Inasikitisha sana kama kweli deal hii imeondoka Tanzania. Shame, shame, shame! Tumepoteza fursa ya kipekee na smart deal ambayo ingeweza kuleta manufaa makubwa kwa Nchi. Nimeumia sana.
Air Tanzania Launches Direct Moscow-Zanzibar Flights
https://t.co/97HXB6FNe2
Tanzanian Airlines have begun a regular Zanzibar-Moscow service designed to promote tourism and trade. The country is renowned for its spectacular beaches, safari’s and wildlife and is another exotic Russian tourism alternative to European destinations.
@RussiasPivot At Fox Africa Safaris we arrange tailormade safaris to the most iconic Tanzania Parks. Serengeti, Ngorongoro Crater, Tarangire, Mount Kilimanjaro, Nyerere National Park, Ruaha National Park, Mahale Mountaind for chimpanzee trekking, Zanzibar beaches https://t.co/T8Vcg0bUwe
@usembassytz Je, ni ile MOU iliyokataliwa na nchi zingine za Afrika? Je, MOU inajumuisha kambi ya Ebola au kushiriki data zetu za matibabu? Kwa nini ni 'America First'?
Tuwekee hiyo MOU hapa tusome yaliyomo.
Je, ni ile MOU iliyokataliwa na nchi zingine za Afrika? Je, MOU inajumuisha ujenzi wa kambi ya Ebola au kushiriki data zetu za matibabu? Kwa nini ni 'America First'?
🇺🇸🤝🇹🇿 Decades of partnership. A future built together.
The new U.S.–Tanzania Health MOU means: ✅ Stronger hospitals ✅ Better data and digital infrastructure ✅ Faster outbreak response ✅ Tanzanian-led, sustainable health systems
This is what America First looks like in action — results for both nations. https://t.co/tfvS677Itd
#USTanzania #AmericaFirst #HealthMOU #GlobalHealth
@usembassytz Je, ni ile MOU iliyokataliwa na nchi zingine za Afrika? Je, MOU inajumuisha kambi ya Ebola au kushiriki data zetu za matibabu? Kwa nini ni 'America First'?
@usembassytz Je, ni ule ushirikiano uliokataliwa na nchi zingine za Afrika? Je, MOU inajumuisha ujenzi wa kambi ya Ebola au kushiriki data zetu za matibabu? Kwa nini ni "Marekani Kwanza"?
@usembassytz Je, ni ile ile iliyokataliwa na nchi zingine za Afrika? Je, MOU inajumuisha kambi ya Ebola au kushiriki data zetu za matibabu ili kutengeneza virusi vingine? Kwa nini ni 'America First'?
Wakati CHADEMA tumezuiwa kufanya Mikutano ya hadhara, kesho Mwenyekiti wa UVCCM atakuwa Mikutano huko Chato.
Ushaidi huu hapa someni wenyewe barua ya Mkurungenzi wa Wilaya ya Chato.
Is it the same turned out by other African countries? Does the MOU include Ebola camp or sharing our medical data to create another virus. Why is it America First?
The United States and Tanzania signed a five-year bilateral global health Memorandum of Understanding (MOU) through the Trump Administration’s America First Global Health Strategy to save lives, advance shared global health goals, and bolster Tanzanian self-sufficiency to address infectious diseases and emerging health threats. Read more: https://t.co/FwhkR15qKh
Kaka @zittokabwe habari yako!
Umekuwa mkali baada ya Mkuu wa Majeshi Uganda, Dikteta Muhoozi Kainerugaba kutoa agizo la kufunga vituo vya NTV na gazeti la Daily Monitor, ukisema ni shambulio dhidi ya uwekezaji wa Kitanzania.
Nyumbani kwetu hapa, kituo cha JAMBO TV (kinachomilikiwa na rafiki yako, John Marwa) kimefungiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa siku 90 kwa kukiuka kanuni zao.
JAMII FORUMS, ilifungiwa kwa siku 90 na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Septemba 2025 kwa tuhuma za kuchapisha maudhui ya kupotosha na kudhalilisha serikali. Hukupaza sauti kabisa.
Walistahili kupiganiwa ipasavyo kwa wewe kupaza sauti. Unatetea maslahi ya matajiri (tycoons) wa kisiasa waliowekeza nje ya nchi wakati huo ukipuuza ukandamizaji wa vyombo vya habari ndani.
Unakaa kimya wakati JAMBO TV inafungiwa hatua inayoumiza waandishi wa habari wa Kitanzania moja kwa moja, unasimama kutetea maslahi ya kampuni ya Mauritius inayofanya biashara Uganda.
Kwamba kufungwa kwa vyombo hivyo Uganda ni pigo kwa uwekezaji wa Watanzania? Muundo wa kampumi ya TAARIFA LIMITED unapingana na hoja yako ya msingi. Huo siyo uwekezaji wa Kitanzania.
TAARIFA LIMITED ni kampuni ya uwekezaji (investment holding company), ilichaguliwa kama muundo wa kisheria kwa ununuzi wa hisa kubwa katika kampuni ya Nation Media Group (NMG)
Ilitumika katika ununuzi wa hisa (54%) katika kampuni ya Nation Media Group (NMG), kupitia kununua NPRT Holdings Africa LTD kutoka Aga Khan Fund for Economic Development (AKFED).
TAARIFA LIMITED, ambayo ilichukua 54% ya hisa zilizokuwa za Aga Khan Fund for Economic Development (AKFED) ndani ya Nation Media Group (NMG) imesajiliwa MAURITIUS siyo Tanzania
Kisheria na kiuchumi, uwekezaji uliosajiliwa katika maeneo yenye nafuu ya kodi (tax havens) kama MAURITIUS haunufaishi uchumi wa Tanzania moja kwa moja. Siyo ‘Tanzanian-owned businesses’
Hakuna namna fedha zinazozalishwa na vyombo hivyo nchini Uganda zitakavyoingia kwenye mfumo wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuongeza akiba yetu ya fedha za kigeni (foreign reserves). HAIPO
Zinaishia akaunti za mabenki ya kigeni Mauritius au kwingineko. Mauritius inajulikana kwa kuwa na mikataba ya kuzuia utozaji kodi mara mbili (Double Taxation Avoidance Agreements - DTAAs)
Inapotokea kampuni imeuza hisa zake au inapata faida, kodi ya faida inalipwa MAURITIUS (ambako viwango ni vidogo au ni sifuri) badala ya Tanzania au nchi ambako biashara halisi inafanyika.
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) haiwezi kudai kodi ya mapato (income tax) ya moja kwa moja kwenye miamala inayofanyika chini ya mwavuli wa kampuni iliyosajiliwa katika nchi ya Mauritius.
Kampuni ikisajiliwa Mauritius, iko chini ya sheria za makampuni Mauritius. Tanzania haina mamlaka ya kisheria (jurisdiction) kuhoji muundo wa utawala, akaunti za benki, uwazi wake wa kifedha.
Kodi, faida, na miamala ya kimkakati ya kampuni hiyo haiingii katika mfumo wa mapato ya ndani wa Tanzania. Huo siyo ‘uwekezaji wa Kitanzania’. Labda utafute jina lingine la kuita huo uwekezaji.
Faida inayopatikana kupitia mianya hii ya tax havens hairudi kama kodi ya kujenga shule, hospitali au barabara, ni pesa za mifukoni za wafanyabiashara wakubwa wa kisiasa na makada wa CCM.
Fedha hizi ndizo zinazotumika kufadhili harakati za kisiasa za ndani, ikiwemo kampeni za uchaguzi na matukio ya ukandamizaji wa kisiasa kama yale yaliyoshuhudiwa nchini mnamo Oktoba 29.
Badala ya kuhoji ni kwa namna gani uwekezaji huo wa Taarifa Limited katika vyombo vya habari vya Uganda unamsaidia mwananchi wa kawaida wa Tanzania, unakuwa mtetezi wa biashara za MaCCM.
Unapigania maslahi ya matajiri ambao wanatumia faida zao kudhoofisha demokrasia. Unasikitikia uwekezaji uliosajiliwa Mauritius usiokuwa na tija ya kodi au ajira ya moja kwa moja kwa Mtanzania.
MMM, Martin Maranja Masese, Masese