Kuna mtu anasema maumivu ya hawa watu ni kwasababu ya Nongwa ya Rais kutoka Zanzibar!!!!
Kwamba hawa watu wanalia kwasababu tu ya Nongwa sio?
Na huo ndio msimamo wa taasisi yenu?
Magufuli tuliempinga kwa udikteta a ukatili wake mpaka akafanya jaribio la kumuua Lissu alikua anatoka Zanzibara pia au?
Tunazidi kufahamiana.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 297
Ajuaye: Ulitoa taarifa sasa wewe polisi?
Mhe. Lissu: Ilikuwa ni miezi sita kabla ya uchaguzi. Natoaje taarifa polisi wakati siku kwenye mkutano wa kampeni na nilishakwambia sikuwa nafanya public meeting.
Ajuaye: Soma kifungu cha 23 cha Political parties act
Mhe. Lissu: Soma wewe uliza swali.
Ajuaye: anakisoma je ulitoa taarifa
Mhe. Lissu: Siwezi kutoa taarifa mikutano ya ndani. NEXT?
Ajuaye: Kifungu kinasema public place or any other area
Mhe. Lissu: Hujui wewe hata kusoma kingereza kifungu kinasema public meeting conducted at any area. Sasa wewe umesoma shule gani Dada angu?
Ajuaye: Tulia kwanza. Una kifungu chochote kinachosema unaweza kufanya mkutano wa ndani bila kibali?
Mhe. Lissu: Hicho hicho kifungu cha 23 cha Sheria ya Vyama vya siasa.
Ajuaye: Maneno ya kukinukisha uliyakubali hata kama video hatujaleta?
Mhe. Lissu: Sikuongea maneno ya Uhaini mimi.
Ajuaye: Ni ukweli kwamba hata kama video haikuletwa lakini uliongea maneno ambayo yapo kwenye hati ya mashitaka?
Mhe. Lissu: Maneno niliyoshitakiwa kwamba yalikuwepo kwenye video yalikuwa ya masaa matatu hayakuwa ya uhaini.
Ajuaye: Video ni kifaa kilichobeba maandishi?
Mhe. Lissu: Kumbe iko hivyo? Mimi sijui.
Ajuaye: subiri nikiwa mshitakiwa au shahidi utaniuliza. Nitakuomba uwe Wakili wangu?
Mhe. Lissu: Siwezi kuwa na mteja kama wewe ambae anasingizia singizia watu makosa.
Ajuaye: ni kweli mahakama ndio inaweza kusema mtu fulani amefanya kosa fulani?
Mhe. Lissu: Itasema kama mtu huyu atakuwa amepelekwa mahakamani.
Ajuaye: Nani anasema walikamatwa kwasababu walikuwa na makosa?
Mhe, Lissu: Walikamatwa bila kuwa na makosa.
Ajuaye: Ulisema kama ukamataji wako ulikosewa?
Mhe. Lissu: Nilisema na Kiswaga aligoma kuandika na hapa nilisema kwenye mahakama hii.
Ajuaye: Ni very serious allegation hizo
Mhe. Lissu: Ndio ndio maana nilileta mahakamani na wewe ulikuwepo siku ile. Uliona.
Ajuaye: Wanaosimamia sheria ya uchaguzi ni serikali?
Mhe. Lissu: Sheria ya Uchaguzi inasimamiwa na Tume ya Uchaguzi. Na tume ya Uchaguzi sio Serikali.
NB. Leo nimeshuhudia ni kwa kiwango gani TAIFA lina Mawakili wa Serikali ni VILAZA.
Ajuaye: Kupinga uchaguzi ni takwa la kisheria?
Mhe. Lissu: Sisi tulikuwa tunataka uchaguzi usifanyike kabisa. Mambo ya kupinga hata kwenye uchaguzi halali kuna kupinga matokeo ya uchaguzi.
Anakuja askari wa Magereza huwa ni mnaa mnaa sana. Mnoko sana. Amewafuata mawakili wa serikali kwasababu imefika saa 11 na nusu kwa sasa.
Wanajadili mawakili wa Serikali muda huu.
Mhe. Lissu: Ule utaratibu wa kuishia saa 11 kamili vipi tumeubadilisha.
Jaji Ndunguru: Tulidhani wanamaliza maswali yao ndio maana tukawa tunawaangalia tu. Sasa ngoja tuwaulize. Upande wa serikali mnasemaje?
Ajuaye: Basi tuahirishe hadi kesho.
Jaji Ndunguru anateta na wenzake.
Sasa tukutane kesho asubuhi kuendelea.
Naomba Repost yako.
Mwalimu Nyerere once said this to Tanzanians. 🇹🇿
His words remain relevant today and remind us of the importance of unity, justice, dignity, and responsibility to our nation.
Let us listen, reflect, and learn from his wisdom. 🇹🇿✊🏽
👏🏽 Lissu kanyoosha na katusanua 👇🏾 leo mahakamani
Katuga: Sasa iambie mahakama demokrasia unayoifahamu wewe kila mtu ana haki ya kufanya anachoona kinamfaaa kwamba siku ya kupiga kura aende anayetaka na asiyetaka asiende. Ni sahihi?
Tundu Lissu: Demokrasia yangu mimi inasema ukiwa hutaki jambo chukua hatua kulizuia kwa njia halali ndio maana maandamano yameruhusiwa kisheria.
Katuga: Demokrasia ipi hiyo?
Tundu Lissu: Katiba inasema ukifanya maandamano na kuuzuia uchaguzi ni demokrasia kabisa. Niambie wapi sheria imekataza?
Katuga: Haya sawa mjanja wewe.
#FreeTunduLissu
#FreeTunduLissuNow
Wapendwa,
Nafikiri tumebakiwa na hatua moja tu kufikia lengo letu. Hebu fikirieni, kama kila mmoja ambaye tayari ameshachangia ataamua kutoa tena mchango wa kiwango kilekile alichotoa mwanzo, basi kufikia kesho tutakuwa tumekamilisha asilimia 100 ya mahitaji ya fedha za Baraza Kuu.
Hii ndiyo roho ya Tone Tone haswa Weekend hii, hatuhitaji mzigo mkubwa kutoka kwa mtu mmoja, bali moyo wa pamoja kutoka kwa wengi.
Tukiamua, tunaweza. Tukisimama pamoja, tunafika.
Asanteni sana kwa kujitoa, mshikamano wenu, na kuendelea kuamini katika wajibu huu mwema.
TONE TONE WEEKEND MISSION
“Kila tone lina thamani; pamoja tunatimiza kusudi.”
Barua ya Tundu Antiphas Lissu si maandishi ya kawaida, ni kengele ya hatari. Inatukumbusha kuwa haki inapocheleweshwa, si tu inaumiza, bali hugeuka mateso ya wazi. Wananchi, tusijidanganye. Ukimya wetu si neutral Bali ni upande ktk kukumbatia dhuluma. Kila tunaponyamaza, tunatoa nafasi kwa dhuluma kuendelea. Kila tunaposita, tunadhoofisha nguvu ya haki.
Je, tutakubali kuwa watazamaji wa historia, au washiriki wa mabadiliko? Kama mbinu zetu hazifanyi kazi, zibadilishwe. Kama sauti yetu haisikiki, ipazwe zaidi. Haki haiombwi kwa sauti ya chini , hudaiwa kwa msimamo thabiti. Huu si wakati wa hofu wala kusubiri wengine wachukue hatua. Ni wakati wa kila mmoja kusimama na kusema inatosha.Kwa sababu ukweli uko wazi, haki ya mmoja inapovunjwa, msingi wa haki ya wote unatetereka. Na jamii inayokubali hilo, hujijengea hatari yake yenyewe. Simama. Ongea. Chukua nafasi yako. Wakati wa haki ni sasa.
Shirikisho la Soka la Guinea limeitaka CAF kuhakiki Kombe la Mataifa ya Afrika la 1976, likidai kuwa taji hilo linafaa kutolewa kwa Guinea kufuatia Morocco kujiondoa wakati wa mechi .
Mnamo 1976, Guinea ilikuwa inaongoza Morocco 1-0 kupitia kwa Chérif Souleymane, kabla ya wachezaji wa Morocco kutoka uwanjani mfupi kupinga uamuzi wa Mwamuzi.
Baadae Morocco ilirudi uwanjani na Ahmed Makrouh alisawazisha katika dakika ya 86, na mchezo kumalizika ikiwa ni 1-1.
Morocco waliongoza kundi hilo wakiwa na pointi tano na kutwaa ubingwa, huku Guinea wakimaliza nafasi ya pili.
Guinea inasema kuvuliwa taji kwa Senegal la AFCON 2025 hivi karibuni na kuipendelea Morocco ni mfano wa
Guinea ikisema tukio hilo linafaa kutathminiwa tena kwa kutumia kanuni zilizotumika katika uamuzi wa 2025.
#KitengeUpdates
Eid ni zaidi ya sherehe, ni kumbusho la uadilifu, ukweli, na haki. Ni wakati wa kujenga uaminifu, na kuanza maisha mapya yenye furaha na baraka.
Eid Mubarak! Furaha, amani, na baraka ziwe nanyi siku hii na siku zote.
Hii ndo maana ya #WenyeNchiWananchi
Na tukisema haya mnataka kututoa roho - ninyi wauaji mna roho ya kishetani - ila Ukweli lazima usemwe!
Kesho mtaona Abdul na genge lake wanakuja na njama nyingine ya kipumbavu kutaka kumdhuru Fr Kitimw tena! Pumbaf sana hawa jamaa
#TutaelewanaTu
Nilichokielewa kwenye KATUNI YA KIPANYA LEO.
Hapo kuna Bendera ambayo inapepea juu kabisa ya mlingoti hiyo ni ishara ya UHAI wa chama. Ingepepea nusu mlingoti basi ingekuwa ishara ya mauti kwa chama.
Bendera iliyochakaaa-huu ni ujumbe kwamba CHAMA kimepitia dhoruba nyingi lakini bado kipo imara kinaendelea kuwakilisha wanyonge.
Na huu ni ujumbe kwa WAKOLONI WEUSI ambao wamewekeza mabilioni kwenye kuendesha KESI za uongo dhidi ya Chadema ili chama kife ila bado chama KIPO IMARA.
Huu ni ujumbe kwa WAKOLONI WEUSI baada ya kutumia mabilioni kuibomoa CHADEMA kwa kuwagawa na kuzusha uzushi kila siku lakini bado chama KIPO IMARA.
Huu ni ujumbe kwa WAKOLONI WEUSI ambao wanatumia mabilioni ya mapesa kuendesha Kesi dhidi ya mwenyekiti TUNDU LISSU kwa miezi 11 sasa lakini bado chama kipo imara.
Huu ni ujumbe kwa WAKOLONI WEUSI ambao kutwa wanateka watu wa CHADEMA kwa hoja zao na ukosoaji wao kama njia ya kuwatia woga wengine ila bado wananchama na watanzania wapo imara na chama chao.
MUNGU ANAYO MAKUSUDI NA HIKI CHAMA-HIKI CHAMA NI MPANGO WA MUNGU.
TUTAKUWEPO🫵😎
Nina wasiwasi mkubwa kuwa hakuna muda mrefu video hii itakuwa haionekani ktk kurasa mbali mbali za Online TV. Sijui itakuwa ni kwa amri ya nani ? Lakini just watch.
DEAR TANZANIA: OPEN LETTER TO THE LAND & THE PEOPLE
Kama Mtoto wa Tanganyika, ambae kitovu chake kimetupwa fukwe za Bahati ya Hindi na mwenye ndui begani, nalazimika kuongea na wewe, TANZANIA…
Tanzania ni ARDHI, WATU, RASILIMALI na KATIBA. Sijaiweka Serikali kwa sababu baada ya October 29th, kwa mujibu wa Katiba, HATUNA SERIKALI, hivyo iliyopo ni HARAMU.
Nimekuwa na Wakati mgumu sana kuendelea na maisha ya kila siku, baada ya matukio yale, na AFYA YA AKILI ilipitia mtihani mkubwa baada ya Matendo na Maneno ya “Viongozi Haramu” kuendelea kutawala, bila dhamira, majuto wala uwajibikaji.
LAKINI TUMEWAJUA Watesi, Wanyonyaji, Waroho wa Madaraka, Wavunja Agano (Katiba, Sheria & Haki za Binadamu), Waoga na Wabinafsi. Ni dhahiri Walitukosea, Wanatukosea na Wanaendelea kutukosea; Wanawakosea Watu, Wanaikosea Ardhi, Wanaikosea Katiba.
Ni rahisi, kuamua kunyamaza na kusema Maisha ya Endelee. Ila amini kwamba. WAO WAMETENDA DHAMBI, ILA DHAMBI KUBWA KULIKO YAO ITAKUWA NI SISI KUSAHAU NA KUKAA KIMYA. Ni kweli Mahakama ni zao, Bunduki ni zao, Jela ni zao, Askari ni wao ILA SAUTI YA MWENYE HAKI NI MIGHTIER THAN ALL THOSE, and Justice may be delayed but it always prevails. Cheza nafasi yako kadri utakavyoweza, bila shinikizo la nje bali Msukumo wa Ndani.
Naomba Samahani kwa wote mliokuwa mnanitafuta na hamnipati. Changamoto was real, ila nashukuru nimepata namna ya ku-move forward. Wengi walishangaa ukimya, ila taratibu nimeanza kurudi to my old self (kidogo Twitter nimejitahidi, ila it hasn’t been easy).
Ahadi yangu ni kwamba, narudi kwenye maisha yangu ya kawaida ila sitokaa kimya kamwe kwa Matamko, Analysis na Muziki! I OWE THAT TO THE LAND and THE PEOPLE, especially those who died in October 29th - November 2nd, and THOSE WHO WERE ABDUCTED AND ARE STILL MISSING
Happy Valentine’s
The Leader
Jana tulikuwa na mazungumzo kuhusu Siku ya historia ya VALANTINE DAY.
Mke wangu aliniuliza, Hivi Godbless , ungependa Brilliant (Binti yetu) aolewe na mume mwenye tabia kama zako ?
Nikajibu faster , aolewe na mtu kama Yesu !!
Akacheka 😂😂😂Bro, acha kurukaruka, Yesu hakuoa!!’ Nakuuliza wewe !!
Mbona jibu rahisi sana ?
Nikajibu, nahitaji marekebisho kidogo na maombi kwa sasa kwanza!!
Akasema, Awake your spirit Godbless, ikiwa wewe ni baba na hauwezi ku recommend mtoto wako aolewe na mwanaume mwenye tabia kama zako basi iko shida!! Bahati nzuri wakati stori zinaendela , Bon Yai alipiga simu , nikaenda pembeni nikasema naona kuna simu ya kikao, nikawa nimepita hivii , nikamwambia Ney , unajua Lissu kanyimwa chakula huku nikiwa nimekunja uso !! Ney , hawa CCM ni sadist sana!! Nikajiongelesha !!
Okay !! Sasa na wewe mwanaume mwenzangu nakuuliza kama nilivyo ulizwa? Je , ungependa binti yako aolewe na jamaa mwenye tabia kama zako ?
Kama jibu ni hapana !! Badilika !! Tubadilike!!
Unajua sisi wanaume tunapenda sana kulaumu wanawake kwa kuchagua mwanaume asiye sahihi, lakini kamwe hatumlaumu mwanaume aliyeficha utu wake wa kweli na kujifanya mtu mwingine ili ampate mwanamke mwema. Hatari kubwa sana hii.
Nawatakia Siku Njema ya Wapendanao.