Psychology, Lugha na Habari. Dr. Salim Ahmed Salim alitoa pesa yake mfukoni kuwa sehemu ya ada ya masomo yangu India. Siwezi kusahau wema na ukarimu wake.🙏🏾🙏🏾🙏🏾
Pongezi za dhati kwa Mwadhama Protase Kardinali Rugambwa, kwa kusimikwa rasmi na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Kardinali. Kauli mbiu ya utume wako ni "Enendeni ulimwenguni kote", ikiakisi mafundisho ya Yesu Kristo katika Injili ya Marko 16:15, juu ya utume unaojali watu wote, sehemu zote na wakati wote. Naungana na Watanzania wote kukuombea kheri, afya njema, na mafanikio katika utumishi wako.