Maisha haya yanapita kama upepo. Usipoona thamani ya siku moja, wiki moja, mwezi mmoja, kufumba na kufumbua, kitenzi kikurupushi kinaanza kukuandama. Ukiwa na miaka 20 ni kama huoni kikwazo chochote mbele yako. Muda unao. Ukitazama mbele unajiona ukipata kila unachokihitaji. Huambiki. Hushauriki. Rahisi sana kupotelea kwenye shughuli zinazokuwekea akiba nzuri ya majuto miaka ijayo.
Ukiwa na miaka 30, na bado hujakarabati tabia zako vizuri, unaanza kugundua mambo sio rahisi kama ulivyofikiri. Kazi ulizozibeza ukiwa na miaka 20 na, kumbe nazo ni ngumu kuzipata. Unaanza kugundua kumbe mahusiano si rahisi kama ulivyofikiri. Unaowapenda hawakupendi na wanaokupenda huwaamini. Kumbe si kila mtu kaumbiwa furaha ya mahusiano. Unajielekeza kwenye kazi ambazo nazo haziendani na ndoto zako. Unaanza kuwa na hofu ya mengi lakini bado unaona muda upo.
Ukiwa na miaka 40 unaanza kuukabili ukweli ulioukwepa kwa muda mrefu. Unaanza kuuishi upweke wa kukosa mtu wa kumwamini. Unaanza kupambana na matokeo ya kuishi maisha yenye mafanikio yasiyokuwepo. Matokeo ya maamuzi uliyofanya miaka 20 iliyopita yanaanza kukuwinda. Unaanza kuishi kwenye ninge, ningefanya hivi, ningekuwa vile. Unaanza kuona ulivyo na mengi ya kufanya na muda huna. Jumatatu, mara Jumamosi hii hapa. Tarehe 1, mara tarehe 30 hii hapa. Muda huna. Unawasahau watoto. Unaitelekeza familia.
Mara unaanza kuona mvi moja moja. Mara huzioni tena siku zako. Mara unaanza kupewa shikamoo na watu unaoamini mnalingana. Kufumba na kufumbua miaka 50 hii hapa. Kila mpango wa muda mrefu unaanza kuuogopa. Hata taasisi za fedha zinaanza kuwa na tahadhari na wewe. Kazini, kama umeajiriwa, wanaanza kukuona kama mzigo. Ubabaishaji wa miaka mingi unaanza ‘kukulipa’. Hakuna anayekuamini. Rika lako wanakuwa viongozi. Unaanza kuongozwa na vijana. Unaanza kuutafuta utulivu. Hupendi tena maeneo yenye kelele. Unaanza kuwaelewa wazee uliofikiri enzi hizo kuwa hawakuwa wapambanaji.
Mara umestaafu. Unatamani uendelee kuchapa kazi na mwajiri anakushangaa. Unawalaani watoto wako ambao nao wanashangaa upendo huu wa ghafla umeutoa wapi. Haikuwa kawaida yako. Unailaani serikali wa kusababisha ufarakane na familia yako. Unaulaani mfumo wa hifadhi ya jamii. Unawalaani viongozi wa dini kwa utapeli. Unalalamika muda wote. Unabaki kuwa mzee mpweke. Ukitazama nyuma unatamani ungepewa nafasi ya pili urekebishe makosa.
Tunajifunza nini? Hata sijui. Rudia tena kusoma utafakari kimya kimya. Ukweli mchungu ni kwamba maisha ni ‘mpandiano’ wa maamuzi madogo madogo, ambayo wakati mwingine, hayakupi nafasi ya pili kufanya marekebisho. Unaweza kuchagua aina ya maamuzi unayoweza kufanya leo (na hakuna mtu wa kukuingilia) lakini huwezi kuchagua matokeo ya maamuzi yako.
Zingatia haya mambo 10 katika maisha ( Ten commandments of life )
Namba 9 muhimu zaidi🙏
1. Usimsaidie mtu bila kuombwa msaada.
2. Lazima ujue kuwa adui wako makubwa ni miongoni mwa ndugu yako.
3. Rafiki wa kweli zaidi ni wewe mwenyewe tu.
Malengo kabla ya miaka 35:
• Tengeneza vyanzo 3 vya kipato,
• Kua na kiba ya miezi 6–12,
• Epuka madeni mabaya,
• Jifunze fedha na uwekezaji,
• Jenga Mtandao wa watu sahihi,
• Jenga Afya bora,
• Jenga ujuzi wenye kipato kikubwa,
• Jenga nidhamu ya kila siku,
Kama upo na +30 yrs; Ni muda sasa.
-Kupunguza ngano
-Kupunguza Sukari
-Kupunguza chumvi
-Kutoka jasho mara kwa mara
-Kuwa na mwenza unayemfurahia
-Kuwa na hobies angalau 3. 1.Inayokupa furaha. 2. Inayokupa elimu. 3. Inayoingiza pesa.