Hii kauli ya “Linda mgongo wako” kutoka kwa Godfrey Tumaini ilitakiwa kuwa adopted na mamlaka inayohusika na malezi ya vijana na kuifanya kuwa kampeni kubwa na endelevu kwa ustawi wa maadili ya watoto wetu.
Mdau anadai “Baada ya kushinda Tsh. 27,760,815 kwenye kubashiriri Mtandaoni, kampuni husika ilisimamisha mkeka wangu bila kunipa taarifa, pia waliingia kwenye akaunti yangu na kuufuta (cancel) mkeka, hiyo ni kinyume na vigezo na masharti yao wenyewe na ya Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania.”
Mdau ametoa wito kwa Serikali kuiongezea nguvu Gaming Board au kuongeza uwajibikaji kwa Wasimamizi wa Kitengo hicho ili kuwasaidia Wananchi wenye changamoto kama yake.
Soma https://t.co/4XnvJo89EW
#JamiiForums #JFMdau2026
Mkutano wangu na waandishi wa habari niliokuwa nifanye katika Hotel ya Golden Tulip nimeuahirisha.
Nimesikiliza hotuba za Makamu Mwenyekiti na Katibu Mkuu. Wameeleza vizuri kuhusu uvumi na upotoshaji uliokuwa ukifanyika juu yangu na misimamo juu ya chama chetu.
Nimedumu katika mapambano haya kwa zaidi ya miaka 22. Nimeenda lock-up zaidi ya mara 50. Nimezunguka nchi hii usiku na zaidi ya mara tatu. Nimewahi kuwa magerezani mara kadhaa, nimekoswa kuuawa zaidi ya mara tatu, na nimewahi kukimbia nchi.
Katika yote haya, nimekuwa nikitoa sadaka kubwa kwa ajili ya mapambano haya, ikiwemo ku-sacrifice familia yangu mara zote.
Kazi hii kwangu si ajira, si cheo, wala si njia ya kujitafutia maslahi. Ni huduma. Ni wito. Ni kama injili ninayoamini na kuitumikia.
Kwa hiyo, siwezi kuruhusu uvumi, upotoshaji au tafsiri za watu kuniondoa kwenye misingi ambayo nimeisimamia kwa zaidi ya miongo miwili.
Nitakuwa kwenye mapambano haya kwa imani, ujasiri na dhamira njema siku zote.
Nimeona matusi na sintofahamu nyingi mtandaoni baada ya kuchapisha ujumbe wa kutoa pole kwa Mama Samia, hasa niliponukuu salamu za pole za Mwenyekiti Lissu kutoka gerezani.
Kwa sisi jamii tunaodai kupigania uhuru wa maoni na demokrasia, hili linapaswa kutufikirisha. Kutofautiana kwa hoja hakuhitaji matusi, dhihaka wala chuki.
Lissu amekaa gerezani takribani mwaka mmoja na miezi sita, akikabiliwa na kesi ambayo sisi tunaamini ni ya kisiasa na isiyo na haki. Anafahamu yaliyompata na serikali iliyomweka mahabusu. Lakini alipofahamishwa kuhusu msiba wa mume wa Mama Samia, akiwa mbele ya mahakama, alitoa salamu zake za pole kwa wafiwa mara mbili.
Huu si unyonge. Hii ni hekima, utu na ukomavu wa kiwango cha juu.
Na si mara ya kwanza. Aliwahi pia kumtetea Sabaya katika kesi yake Moshi. Wengi tulishangaa, nami nilishangaa. Lakini nilipomuuliza baadaye, nilielewa kwamba kwake haki haichagui upande.
Hilo ndilo fundisho kubwa tunalopaswa kulibeba. Tunaweza kupinga serikali, kudai haki na kupigania demokrasia bila kujenga harakati zetu juu ya chuki na kisasi.
Lakini kama tunasema tunampenda Lissu, basi pale anaposema ana pumzi ya kuvumilia mateso na kukaa gerezani, sisi tunapaswa kuchukua kauli hiyo kama mwito wa ujasiri, si ruhusa ya kukaa kimya.
Kama tunaamini kesi hii si ya haki, basi viongozi tunanapaswa kuwaongoza wananchi katika hatua za amani, kisheria na kidemokrasia za kudai haki, pengine kwa njia ya maandamano. Sio kwenye keyboard tu na microphone.
Demokrasia inahitaji wananchi wanaothubutu kusimama kwa kile wanachoamini. Na kama siku moja tutapata nafasi ya kuongoza nchi hii, tusije tukarudia makosa tunayoyapinga leo. Lazima tutawala kwa haki, utu na dhamira njema.
Mimi nitasimama kwenye upendo, utu na haki siku zote ktk kazi hii. Anyway , hekima ya Lissu kutoa pole kwa Mama Samia was a top-class thinking. Inaonyesha kwamba hata unapoteseka, unaweza kuchagua utu, hata unapopinga, unaweza kukataa kisasi.
Wakati mwingine Mungu hataki umshinde adui yako kwa chuki, bali kwa upendo, hekima na maisha yenye ushuhuda kwamba uovu wake haukukushinda.
Mimi niko tayari kusimama kwa amani na kwa ujasiri. Katika hatua ya kupigania uhuru wa Lissu kuwa nje ya kuta za gereza na sio kusema ana pumzi ya kukaa jela hata maisha. Tuna watu wengi sana Chama hiki , pumzi yetu itoke mtandaoni , fikeni tu hata mahakamani kwa sasa na huku viongozi wakuu watusaidie kutafakari jambo muhimu la haki , sheria na amani.
“You don’t have to hate those who hurt you. Sometimes the greatest revenge is to rise above them with peace, dignity, and success.”
Thank you !!
If you have a family history of CANCER, get pigweed and dry the entire plant.
Burn the plant into ashes. Mix a teaspoon of the ash with half glass of water and drink this once every week. Cancer will be far from you.
This preparation also cures colon cancer. Nature heals.
Madaktari Hospital ya Rufaa Mount Meru Arusha wanamoyo ubinadamu mbali na mishahara midogo wanayolipwa mazingira magumu ya kazi wanajitolea sana. Madaktari wanachanga kumnunulia mgonjwa dawa Mwenyezi Mungu uwalipe mema kwa sadaka yao uwajaalie afya njema uwalinde na mabaya Amin.