Benjamin Fernandes' fintech, Nala, helps 500,000 Africans working abroad send money back home. Now he's aiming to build a cross-border payment system for multinationals doing business in Africa. https://t.co/W1QSDkwLnf
" Tusichanganye Dini na Siasa " Baada ya hii kauli kutoka kwa Rais Mst Mh J.Kikwete kumekuwepo na FIKRA tofauti ktk mjadala.Pengine ni kwa sababu ametoa kauli wkt TEC wametoa waraka wao kuhusu uwekezaji bandarini otherwise ni kauli nzuri.Swali ninalo jiuliza hata mimi , Je,ni muda gani sahihi wa kusema ukweli na ni muda gani sahihi wa kuficha ukweli ?Pili , Je,Viongozi wa CCM wanayo legimacy ya kusema maneno haya wkt CHAMA chao ni mafundi wa " Divide and rule".Lakini naamini pia JK anaweza kuwa ameona trend ya mwelekeo wa Nchi haswa kwa watetezi wa uwekezaji wa bandari toka mjadala huu kuanza na akafikiri asikae kimya zaidi wkt mpasuko unaendelea kuwa mkubwa.CCM kwa miaka yote wamekuwa wakitumia kila njia kugawa watu kwa maslahi yao.Wkt CUF Inaimarika miaka ya nyuma CCM walipita Makanisani kwa Wakristo wakiwaambia kuwa CUF ni Chama cha Waislamu na wana malengo mabaya dhidi ya Wakristo. Wakristo wengi walijitenga na CUF kwa sababu ya Propaganda hii.Wkt huo IGP Mahita (Mwislamu) alitengeneza propaganda feki ya kontena la majambia limeshikwa bandarini mali ya CUF kuja kuteketeza Wakristo.Hiyo kesi sijui imeishia wapi mpaka leo.
Wkt CHADEMA inaanza kuimarika. CCM waliingiwa hofu,wakaendelea na kazi tena ya kugawa watu, wkt huu ilikuwa " CHADEMA Chama cha Kaskazini/Wakristo" CHADEMA tulipingana na proganda hii ambayo ilifanywa na viongozi waandamizi na machawa ndani ya CCM kwa nguvu zote na wkt Dr Slaa anagombea Urais ilianzishwa kampeni chafu kuisaidia CCM na Rais JMK iliyopewa jina " Kura ya Maslahi" Niliongea jambo hili baada ya Uchaguzi ndani ya Bunge na kulikemea.Nilitakiwa kuthibitisha kauli zangu ndani ya Bunge, Spika Anna Makinda alinipa siku saba , mimi niliomba dakika saba tu, nitoke niende hotelini nilete ushahidi, Anna Makinda akashituka ,kuna watu wakatumwa kwangu niweze kuwaonyesha ushahidi nilionao baada ya kutazama kirefu niliombwa niachane na hiyo hoja na watamweleza Spika kuwa wamefanya hivyo kwa maslahi mapana ya Nchi.
CCM tena ,wakati wa Bunge la Katiba CCM hawakuchoka na tabia yao.Wkt hoja ya Serikali tatu ktk mjadala wa Zanzibar/Tanganyika ilipokolea, CCM walianza kupita Makanisani, wkt huu walitumia viongozi wao waandamizi kutisha na kugawa Wakristo, William Lukuvi Wazir ktk Serikali ya Mh J.K (Mwislamu) alisimama Kanisani na kuwabagua vibaya Waislamu kwa nia ovu sana na Rais Jakaya (Mwislamu) hakuchukua hatua yoyote kwa Lukuvi hata kama maneno ya Lukuvi yaliligawa Taifa. Lengo likiwa kukwamisha malengo ya Zanzibar huru,ikumbukwe wkt huo pia Rais wa Zanzibar Mwislamu mjumbe wa CC CCM na anayeingia kwenye Baraza la Mawaziri Tanganyika alikaa kimya kwa kauli ya chafu ya William Lukuvi.
Mwaka 2015,CCM wakaendelea tena, wkt huu Edward Lowassa Mkristo alikuwa anagombea Urais dhidi ya John Magufuli Mkristo,tukafikiri propaganda zitakuwa ngumu , CCM wakaja na formula mpya ya Mkatoloki vs Mlutheri na siasa za ukanda zikaanza kuchomoza kwa mkakati ambao uliendelea mpaka Rais Magufuli anafariki.
Hatuwezi kuandika yote hapa ktk ukurasa wa X (Tweeter) Lakini ukweli ni kwamba CCM wametumia sana mbinu ya wagawe/watawale kwa muda mrefu sana na bahati mbaya njaa imetumika kama silaha muhimu kwa kufanikisha malengo haya.Hata sasa jitihada nyingi zitafanyika kubeza maoni ya TEC kwa njia hizo hizo.Taasisi yoyote iwe Kanisa/Msikiti muda wake wa kutetea raslimali za Nchi,haki na kweli ni wakati wowote na huu ndio wajibu wao .Je , wakati mzuri ni wakati gani ? Wakati mzuri ni wakati wowote na busara ni ukweli kuchukua hatua kila wakati.
Maneno ya Mh JKM ni maneno mazuri lakini anapaswa kuionya CCM wkt ana sauti na CCM wanapaswa kujishahisha.Kiongozi wa dini anapaswa kuwa wa kwanza kuona, kusema,kukemea,kuonya na kushauri mienendo yote inayotishia maslahi na ustawi wa Nchi.Huku sio kuchanganya dini na siasa bali ni kuchanganya akili na sias. Dini isichanganywe na Siasa lakini ni lazima siasa ichanganywe na hekima za Mwenyezi Mungu.
Kuanzia Mwaka jana Dec hadi mwezi wa nne mwaka huu nilikuwa busy sana ku design jukwaa ambalo itakuwa rahisi wanaopenda kujifunza kupata Premium content kwa urahisi. Mpaka sasa imefika stage ambayo lengo linaelekewa ipo kupitia https://t.co/EEmWI1LCMI. Maoni yako yanakaribishwa.