JESHI LA POLISI LIMEVAMIA NYUMBANI KWA MBYELLA (ANAYEUZA NGUO NA VIFAA VYA CHADEMA NA KUONDOKA NA TSHIRT, KOFIA, NGUO NA BENDERA ZA CHADEMA.
Nimepata taarifa kwamba usiku wa kuamkia leo mida ya saa nane, Jeshi la Polisi limevamia nyumbani kwa Yoromu Mbyella, mfanyabiashaa ambae huwa anauza sare za CHADEMA wakidai wanamtafuta kwa kosa la kutengeneza Tshirt zenye maandishi “FREE TUNDU LISSU”
Kwa mujibu wa mtoa taarifa, Mbyella mwenyewe hakuwepo nyumbani so Polisi walifanya upekuzi na baada ya kumkosa waliondoka kwa muda.
Baadaye walirejea wakiwa na Gari aina ya Fuso kisha wakabeba nguo zote na vifaa vyenye nembo ya chadema ikiwemo Bendera za Chadema ambazo huwa anauza kisha wakaondoka na mali hizo bila kutoa sababu zaidi.
Kwa mujibu wa mke wa Mbyella (anayeuza nguo na vifaa vya chama) nyumbani kwao kuna duka la kuuza vifaa hivyo ambavyo Polisi wameondoka navyo vyote.
Tunafuatilia kufahamu sababu hasa ya kuvamia nyumbani hapo na kuleta taharuki kwa mtu ambaye hata kama wangemhitaji Polisi, wangempatia wito na angefika kituoni kama Polisi walikuwa na jambo na Mbyella.
Kuuza vifaa vya chama kama nguo, kofia, Bendera siyo kosa kisheria.
REPOST 200
Tundu Lissu ambaye yupo ndani ya kuta za gereza Ukonga asingeweza kwa njia yoyote ile kumtafuta Dr. Chakwera
Kwa hiyo hapa hoja ya nani alimtafuta mwenzake it’s obvious ni Chakwera ndiye aliyemtafuta Lissu ama kwa maelekezo, au utashi binafsi.
Kauli ya Lissu “Nipo tayari kwa mazungumzo nikiwa huru”
Kwa wasioelewa hii ni lugha yangu kisheria kuhusu makubaliano.
Makubaliano yanayotambulika kuwa halali kisheria ni yale yanayofanyika under FREE and genuine consent. Neno FREE hapo linasimama likimaanisha FREE from COHESION or UNDUE INFLUENCE
Lissu anaamaanisha kuwa, kwa yeyote anayetaka kuzungumza na yeye kuhusu lolote, asifanye hivyo wakati Lissu kwa kutumia ukosefu wa Uhuru wa Lissu kama UNDUE INFLUENCE kuchagiza maamuzi yake.
Kwa hiyo kwa ambao hamjaelewa, Lissu bado amekaza kutuuza kwa mazungumzo yenye ushawishi wa kumpa Uhuru.
Lissu anataka UHURU KWANZA ndipo umpelekee hoja mezani aamue kukubali au kutokubali akiwa HURU.
Lissu hajataka akatokee Ikulu.
Anataka atokee kwenye malango ya Ukonga. Sio kwa huruma, bali on merit either kwa serikali kufuta kesi yake yenyewe ambayo mpaka sasa wameipakisha basi kwa Pilato bila sababu, au hukumu ya NOT GUILTY.
Nimeona mnajimu mmoja wa mizimu anatafsiri tofauti ikabidi niweke sawa.
Yours,
The Hoofman