"Tutashiriki kwa namna itakayolenga kulinda na kukuza utu wetu. Tutashiriki
kwa kuzungumza lugha itakayoeleweka na dola. Tutashiriki kimapambano na kigangwe. Tutashiriki kushinda na sio
kuchezewa na kufanyiwa fedheha." - Dorothy Semu na Othman Masoud Othman Shariff
ALIYEKUWA Naibu Meya wa Ilala Ojambi Didas Masaburi, amechukua fomu leo kuwani Jimbo Jipya la Kivule, Jijini Dar es Salaam.
Ojambi kabla alikuwa Diwani wa Kata ya Chanika, Wilayani Ilala.
#KitengeUpdates
Kuna siku tumeenda kuzurura Serengeti sasa tukafika kwenye pool ya Hippo’s tukashuka bana ile kushangaa shangaa dreva akapiga kelele ya kuona Simba, watu watatu wote tukaingia kwenye mlango mmoja ndani ya sekunde kadhaa!
Zaidi ya 70% ya watu wanaowania UBUNGE na nafasi nyingine za kuchaguliwa ndani ya CCM, hawafanyi hivyo kwa sababu ya utashi wa kuitumikia Nchi Ila wengi wanajitokeza kwa sababu mazingira ya uchaguzi yamezungukwa na dhuluma,uharamia na wizi wa kura na hivyo hakuna hofu ya wao kushindwa uchaguzi kwa sababu ya tabia hizi mbaya ambazo zimeondoa ushindani wa haki ktk Uchaguzi.
Ni hatari kuwa na aina hii ya jamii haswa vijana.Hatari zaidi unaendelea kuwa na Wabunge wenye aina hii ya fikra na kwamba ushindi wao umeamuliwa na dhambi mbaya ya uhalifu.Inatisha sana, kazi ya wito mwema ya kujenga Nchi bora zaidi kesho inapokuwa biashara ya kitapeli na kihuni. Kila mtu atajuta kabla hatujaamka wote huku tukiwa tumechelewa sana. Mshahara wa matendo haya utaligharimu sana Taifa letu. Naogopa hata kuwaza, kwamba una jamii inayopata ujasiri ktk ukatili wa matendo mabaya. So Sad.
Ingekuwa Bongo Kuna Mambo za Mgombea Huru (Asiye na Chama ) kesho Asubuhi Ningechukua Pesa zangu za Mbaazi Nikavute Iyo Fomu ya Ubunge pale Arumeru Mashariki !! 🤣
Daniel Chongolo amechukua form kugombea Ubunge jimbo la Makambako, kabla alikuwa Mkuu wa mkoa wa Songwe.
Kwasasa Jimbo la Makambako Mbunge wake ni Deo Sanga.
Hapa napo pamoto sana