Tundu Lissu amepewa namba ya mfungwa ambayo ni 623.
Ukisoma Luka 6:23 inasema “Furahini siku ile na kuruka-ruka, kwa kuwa, tazama, thawabu yenu ni kubwa mbinguni, maana, baba zao waliwatenda manabii vivyo hivyo.”
Kila kitu kinachotokea kwenye maisha ya Tundu Lissu ni kusudi la MUNGU tusihuzunike sana.
USHINDI UNAKUJA NA HAUPO MBALI.
GOOD MORNING.
REPOST 200
#FreeTunduLissu
VIDEO:
Mzee Muro Lissu, mdogo wa marehemu Wakili Alute Lissu, amesema anatamani Tundu Lissu angekuwepo ili aweze kushiriki maziko ya kaka yake, lakini isivyo bahati sheria haijamruhusu kufanya hivyo.
Mzee Muro ameyasema hayo leo Novemba 9, 2026, eneo la Mahambe, Wilaya ya Ikungi, Mkoa wa Singida, ambako mwili wa marehemu Wakili Alute Lissu unatarajiwa kuzikwa kesho katika makaburi ya familia.
Amesema hukumu ya kifungo cha miaka minne alichopewa Tundu Lissu imewaumiza na kuwahuzunisha, kwani walikuwa na matarajio ya kumuona kiongozi wao akishiriki mazishi ya kaka yake.
Nimetoka Gereza la Ukonga, kumtembelea Mhe Tundu Antiphas Mghwai Lissu mfungwa mwenye namba 623/2026, yuko salama ameanza maisha mapya.
Mhe lissu ametupatia ridhaa Mawakili wa Chama, chini ya Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA Dr Rugemeleza Nshalla kumwakilisha kwenye rufaa inayokusudiwa kusajiliwa na mambo yote yanayohusiana nayo, kufuatia uamuzi uliotolewa tarehe 6 November 2026 na Mahakama kuu, Masijala ya Dar Es Salaam.
Mhe Lissu amepokea nakala ya taarifa ya kukata Rufaa (Notice of Appeal) ambayo imesajiliwa Mahakamani, pamoja na nakala ya hukumu iliyosomwa November 06, 2026.
Aidha, hatua nyingine za kisheria zinaendelea kwa uratibu wa mawakili wake.
5. ATHALI YA HUKUMU YA MIAKA 4 KWA TAL (ZUIO LA DHAMANA):
Kwa kumpa TAL kifungo kizima cha miaka 4 bila kupunguza siku 577 za mahabusu, mahakama imefunga mlango wa yeye kupata dhamana ya rufaa kwa kigezo kifuatacho:
Mahakama inaweza kutumia kisingizio kuwa adhabu yake ni ndefu (miaka 4), hivyo kuna muda mwingi kwa mahakama kupanga na kusikiliza rufaa ya LISSU akiwa bado yuko gerezani. Hii itamlazimisha LISSU kubaki ndani.
HESABU YA KISHERIA KUHUSU IDADI YA SIKU ZA ADHABU & UMUHIMU WA UPUNGUZWAJI WAKE (Kama Siku Zingekatwa):
Kama mahakama ingefuata sheria na kukata siku 577 za mahabusu ambazo LISSU amekaa gerezani kabla ya kutiwa hatiani, pamoja na punguzo la robo la Sheria ya Magereza (Kifungu cha 49 cha Prisons Act [CAP. 58]), ambalo ni AUTOMATICAL mfungwa anapoanza tumikia kifungo chake siku ya kwanza, adhabu ya TAL ingebaki kuwa Mwaka 1 na Miezi 9 (Siku 663) tu.
Hili lingetokea, ingekuwa nguvu ya kupata dhamana kupitia maamuzi ya Mahakama Kuu & ya Rufani. Kwa kuwa, kisheria, muda huu wa mwaka mmoja na miezi 9 unaangukia kwenye kundi la "adhabu fupi" (short sentence), ambapo huzingatiwa kwenye dhamana.
Misingi ya utoaji dhamana wakati wa rufaa kwa adhabu fupi inalindwa na kesi zifuatazo:
1. Subira Lukanima and Others vs Samson Bulime (2026): Katika uamuzi huu wa Mahakama Kuu, mahakama ilitoa dhamana wakati wa rufaa kwa wafungwa kwa msingi mkuu kuwa adhabu waliyopewa ilikuwa fupi na kulikuwa na hatari kubwa ya kifungo hicho kuisha au kuisha kwa kiasi kikubwa kabla ya rufaa yao kusikilizwa kikamilifu.
2. Melaku v The People (Pamoja na miongozo ya kikanda ya Bail Pending Appeal): Kesi hii inasisitiza msimamo wa kawaida wa kisheria kuwa pale mfungwa anapopewa adhabu fupi, kuwepo kwa pointi za msingi za kisheria kwenye rufaa yake kunailazimisha mahakama kumpa dhamana. Hii ni kwa sababu itakuwa ni uonevu mkubwa kumzuia uhuru wake gerezani kwa miezi michache, halafu baadaye ije ionekane alikuwa hana hatia wakati adhabu ameshamaliza.
Kutokana na hoja hizi & msimamo wa kisheria, nina imani kubwa LISSU atapata dhamana, na hata huenda mahakama ya Rufani ikabadili adhabu yake au hata kufuta hukumu ya Mahakama Kuu (kwa sababu hakukuwa na kosa la UCHOCHEZI).
Ila tu, pia tuzingatie kuwa hii ni kesi ya KISIASA & tujiandae kwa lolote. Ila, kikubwa najua adhabu yake ni LAZIMA itapunguzwa.
HAKI HAIOMBWI BALI HUPIGANIWA.
TUSONGE MBELE #BabaMwita ⚖️
Breaking news
Nimepigiwa simu na mke wa Gwamaka kuwa Gwamaka amekamatwa na polisi asubuhi ya leo saa moja, pia napoandioanhii sms naambiwa Mwenyekiti wa Chadema Songwe Isakwisa Lupembe naye amekamatwa leo!
TAL!
Baada ya kukutwa na hatia aliomba kuongea na mawakili wake, tukamzunguka kila mtu akawa anampa mitigation facts,
akasema kwani hamjui wana hukumu?, tukamjibu tunajua!,
akasema nikifanya mitigation itabadili hukumu yao?, tukajibu hapana!
Akasema let me speak my mind!
Mwaka 1957 wakoloni wazungu walimfungulia Mwalimu Nyerere kesi ya uchochezi.
Kwenye hiyo kesi wakoloni wazungu walimkuta na hatia mwalimu Nyerere. Pamoja na kumkuta na hatia Mwalimu wakoloni hawakumfunga Nyerere gerezani bali walimlipisha faini na akaenda nyumbani.
Miaka zaidi ya 70 baadae, mahakama chini ya majaji kina Ndunguru na Jaji mkuu Masaju.
Yenyewe imejiundia kosa, imejitafutia ushahidi, imemfunga kiongozi wa upinzani nchini tena kwenye kosa lenye faini.
Ccm na serikali ya Samia Suluhu Hassan ni makatili kuliko wakoloni wazungu.
Historia itawaweka mnapostahili.
SIKU YA AIBU KWA UTAWALA WA SHERIA!
Sisi ni nchi inayofuata mfumo wa Common Law, siyo mfumo wa Civil Law Katika mfumo wetu, Mahakama ni mwamuzi huru na asiyeegemea upande wowote (impartial adjudicator), siyo mpelelezi, siyo mwendesha mashtaka, wala siyo mtunga mashtaka.
Lakini kwa hali ya kushangaza, leo tunakutana na Mahakama inayochukua majukumu yote kwa wakati mmoja: inaandaa shtaka (charge), inafanya uchunguzi, inaendesha mashtaka, inakusanya ushahidi, inabaini kosa, inamkuta mtuhumiwa na hatimaye kumhukumu, bila kumpa nafasi ya kusikilizwa ipasavyo.
Huu siyo utendaji wa Mahakama inayosimamia haki. Huu ni kuvuruga misingi ya haki asilia (Principles of Natural Justice), haki ya kusikilizwa (Right to be Heard) na kanuni ya kutokuwa hakimu katika shauri lako mwenyewe (Nemo Judex in Causa Sua).
Mahakama haiwezi kuwa mlalamikaji, mpelelezi, mwendesha mashtaka na hakimu kwa wakati mmoja.
Hata kama ni kosa dogo lazima liwe cognate offence yaani kosa linaloendana au kuhusiana na kosa analoshtakiwa. Naliwe sehemu ya shitaka na ushahidi utolewe kuhusu hilo na mtuhumiwa ajitetee.
Na pia ni Kanuni za Msingi katika Taifa letu kwamba kunapokuwa na adhabu ya Kigungo na Faini au vyote kwa pamoja ni lazima uanze kwanza na adhabu ya faini akishindwa kinafuata kifungo. HII NI AIBU KUBWA.
Kazi ya Mahakama ni kutenda haki kwa kusikiliza pande zote kwa usawa, siyo kutafuta au kubuni njia za kumtia mtu hatiani.
Tunapofika hapa, tunakuwa hatujadili tena hatima ya mtuhumiwa mmoja tu; tunajadili uhai wa utawala wa sheria katika nchi yetu.
UKWELI, HAKI NA UWAJIBIKAJI NDIVYO VITALIPONYA TAIFA!
BAK MWABUKUSI
BAIL PENDING APPEAL:
Kwa kuwa TAL ameshinda kesi ya UHAINI ambayo haina dhamana, na kukutwa na hatia kwa kosa la UCHOCHEZI, Lissu anaweza kuwa nje kwa DHAMANA kupitia utaratibu unaojulikana kisheria "BAIL PENDING APPEAL" kwa sababu uchochezi una dhaminika, hata kama mtu amefungwa. Ila tu utaratibu ni kwamba, ni LAZIMA mfungwa aanze kutumikia kifungo chake gerezani japo kwa siku moja tu.
Hii inawezekana kama mawakili watajenga hoja za AFYA ya Lissu na kwamba atashindwa kupata matibabu stahiki akiwa gerezani. Pia, siku 577 alizokaa gerezani ni fimbo ya kuomba dhamana. Imefanyika mahakama Kuu & pia kuna msimamo wa mahakama ya Rufani juu ya utaratibu huu.
HAKI HAIOMBWI bali HUPIGANIWA.
Leo ni BLACK FRIDAY.
Mahakama Kuu inapotoa uamuzi kuhusu tafsiri ya sheria, uamuzi huo unaweza kuwa na athari kwa kesi zijazo, hasa katika Mahakama za chini.
Uamuzi wa leo uliotolewa na Mahakama Kuu una hatari ya kuwa judicial precedent itakayotumiwa na Mahakama za chini katika kuamua kesi zijazo,
Uamuzi huo utaathiri kwa upana zaidi haki ya washtakiwa wanaoshindwa kutiwa hatiani kwa makosa makubwa waliyoshtakiwa nayo.
Kwamba sasa imewezekana mtuhumiwa kufikishwa mahakamani kwa kosa kubwa, akanyimwa dhamana na kukaa mahabusu kwa takribani siku 577
Wakati mtuhumiwa akisubiri haki yake atakuwa akitokea gerezani kwenda mahakamani. Kwamba, mtuhumiwa atapoteza uhuru wake wakati wote.
Upande wa Jamhuri ukishindwa kuthibitisha kosa aliloshtakiwa nalo, Mahakama inachukua ushahidi huo huo na kutengeneza kosa jingine dogo,
Halafu Mahakama inatoa hukumu ya kifungo gerezani bila fursa ya kulipa faini. Hakimu atafanya rejea ya kesi ya Jamhuri Vs. Tundu A.M Lissu.
Unafungwa gerezani kwa kosa ambalo hujashtakiwa na hujawahi kusikilizwa popote. Unabadilishiwa kosa lako ukiwa kizimbani na unahukumiwa kifungo.
Hii ni siku mbaya sana kwa utawala wa sheria, haki ya kusikilizwa na misingi ya utoaji haki. Kama unaona haikuhusu, itawagusu ndugu, jamaa na rafiki zako
Mwenyekiti wa Chadema, Mhe. Tundu Lissu, alichaguliwa kuwa Mwenyekiti Januari 21, 2025.
Hata hivyo, ameongoza nafasi hiyo akiwa uraiani kwa siku 78 pekee, sawa na miezi miwili na siku 19.
Alikamatwa Aprili 9, 2025, mjini Mbinga, mkoani Ruvuma. Aprili 10, 2025, alifikishwa mahakamani na kusomewa shtaka la uhaini.
Baada ya kukaa mahabusu kwa takribani mwaka mmoja, miezi sita na siku 28, Mahakama Kuu ya Tanzania, leo Novemba 6, 2026, imemuondolea hatia ya uhaini baada ya kubaini kuwa upande wa mashtaka haukuthibitisha kosa hilo.
Hata hivyo, Mahakama imemkuta na hatia ya kosa dogo la uchochezi katika shitaka la Uhaini na kumhukumu kifungo cha miaka minne jela.
Mahakama imemhukumu Mwenyekiti wa Chadema, Mhe. Tundu Lissu, kifungo cha miaka minne jela kufuatia kutiwa hatiani kwa kosa la uchochezi katika kesi iliyokuwa ikimkabili ya uhaini.