Mtu pekee unaetakiwa walau kumfkiria kumwachia asimamie biashara yako ni aidha awe amewekeza kikubwa au sawa sawa na ulichowekeza wewe kwenye hiyo biashara..
Hii ya kuchukua tu mtu kwasababu mnajuana unamwachia asimamie biashara yako imeliza wengi sana.
Anakuwa Hana uchungu.!!
Muogope sana mtu anaetoa pesa yake mfukoni kununua kitabu au course flani. Pesa ambayo alikuwa na uwezo kwenda kuilia nyama choma.!!
Muogope sana mtu uyo. Narudia Muogope sana.!!!
Assets sio tu sijui real-estate, stocks au bonds etc..
Kuna WATU pia tupo nao kwenye maisha yetu ni ASSETS. Kama zilivyo assets nyingine hawa ni wa kuwatunza sana.!!
Ni ngumu kuamini ila ndo ukweli,
Njia rahisi ya kupata unachotaka kwa mtu yoyote ni kum offer bure anachokitaka yeye.
Nipe nikupe ni kanuni ya maisha,
Next time ukitaka kitu kwa mtu, muulize kwanza yeye anashida gani, isolve then peleka swala lako.
Kitu cha msingi ni kuhakikisha ubongo wako upo active muda wote..
Kuna hii theory ya “use and disuse” kwamba kitu usipokitumia kina tabia ya kufa taratibu overtime..
Sasa usipotumia ubongo wako vizuri jua kabisa upo mbioni kuupoteza, utabakia kichwani lakini kama pambo tu.