Official Twitter Account of Hamad M. Hamad, Secretary General of The Civic United Front-CUF & Former Minister of Infrastructure & Communication: Views are mine.
Tumekutana na kufanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mussa Azzan Zungu(Mb), tukiongozwa na Mwenyekiti wetu wa Taifa Mhe. Mirambo Yusuf Camil, tarehe 20 Aprili, 2026, katika Ofisi ya Bunge, Jijini Dodoma.
Tutamkumbuka Mhe. Suleiman Bungara (Bwege) kama mtu mwenye misimamo, asieyumba na anaesimamia kile anachokiamini. Bwege aliamini katika kusimamia maslahi ya watu bila ya kujali afya yake na siku zote hakuchoka kupigania haki. Allah ailaze roho yake mahala pema, Peponi; Amen.
#TANZANIA: MWENYEKITI WA CUF TAIFA AFIKA MSIBANI KWA BWEGE KILWA
Mwenyekiti wa CUF Taifa, Milambo Kamili Yusuph hii leo Machi 31, 2026 amefika msibani kwa aliyekuwa Mbunge wa Kilwa Kusini mkoani Lindi, Selemani Bungara maarufu Bwege tayari kwa kumpumzisha marehemu Bwege kwenye nyumba yake ya milele.
Zaidi: https://t.co/UalpIjZCbV
Chama cha Wananchi (CUF) kimemchagua Mirambo Yusuf kuwa Mwenyekiti mpya wa Chama hicho baada ya kupata kura 257 alizopigiwa na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa dharura wa chama hicho, uliofanyika katika Ukumbi wa Lekham, Buguruni, jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo Jumapili Februari 22, 2026.
Mirambo, ambaye ni Mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Kigoma Mjini, amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa nne wa chama hicho akichukua mikoba ya Profesa Ibrahim Lipumba katika nafasi hiyo.
Mgombea wa pili aliyefuatia kwa wingi wa kura, Othman Omar Dunga, amepata kura 177 huku mgombea wa tatu, Nkunyunyika Siwale akijikusanyia kura 6 kati ya jumla ya kura 448 zilizopigwa ambapo kura sita zikiharibika.
Kwa upande wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti Tanzania Bara, Miraji Mtibwiliko amepata kura 264 na kuwashinda Mohammed Ngulangwa aliyepata kura 88 pamoja na Mussa Mbarouk aliyepata kura 82.
Nafasi ya Makamu Mwenyekiti Zanzibar imechukuliwa na Haroub Mohamed Shamsi aliyepata kura 256, akimshinda Mbarouk Seif Salim aliyepata kura 171, huku Amina Rashid Salim akijitoa kabla ya upigaji kura.
#KitengeUpdates
Tanzania has passed through perilous times before, during and after election as myriad dead bodies littered the streets. What happened is not only a shame and tragedy for our nation but a call for the government to be attentive to the people's opinions and respect their wishes.
Nikipokea fomu ya uteuzi ya kugombea nafasi ya Urais wa Zanzibar kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC). Zoezi hilo limefanyika leo tarehe 30/8/2025 katika Ofisi za Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) zilizopo Maisara, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja.
Nawashkuru sana Wajumbe wa Mkutano Mkuu Taifa kwa kuniamini na kunichagua kwa kura nyingi (406) kua Mgombea wa Urais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Chama chetu cha Wananchi - CUF. Nawaahidini ndani ya muda huu mfupi uliobaki nitapambana kuhakikisha tunashinda.
Nikiwa rais wa nchi hii yajayo yatakua ni neema kwa wote. Tuna mikakati mizuri, ya kistaarabu na ya amani kabisa ya kuhakikisha tunawaunganisha Wazanzibari na Watanzania wote.
Tembelea https://t.co/GBq1mnPFO0 kusoma gazeti lako au wasiliana nasi 📞+255 745 -700 710 au 0677- 020 701 kwa maelezo zaidi.WhatsApp 0715086344
Julai 01, 2025
Namshukuru Allah kwa kuniwezesha kukamilisha hatua moja muhimu ya kuchukua na kurejesha fomu ya Chama ya Kugombea Urais wa Zanzibar. Ni matumaini yangu kwamba kama nilivyoweza kukamilisha hatua hii ya awali, nitaweza pia kukamilisha hatua zote muhimu zilizobaki.
Leo tarehe 30/06/2025 nitachukua fomu ya Kugombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama changu cha Wananchi - CUF. Zoezi hilo litafanyika katika Ofisi za Wilaya ya Magharibi B, Kilimahewa, Unguja, Zanazbiar saa 5:00 za asubuhi. Namumboa Allah aniongoze katika kila hatua.
Nimezipokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Ikulu na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Charles Hillary. Natoa pole kwa familia, ndugu na jamaa kwa msiba huu nzito na namuomba Allah amlaze mahala pema peponi. Amen.
Nimezipokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha aliewahi kua Mbunge wa CUF, Jimbo la Malindi, Mhe. Mohammed Sanya. Natoa pole kwa familiya yake na namuomba Allah amsamehe makosa yake na amjaalie pepo yawe makaazi yake.
Hakika sisi sote ni wa Mungu na kwake tutarejea.
Eid El Fitri ni siku ya sherehe na shukrani kwa baraka zilizopatikana ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani. Nachukua fursa hii kuwatakia Waislamu wote #EidMubarak na muomba Allah atujaalie furaha na amani katika kusherehekea siku hii muhimu kwetu.
Nawatakia Waislam wote duniani Ramadhan Qareem. Allah atutakabalie Dua na Ibada zetu, atupe nguvu za kutekeleza faradhi na sunna za mwezi huu na atupe amani, mapenzi na fadhila za Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhan; Amiin.
Nikiondoka mara baada ya kumalizika kwa Mazishi ya Shekh Mohamed Iddy yaliyofanyika Mkata, Handeni, Tanga jioni ya leo tarehe 31/01/2025. Allah amsamehe makosa yake na amjaalie yeye pamoja na sisi Pepo yawe makaazi yetu. Amen!
Hakuna Binadamu Mkamilifu. Inawezekana kabisa tulikoseana ama kwa Makusudi au kwa kutokujua. Nawaombeni radhi wale wote niliowakosea na ukweli huu kwangu anaujua Mungu, mimi nimewasameheni nyote. Nakutakieni safari njema, murudi nyumbani salama na kwaherini ya kuonana.
Leo tarehe 18 Desemba, wajumbe kutoka Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) wamehudhuria Mkutano Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF). TCD imepokea cheti cha kutambua mchango wake katika kukuza demokrasia nchini.
Tunatoa shukrani za dhati kwa uongozi wa CUF kwa heshima hii.