Klabu ya Yanga imezindua jezi mpya itakazotumia katika msimu wa 2026/27, huku uzinduzi huo ukipewa uzito wa kipekee baada ya kufanywa na mwandishi maarufu wa habari za usajili duniani, Fabrizio Romano.
Hatua hiyo imeongeza mvuto wa uzinduzi wa jezi hizo, ambazo Yanga itazitumia katika mashindano ya kimataifa.
Kwa Wananchi, kuhusishwa kwa jina kubwa kama Fabrizo Romano katika uzinduzi huo ni ishara nyingine ya namna Yanga inavyoendelea kujijenga kama brand kubwa nje ya mipaka ya Tanzania.
#KitengeSports
Breaking: Meli ya Mafuta inateketea kwa moto muda huu katika Bandari ya Kigoma ya Ziwa Tanganyika huku Chanzo cha moto huo kikiwa bado hakijafahamika.
Inasemekana Meli hiyo ya Mafuta ilikuwa ikijiandaa kuelekea nchini Congo.
Endelea kufuatilia #kitengetv_tz kwa taarifa za kina zaidi juu ya tukio hilo
#KitengeUpdates
Klabu ya Simba kupitia kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Jayrutty, Joseph Rwegasira, wamezindua mfumo wa kununua jezi ambao utashirikisha mashabiki wa simba kushiriki kununua Mchezaji wanaemtaka kabla ya Dirisha la Usajili kufungwa Agosti 15, 2026.
#KitengeSports