A great pleasure to meet with the President of #Tanzania H.E. @SuluhuSamia and thank her for championing positive change for children.
We discussed ways to further strengthen our collaboration, including in nutrition, health and education to reach the most vulnerable children.
Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (@UNICEFTanzania ), limeipongeza Tanzania kwa kupiga hatua kubwa katika masuala ya uwazi kwenye mchakato wa uandaaji na utekelezaji wa Bajeti Kuu ya Serikali kutokana na matokeo ya utafiti wa uliofanywa na Shirika hilo.
Pongezi hizo zimetolewa jijini Dodoma na Mwakilishi Mkazi wa UNICEF nchini Tanzania, Bi. Elke Wisch, alipokutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb) ambapo walijadiliana mambo mbalimbali ya ushirikiano kati ya Serikali na UNICEF.
Kutokana na utafiti walioufanywa na UNICEF, utakaozinduliwa hivi karibuni unaonesha kuwa katika kipindi cha miezi 16 iliyopita ambacho utafiti huo umefanyika, Tanzania imepanda viwango vya uwazi katika masuala ya bajeti kutoka asilimia 21 hadi 41 na kuzizidi nchi zote za Bara la Afrika.
Alisema kuwa katika kipindi cha Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Tanzania imepiga hatua kubwa katika suala la uwazi na uwajibikaji kutokana na bajeti yake kuwa na uhalisia na kuweka mazingira mazuri kwa wafanyabiashara, wawekezaji, wadau wa maendeleo na taasisi za fedha.
Bi. Wisch alisema kuwa hatua hiyo inafaa kupongezwa na wadau wote wa maendeleo na kwamba matarajio ya Shirika hilo ni kuona kiwango hicho kinaongezeka zaidi ili angalau kifikie zaidi ya asilimia 50, jambo ambalo alisema kutokana na uongozi thabiti wa Serikali ya Awamu ya Sita, viwango hivyo vitafikiwa hivi karibuni.
Bi. Wisch ameahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania katika masuala mbalimbali ya maendeleo hususani masuala ya elimu, lishe, Watoto na vijana.
Aidha, Bi. Wisch alieleza kuwa Tanzania ina programu za chakula mashuleni jambo ambalo linawasaidia wanafunzi kuwa na mazingira mazuri ya kupata elimu, lakini pia msisitizo wa lishe bora kwa Watoto ni jambo muhimu ili kupambana na udumavu wa akili na kuwajengea watoto ubongo unaomuwezesha mtoto kuwa na akili nzuri.
Alisema pia kuwa Tanzania imeendelea kufanya vizuri katika masuala mbalimbali ukilinganisha na nchi nyingine za Afrika jambo ambalo linachochea ushirikiano zaidi na mashirika ya maendeleo katika kusaidia kuchochea zaidi maendeleo ya wananchi wake katika sekta mbalimbali.
Kwa upande wake Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 alisema kuwa katika Bajeti Kuu ya mwaka wa fedha 2023/24 UNICEF, iliahidi kutoa msaada wa zaidi ya dola milioni 20.3 kwa ajili utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ya uchumi wa kijamii kwenye eneo la afya, lishe, elimu, kuwalinda Watoto, sera ya jamii, jinsia na mipango.
Dkt. Nchemba ameipongeza UNICEF kwa kuendelea kushirikiana na Tanzania katika nyanja mbalimbali zinazokuza ustawi wa jamii kupitia michango yao katika Bajeti Kuu ya Serikali zinazoelekezwa kuhudumia jamii ikiwemo afya na elimu.
Aidha Dkt. Nchemba amelishukuru Shirika hilo kwa msaada wake katika masuala ya uwazi, uwajibikaji na kusaidia ushiriki wa umma katika hatua mbalimbali za maandalizi ya bajeti kupitia utafiti wao wa uwazi wa masuala ya bajeti.
Alisema kuwa Tafiti hizo zimesaidia kuboresha bajeti jambo lililosaidia kujenga imani ya wananchi kwa Serikali yao na matumizi bora ya rasilimali.
Amesema kuwa anatumaini UNICEF itaendelea kuisaidia Serikali katika masuala ya kibajeti na Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano ulioanzia mwaka 2021/22 hadi 2025/26.
@OlengurumwaO Ajali hii ilitokea asubuhi. Hapa hawakufuata alama za barabarani. Mwendo kasi sijajua huwa unahusishwaje na ajali nyingi hapa nchini. Magari haya yametengenezwa kwenda mpaka
speed 180. Ajali nyingi hutokea kwa kuovertake kwenye kona/vilima
Waziri @Dr_DGwajima amesema ili kuhakikisha tunakuwa na Taifa lililo bora ni lazima kuanza kuwekeza kwa watoto na kwamba Serikali imeshaanza kutekeleza afua ya malezi na Makuzi ya awali katika vituo kadhaa hivyo jitihada za kuongeza zinafanyika.
“We must work together for Artificial Intelligence that bridges social, digital, and economic divides – not one that pushes us further apart.”
– @antonioguterres says he is convening an advisory board to explore options for global AI governance. https://t.co/LU5VnXIlnq
Kwa utafiti uliofanywa na Wizara pamoja na @UNICEFTanzania mwaka 2022 ulibainisha 67% ya watoto wenye umri kati ya miaka 12 hadi 17 wanatumia simu; na kwamba asilimia 4 kati yao wamefanyiwa ukatili.
2/4
Jana katika maadhimisho ya #SikuYaMtotoWaAfrika, nimezindua mwongozo wa kupinga ukatili wa watoto kwenye michezo, vitini vya mafunzo ya malezi ya watoto na Baraza la watoto Taifa.
1/4
Waziri wa @maendeleoyajami Mhe. @Dr_DGwajima amesema utafiti uliofanywa na Wizara pamoja na @UNICEFTanzania mwaka 2022 ulibainisha 67% ya watoto wenye umri kati ya miaka 12 hadi 17 wanatumia simu, asilimia 4 kati yao wamefanyiwa ukatili.
📍 Dodoma
"Jamii ina wajibu wa kuhakikisha mitandao ya kijamii inatumika kwa manufaa mazuri, Na naisihi jamii kuacha kusambaza taarifa zao binafsi kwenye Mitandao" Mwakilishi wa @UNICEFTanzania John George katika Maadhimishoya siku ya Mtoto wa Afrika Juni 16, 2023.