"Kuku mmoja anayetaga mayai ya dhahabu ni bandari ya Dar Es Salaam. Unachotakiwa kufanya ni kuhakikisha hakuna usumbufu kwenye mizigo, kwanza unawatengenezea watu barabara za uhakika kutoka Bandarini. Magufuli alianza kujenga bandari ya Nchi kavu Kwala kwamba mizigo yote itoke bandarini iende Kwala na pale Kwala Magufuli aliweka eneo la Zambia, Congo, Burundi na nchi zote zinazotutegemea."
"Ameondoka Magufuli, Bandari ile imerudi Mjini, Dar Es Salam Mji wote imekuwa sehemu ya kuweka Makontena, wanafanya usumbufu mkubwa sana kwa Wafanyabiashara, Kontena za mtu mmoja zinagawanywa Posta, lingine Mbagala, lingine Vingunguti, unapata usumbufu mkubwa sana wa kutafuta kontena. Bandari hii tusipochukua hatua inaenda kufa." John Heche, Makamu Mwenyekiti wa Chadema akizungumza na Vijana wa Chadema leo Jumatano.