Sasa hivi wanawake hatuko salama, anatekwa mume hujakaa sawa na mama na wewe unakamatwa watoto wanabaki bila wazazi. Hata huko kwenye vita watoto na wanawake huwa wanapewa ulinzi. Tumefika pabaya sana.
#FreeJanethRithe#FreeJanethRithe#FreeJanethRithe
DOROTHY SEMU: FEDHA ZA UCHAGUZI MKUU ZISITUMIKE KUMINYA DEMOKRASIA
Chama cha ACT Wazalendo kimeitaka Serikali kuhakikisha kuwa fedha za umma zinazotengwa kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 hazitumiki kuminya demokrasia wala kupora haki ya wananchi kuchagua viongozi wanaowataka kwa uhuru.
Akizungumza leo Juni 21, 2025 katika Makao Makuu ya ACT Wazalendo Magomeni, Dar es Salaam, wakati wa uchambuzi wa Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2025/26, Kiongozi wa chama hicho, Bi. @SemuDorothy, alisema kuwa tayari shilingi bilioni 741.5 zimetumika kati ya shilingi trilioni 1 zilizotengwa kwa uchaguzi, huku bilioni 378.2 zikitarajiwa kutumika kwa mwaka huu wa uchaguzi.
โFedha hizi ni mali ya wananchi wa Tanzania, si mali ya CCM wala chama chochote cha siasa. Zinapaswa kutumika kwa minajili ya kuwezesha uchaguzi huru, wa haki na unaoaminika, si kwa ajili ya kuumiza, kubughudhi au kupora maamuzi ya wananchi,โ alisema Dorothy.
ACT Wazalendo imetolea mfano wa matumizi ya zaidi ya shilingi bilioni 254.82 kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2019, ambao ulitawaliwa na vitendo vya kuvunjwa kwa haki na misingi ya kidemokrasia. Chama hicho kimesema kuwa hali hiyo bado inaendelea hadi sasa.
โTunaelekea tena kwenye uchaguzi bila matumaini ya haki na demokrasia. Tumeamua kuingia kwa ari ya mapambano โ si ya vurugu, bali ya kulinda thamani ya kura za wananchi wetu,โ alisisitiza Bi. Dorothy.
Katika mkutano huo na waandishi wa habari, ACT Wazalendo ilitoa msimamo wake na kusisitiza madai makuu sita kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025:
1. Makamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wapatikane kwa ushindani wa wazi na mchakato wa usaili uanze mara moja kama sheria inavyotaka.
2. Wakurugenzi wa Halmashauri wasiwe wasimamizi wa uchaguzi katika majimbo. Tume iajiri wasimamizi huru wa uchaguzi.
3. Mawakala wa vyama wafanye kazi bila bughudha wala vizuizi.
4. Wagombea wote wapewe fursa sawa na wasienguliwe kwa visingizio visivyo na msingi.
5. Kura feki zipigwe marufuku, na fedha za umma zisitumike kuchapisha kura za wizi.
6. Vyombo vya ulinzi na usalama visiingilie mchakato wa uchaguzi kwa namna yoyote.
ACT Wazalendo pia imetoa angalizo kali kwa Serikali dhidi ya matendo yoyote yatakayolenga kuhodhi au kuharibu mchakato wa uchaguzi. โTume ya Uchaguzi si mali ya CCM, na fedha za umma hazipaswi kutumika kuibeba chama kimoja. Zinapaswa kutumika kuhakikisha haki inatendeka kwa Watanzania wote,โ aliongeza Dorothy.
Chama hicho kimetoa wito kwa Watanzania kutumia hasira na masikitiko yao dhidi ya utawala wa CCM kama chachu ya kushiriki kikamilifu kwenye uchaguzi, kupiga kura na kuzilinda.
โTumejidhatiti kuongoza mapambano ya kulinda demokrasia. Tunawaomba Watanzania wote tuungane kukataa ufedhuli wa Serikali ya CCM inayotudumaza kiuchumi, kijamii na kisiasa,โ alihitimisha Dorothy Semu.
Kitendo cha @tanpol kuendelea kumshikilia mwenyekiti wa wanawake Taifa @ACTwazalendo ni Unconstitutional hatuwezi kuendelea kua kwenye taifa ambalo linaendeshwa kwa utashi bila ya kufuata sheria, Polisi wamuachie @JaneRithe bila masharti yeyote. #FreeJaneRithe
Katika bajeti ya mwaka wa fedha wa 2025/26 Serikali imetenga fedha ndogo kwa ujenzi na matengenezo ya barabara. Aidha madeni kwa wakandarasi yanadumaza kasi ya ukamilikaji miradi."
Waziri Kivuli wa Uchukuzi
@HalimaYusuf_N
Oktoba #LindaKura
Chama cha ACT Wazalendo kimelaumu Serikali kwa kushindwa kusikiliza kilio cha wastaafu kuhusu marekebisho ya kikokotoo cha mafao ya pensheni kwa watumishi wa umma na sekta binafsi. Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri Kivuli wa Uchukuzi, Halima Nabalangโanya, katika mkutano uliofanyika Makao Makuu ya chama hicho Magomeni, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Nabalangโanya, mfumo wa sasa wa kikokotoo unaotumika kwa wastaafu wanaochangia mifuko ya PSSSF na NSSF unawapunja kwa kiwango kikubwa, huku akibainisha vipengele vinne kandamizi vinavyochangia hali hiyo.
โMfumo huu unapunguza mafao kwa wastani wa asilimia 60 kutokana na asilimia ya malipo, kutumia kipimo cha 1/580 badala ya 1/540 kunapunguza mafao kwa zaidi ya asilimia 7, na pia kutumia wastani wa mishahara mitatu ya mwisho badala ya mshahara wa mwisho kunapunguza mafao kwa asilimia 7.2. Aidha, kupunguza muda wa kuhudumu kwa pensheni kutoka miaka 15-5 hadi 12.5 kunazidi kuwanyima haki wastaafu wetu,โ alisema.
ACT Wazalendo imesema hatua hii siyo tu inawapunja wastaafu, bali pia inaendeleza ubaguzi kati ya wafanyakazi wa sekta binafsi na wale wa serikali, hasa wanaohudumiwa na mifuko tofauti ya hifadhi ya jamii.
Chama hicho kimetaka kurejeshwa kwa mfumo wa zamani wa kabla ya mwaka 2018, uliokuwa unatoa mafao ya mkupuo kwa asilimia 50 na kutumia kikokotoo cha 1/540, huku mstaafu akipewa mafao kulingana na umri wake wa kuishi badala ya muda uliodhibitiwa.
Pia ACT Wazalendo imekosoa Serikali kwa kushindwa kumaliza deni la wafanyakazi waliostaafu kabla ya mwaka 1999. Nabalangโanya amesema kuwa katika deni la trilioni 4.46 ambalo PSSSF inadai, Serikali imelipa trilioni 2.18 pekee, hali inayosababisha mfuko huo kushindwa kulipa wastaafu kwa wakati na kushindwa kuwekeza kwenye miradi ya maendeleo.
โHaiwezekani Serikali inapanga kulipa bilioni 630 tu. ACT Wazalendo tunaitaka Serikali kulipa deni lote kupitia mfumo wa hati fungani, ili kuimarisha PSSSF na kuhakikisha wastaafu wanapata haki yao kwa wakati,โ alisisitiza Nabalangโanya.
Kauli hii inakuja wakati kukiwa na malalamiko ya muda mrefu kutoka kwa wastaafu na vyama vya wafanyakazi kuhusu hali ngumu ya maisha baada ya kustaafu na ukosefu wa mfumo wa hifadhi ya jamii unaolinda utu wa wazee.
@Ndolezi_Petro Kaka sababu za kiusalama tu ambazo zilikua nnje ya uwezo wangu, zilinipa likizo ya muda kidogo kwenye mitandao ya kijamii
Ila tupo pamoja sana kaka
Mbunge Mstaafu CUF Mtwara mjini, Makamu Mwenyekiti Chama Cha Wananchi CUF Leo June/19/2025 ameitikisa kusini. Karibu sana @ACTwazalendo chama kilichobeba matumaini ya suluhu ya matitizo ya watanzania. #Octobar#Tunalinda KURA
HABARI PICHA:
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mtwara Mjini na Makamu Mwenyekiti wa chama cha CUF, Maftaha Nachuma amekihama chama hicho na kujiunga na chama cha ACT Wazalendo.
Maftaha amekabidhiwa kadi ya ACT Wazalendo na Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho bara, Isihaka Mchinjita kwenye kongamano la kumpokea lililofanyika katika Ukumbi wa Kanisa la Pentekoste Mtwara tarehe 19 Juni 2025.
Kuna namna chama changu kinaimarisha kikosi chetu kuelekea uchaguzi mkuu wa october i am impressed, wacha tumalize Fungate tuingie mzigoni. #OktobaLindaKura