#BreakingNews Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Emmanuel John Nchimbi, ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo baada ya kutafakari kwa kina. Ameeleza kuwa uamuzi huo ni wake binafsi.
Katika taarifa yake kwa umma iliyotolewa leo, Agosti 25, 2026, ikitumwa pia kupitia akaunti yake ya Instagram, Dkt. Nchimbi amesema ataacha nafasi ya Makamu wa Rais pamoja na utumishi wa umma kuanzia Septemba 4, 2026.
Dkt. Nchimbi amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini na kumpa nafasi ya kumsaidia katika uongozi wa nchi. Amesema amejifunza mengi kutokana na kufanya kazi na watu mbalimbali katika kipindi chake cha utumishi.
Amesisitiza kuwa uamuzi wake wa kujiuzulu hauhusiani na mabadiliko yoyote katika uhusiano wake na Rais Samia. Pia amemshukuru Mwenyekiti wa CCM kwa imani aliyokuwa nayo kwake.
Dkt. Nchimbi amesema ataendelea kuwa mwanachama wa CCM na kuitumikia Tanzania kwa nafasi nyingine atakayopewa.
#EastAfricaRadio #TogetherTunawakilisha
Mwanasiasa Zitto Kabwe amehoji kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, aliyesema kuwa hakuna mtu aliye juu ya sheria na kwamba yeyote anayevunja sheria atachukuliwa hatua.
Kupitia ujumbe aliouchapisha kwenye mtandao wa X, Zitto amesema bado hajashuhudia hatua zozote zikichukuliwa dhidi ya Katibu wa Baraza la Habari la Waislamu nchini Tanzania (BAHAKITA) Sheikh Said Mwaipopo, ambaye alitangaza hadharani kuunda kundi la kijeshi kinyume cha Katiba na sheria.
"Kwa makosa ya ukweli. Yule Mwaipopo aliyeunda kundi la kijeshi kinyume cha katiba na sheria hatujaona hatua yeyote dhidi yake! Yupo juu ya sheria? Kwanini hajakamatwa? Ndugu Rais @SuluhuSamia iponye nchi yetu. Turudishe 2021–2023. Hatua ya kwanza ni Tundu Lissu kuwa huru," ameandika Zitto.
Mbali na kuhoji hatua za kisheria dhidi ya Mwaipopo, Zitto amemtaka Rais Samia kuirejesha nchi katika mazingira aliyoyaeleza kuwa ya kipindi cha mwaka 2021 hadi 2023, akisisitiza kuwa hatua ya kwanza iwe kumuachia huru Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu.
Kauli ya Zitto imekuja baada ya Rais Samia, akifungua Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha Mawakili wa Serikali (TPBA) jijini Arusha, kusisitiza kuwa Tanzania inazingatia haki za binadamu na kwamba hakuna mtu aliye juu ya sheria.
Rais Samia alisema, "Tanzania tuko vizuri, waendelee kusema hakuna haki, tunavunja haki, lakini hakuna aliye juu ya sheria, akiongeza kuwa yeyote anayevunja sheria anashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.
🚨LEO TUNAAMKA NA HABARI KUBWA ANZA KWA KUREPOST.
COMMONWEALTH MINISTERIAL ACTION GROUP
WAMETOA RATIBA YA HATUA ZA UTEKELEZAJI KWA TANZANIA NDANI YA SIKU 30, 60 NA 90
Pamoja na mambo mengine Serikali haram ya Nduli Idd Amin Mama imepewa siku 30 iwe imetatua suala la kuzuiliwa kwa Mhe. @TunduALissu kupitia njia ya kisiasa na kisheria lakini pia kuwaachilia huru watu wengine wote wanaoshikiliwa kwa sababu tu ya kutumia haki zao za msingi kwa njia ya amani.
Ndani ya siku 60 wameambiwa warejeshe upatikanaji kamili wa majukwaa ya kidijitali (digital platforms) kusitisha vitendo vya vitisho na unyanyasaji dhidi ya vyombo vya habari na watetezi wa uhuru wa kujieleza.
Ndani ya siku 90 wahakikishe waitishe jukwaa la kuaminika na shirikishi la mashauriano kati ya vyama vya siasa, likiwa na wawezeshaji wasioegemea upande wowote yani Jukwaa hilo liwe na mamlaka ya kujadili na kukubaliana kuhusu marekebisho ya mfumo wa uchaguzi, ushindani wa kisiasa, suala la watu waliowekwa kizuizini na uwajibikaji.
Lakini pia wametoa Onyo la Septemba 2026 kwamba Tanzania imeamriwa kuwasilisha ripoti ya utekelezaji wa mambo hayo kabla ya mkutano maalum utakaofanyika Septemba 2026.
Onyo la Novemba 2026 (Hatua Kali): Jumuiya ya Madola imetoa onyo la mwisho kwamba isipoona maendeleo yoyote kufikia Novemba 2026, itachukua hatua kali zaidi dhidi ya Tanzania (ambayo kwa sasa tayari ipo chini ya uangalizi kwenye Agenda Rasmi
Acha kuendelee kuwaka.
TUTAKUWEPO🫵🏾😎
Rais wa Chama cha Mawakili wa Tanganyika (TLS), Wakili Boniface Mwabukusi, ameingilia kati mtafaruku mkubwa wa kisiasa unaoendelea ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), akiwaonya wanaharakati na wapenda demokrasia nchini kuacha mara moja propaganda za "kumchafua" Makamu Mwenyekiti wa chama hicho bara, John Heche, na viongozi wengine wakuu.
Katika mfululizo wa maandiko yake kwenye mitandao ya kijamii ndani ya saa 24 zilizopita, Mwabukusi amebainisha kuwa CHADEMA ni uwekezaji wa miaka 30 wa jasho la Watanzania na kwamba kampeni za sasa za kuwagawa viongozi wake kwa kauli za jumlajumla na mihemko zitalirudisha nyuma taifa ki-demokrasia kwa miongo minne ijayo.
“Kudharau na kuchochea mgawanyiko ndani ya CHADEMA kukifanikiwa kwa kuwagawa viongozi wao kwa kukosa staha na kuyumbisha muelekeo wake kisiasa, tutahitaji miaka mingine 45 kupata taasisi imara kama CHADEMA, CHADEMA hapo ilipo ni uwekezaji wa takribani miaka 30”, ameeleza Mwabukusi.
Kauli ya Mwabukusi inakuja kutokana na wiki moja ya sintofahamu iliyoibuka baada ya vikao vya Kamati Kuu ya CHADEMA vilivyoketi mkoani Kigoma Juni 30, 2026, ambapo kulienea tuhuma nzito za ufisadi wa mamilioni ya michango ya chama dhidi ya John Heche, tuhuma ambazo upande wa pili unadai ni mkakati wa kisiasa uliolipiwa ili kumshinikiza Heche aingie kwenye maridhiano na serikali na kusaliti msimamo wa Mwenyekiti Tundu Lissu ambaye bado yuko kizuizini.
Mwabukusi amewataka Wanachadema mitaani na mitandaoni kuheshimu taratibu za kiofisi za chama hicho kikongwe cha upinzani na kuacha kukiyumbisha kwa mashinikizo ya nje.
Aidha, Mwabukusi amekemea vikali tabia ya wanaharakati wa mtandaoni kushambulia viongozi waandamizi kama Godbless Lema na Joseph Mbilinyi (Sugu) kwa hisia au kusikiliza upande mmoja wa hadithi.
“Ni jambo baya kabisa kubeza nafasi na mchango wa Godbless Jonathan Lema au Joseph Mbilinyi (Sugu) kuwashutumu kwa kauli za jumlajumla hadharani, hii ni kushambulia demokrasia ya upinzani na maendeleo ya demokrasia ya mageuzi. Kama kuna kisa unashindwaje kuwasiliana nao kujua ukweli?”, amehoji.
Mnyukano huu wa maneno unakuja katikati ya propaganda nzito ambapo kada wa CHADEMA, Lembrus Mchome, na makundi ya watu mtandaoni walimshutumu John Heche kuficha michango ya chama na kushirikiana na wafanyabiashara wakubwa wa sekta binafsi kuvuruga mfumo wa uingizaji mafuta nchini. Hata hivyo, taarifa kutoka wandani wa chama hicho zinasema madai yote hayo ni propaganda.
Dola limekosea pakubwa kumshambulia @HecheJohn kama alikuwa na influence kwa 88% sasa wamei boost imekuwa 8888%
Hakuna kitu wananchi wanachukia kwa sasa kama mikakati ya dola ndani ya vyama vya siasa. Hakuna kitu wananchi wanachukizwa nacho kama kutengeneza migogoro ndani ya vyama vya siasa.
Bahati mbaya wanaofanya haya wengine tuliwaamini sana, bahati mbaya zaidi kuna dada zetu wanaongea kwa uchungu sana kwenye majukwaa lakini wameingia kwenye hii migogoro sababu za wahuni walio nyuma yao
Mwezi wa pili walimtanguliza Magere aanza kampeni kali sana ndani ya CDM kuyumbisha uongozi, mikwara mingi akisema kwamba akuzungumza sijui chama kitasambalatika ?
Watanzania wa sasa hakuna kitu tunataka sikiliza nje ya spana dhidi ya Samia na CCM, ujinga ujinga mwingine sio shughuli tunataka sasa. Focus ni CCM na vibaraka wake.
Kama kuna mtu anafikiria Heche anaweza kwamisha Lissu kutoka Gerezani basi amelamba sana asali za Samia
Hivi inawezekana vipi Lissu amefugwa na Samia, huyo Samia anamtesa Lissu gerezani, halafu eti Heche anaweza mtoa Lissu Gerezani ? Hii inawezekana vipi ? Heche pekee yake anaweza vipi hii shughuli ?
Lissu anaweza toleo gerezani na Samia mwenyewe au wananchi. Haya mengine ni maneno ya umbea na kuchonganisha watu.
Kama Heche akai kunywa bia na mtu au kufanya social activities hii inakuwaje kosa kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA ? Yaani mtu akiwa kiongozi wa CHADEMA anabadilishwa mpaka tabia kwamba kuna wale anywe nao bia , achukue nao mademu na akae kupiga nao story inakuwa lazima ?
Shutuma za kiongozi wa taasisi yoyote ile inatakiwa iwe ya kuvunja katiba na taratibu za chama, mambo social sio lazima mazingira yenye haya sio salama, why kushinikiza issue social nyakati ambazo kuna hatari nyingi mbele yetu ?
Heche amefiwa na dereva wake wa muda mrefu, kama nyie social kwenye mbona msibani amkufika? Kwamba sawa huyu jamaa analinga na nyie msiokwenda mpaka kwenye msiba ? Ndio tuje wawaamini mna nia njema wakati tunaona matendo ya chuki kali ?
Mimi nasubiria kuona tu wana CHADEMA watakipigania vipi chama chao dhidi ya wahuni wote wanatenda haya matendo ya kufitinisha na kutesana ili kikatishana tamaa.
CHADEMA inaweza pambana na hawa wahuni wote hiyo naamini kabisa na wanajulikana
Ni muhimu pia kwa vyama vya siasa kutenganisha majukumu ya utendaji wa kila siku ( viongozi wa Taifa na Kanda) hawa wana majukumu ya kila siku , Watu wa kamati kuu wakiingia kwenye majukumu ya kila siku ni kuchochea migogoro na kuondoa accountability, Kamati kuu ni kama jicho la CHAMA, kama mtu hana cheo kinachompa majukumu ya kila siku anakuwa kwenye shughuli za kila siku za chama ? Hapo secretariat ya CHAMA itafanya mambo gani ? Choreni mstari mapema na ondoe utaratibu wa kuwapa majukumu ya kila siku watu ambao jukumu lao ni accountability yaani jicho, ili wafanye kazi zao kwa usahihi .
Na itapunguza sana hii agenda ya kificho ya maridhiano, anaye taka maridhiano aende Ukonga kwa Lissu
Fikiria leo kuna viongozi wanaandikwa vizuri na Yericko ?!!!!
Viwanja vya Mtekelezo, Dodoma Mjini.
CHADEMA tumekusanya TONE TONE TZS 3,209,200. RUZUKU ya kiwaki HATUTAKI. CHADEMA ni mali ya UMMA na itaendeshwa na WANANCHI. Angusha TONE lako kuwezesha mikutano mingine kupitia 0744 446 969; Jina - CHADEMA HQ. #PeoplePower. 👊🏾
“Kumekuwa na majaribio na vitisho kutoka kwa watawala kunizuia nisiongee. Kuna wakati niliambiwa nizime simu yangu, nisiitumie mpaka (wao) watakapo niambia. Nikawauliza, kwa sheria gani? Kuna wakati nilikaribishwa mahali fulani, nikapigiwa simu na watawala, wakasemam mzee usiendee kwenye huo mkutano. Kwanini? Hauna manufaa. Nikawauliza, nani anaamua hayo manufaa? Nikakataa. Wakawafuata watu walio karibu na mimi ili wanishawishi nisiende, nikakataa pia. Mnakumbuka nilifanya mahojiano hapa na Jamhuri? Wakatoa summary, wakasema watachapisha mahojiano yote, neno kwa neno. Baadae Jamhuri wakanieleza wamezuiwa wasitoe yale mahojiano. Kuna viongozi wanaogopa kuzungumza na mimi, wanatuma ujumbe kupitia mbali huko. Marafiki zangu wanaogopa wakisema nitatekwa au kupewa sumu. Nawaeleza mimi ni mali ya Mungu, ndiye atakayeamua lini ananihitaji.”
— Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais Tanzania.
Usiwafanyie watu mabaya tu, bali pia usiwatamanie mabaya mioyoni mwako. Maana dunia ina mzunguko—unayotenda au kutamani kwa wengine, nayo hukurudia. Chagua wema kila wakati. 🙏
HAKIKA RC MTAKA UAMINIFU umetupiga chenga. TUTATESEKA sana . Tunaambizana uongo hata kwa yale yaliyo wazi kwa wengi kwamba yalitokea. Hivyo hasira zinapanda, vidonda vinatoneshwa upya badala ya kupona. Halafu tunadanganyana tutaliponya taifa?. HOW?? Kwa kutafuta kafara badala ya KUTUBU NA KUJIREKEBISHA?
Yes kwa sababu mmezingua sana, yaani mmejivunjia hata heshima ndogo mliyokuwa mmebaki nayo kama WAZEE…Mmelisaliti Taifa na kuliongezea maumivu mioyoni kwa kutoa ripoti ya ovyo ya KUBUMBA!
Baadhi ya wajumbe walioshiriki katika kura za maoni za uteuzi wa mgombea ubunge Jimbo la Isimani wameibuka na malalamiko wakidai kutoridhishwa na mchakato uliotumika kuwashindanisha wagombea hao.
Wajumbe hao wamesema kuwa kuna viashiria vinavyoibua wasiwasi juu ya uwepo wa rushwa katika mchakato huo hali ambayo imeathiri matokeo yaliyopatikana kwa makada watatu walioongoza kura hizo za maoni.
Aidha wamelalamikia kukosekana kwa fursa kwa wagombea kujinadi sera zao mbele ya wajumbe wakieleza kuwa wengi wao hawakuwa na ufahamu wa kutosha kuhusu wagombea hao kabla ya kupiga kura.
“Imekuwa jambo la kushangaza kuona baadhi ya wagombea wakipata ushindi wa kishindo ilhali wajumbe wengi hawawafahamu wala hawakusikia sera zao,” amesema mmoja wa wajumbe aliyeshiriki zoezi hilo.
Kutokana na hali hiyo wajumbe hao wamekitaka Chama kurejea mchakato huo kwa maslahi mapana ya chama ili kuhakikisha haki inatendeka na taratibu zote zinazotakiwa ikiwemo wagombea kujieleza na kujibu maswali ya wajumbe zinafuatwa kikamilifu.
Wamesisitiza kuwa kurejewa kwa kura hizo za maoni kutasaidia kurejesha imani ya wanachama na kuhakikisha kuwa mgombea atakayepatikana anawakilisha kweli matakwa ya wajumbe.