Top Tweets for #Kifafa
Mapema leo, @AmrefTanzania kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Ofisi ya Rais TAMISEMI na wadau wengine, wamekutana katika kikao kazi cha kutambulisha Mradi wa Kuimarisha Huduma za #Kifafa (Enhancing Epilepsy Care Africa (EECA) in Tanzania).
Akizungumza katika kikao hicho, Katibu Tawala wa Mkoa wa #Dodoma, Kaspar Mmuya, ameipongeza @AmrefTanzania kwa kuendelea kushirikiana na serikali katika kuimarisha utoaji wa huduma za afya kwa jamii hususani kwa magonjwa yasiyoambukizwa kama kifafa.
Mradi huu unalenga kupunguza unyanyapaa kwa Watu Wenye Kifafa na utatekelezwa katika Wilaya za #Bahi na #Chamwino mkoani #Dodoma.
cc. @wizara_afyatz @ortamisemitz

Tutakuwa Live Hapa (X-Space) kuanzia saa Mbili Usiku huu kuendelea na Mjadala wetu kuhusu Ugonjwa wa #Kifafa
Jiandae na umualike rafiki yako.
Sababu za Mtu kupata Ugonjwa #Kifafa ni pamoja na kupata Changamoto kwenye Ubongo au jeraha wakati wa kuzaliwa, Uvimbe au hali za 'Kijenetiki' zinazohusiana na Ubongo
Kupata Jeraha kubwa Kichwani, Kiharusi (Stroke) kinachopunguza kiasi cha Oksijeni kwenye Ubongo, na Maambukizi ya Ubongo kama vile #Meningitis
Soma https://t.co/naIpsUw6Cg
#WorldEpilepsyDay #Epilepsy #JamiiForums #PublicHealth #EpilepsyAwareness

Tukiwa katika wiki ya Kuadhimisha uelewa kuhusu #kifafa tutakuwa na mjadala kupitia mtandao wetu wa x kuanzia saa 12 Jioni
Ungana nasi tutakuwa na Madaktari wetu bingwa wa mifumo ya fahamu katika mdahala huo.
#myepilepsyjourney

Siku ya #Kifafa Duniani huadhimishwa kila Februari 12 ikilenga kujenga uelewa na kupunguza unyanyapaa unaohusiana na Kifafa, kusambaza Habari sahihi kuhusu Ugonjwa huu, na kukuza uelewa wa Umma jinsi ya kusaidia Watu walio na Kifafa na Familia zao
Siku hii huwaleta pamoja Wataalamu wa #Afya, Mashirika, Watu wenye Kifafa, na Jamii ili kujenga Jamii yenye uelewa na msaada kwa Watu wenye Kifafa.
Soma https://t.co/naIpsUw6Cg
#WorldEpilepsyDay #Epilepsy #JamiiForums #PublicHealth #EpilepsyAwareness

DKT. NORMAN JONAS (KCMC): Kama Mgonjwa aliacha kutumia Dawa akiamini amepona #Kifafa bila kupima wala kumhusisha Daktari, anashauriwa kurejea Kituo cha Afya na kumuona Daktari kwa ajili ya kupata maelekezo zaidi, hilo ni muhimu sana kulifanya
#JamiiForums #Afya #PublicHealth #Epilepsy #EpilepsyAwareness
DKT. KIGOCHA OKENG’O (Daktari Bingwa wa Mishipa ya Fahamu na Ubongo Hospitali ya Taifa Muhimbili): #Kifafa kinaweza kumpata Mtu mwenye umri wowote, iwe ni Wazee, Watu wazima na hata Watoto
Utafiti ulifanyika Nchini #Tanzania na kubaini kuwa kila Mtu yupo hatarini kupata Kifafa kwa kiwango cha Asilimia 2
#JamiiForums #Afya #PublicHealth #Epilepsy #EpilepsyAwareness
DKT. DAVID KOMBO (Daktari Bingwa wa Watoto Wenye Shida za Ubongo na Mishipa ya Fahamu MNH): Takwimu za Kisayansi zinaeleza kati ya Watu 100 wenye #Kifafa, Watu 70 wanaweza kupona kabisa
Hao 30 waliosalia wanaweza kuendelea kuwa na changamoto huku wakitumia Dawa
Pia, kuna aina za Kifafa ambazo haziwezi kutibika kwa Dawa bali kwa upasuaji
#JamiiForums #Afya #PublicHealth #Epilepsy #EpilepsyAwareness
DKT. NORMAN JONAS (KCMC): #Kifafa hakiambukizwi kutoka kwa Mtu mmoja kwenda kwa mwingine, hata kama unamuuguza Mgonjwa kwa muda mrefu haimaanishi nawe utapata Kifafa
#JamiiForums #Afya #PublicHealth #Epilepsy #EpilepsyAwareness
FIDES UISO (Mzazi ambaye Mtoto wake ana Kifafa na Mkurugenzi wa Tanzania Epilepsy Organisation): Nashauri wanaotumia Dawa za #Kifafa kuzingatia muda sahihi wa kumeza Dawa kwa kuwa kuzipishanisha sana au kusitisha kunaweza kumuathiri Mgonjwa
#JamiiForums #Afya #PublicHealth #Epilepsy #EpilepsyAwareness
DKT. KIGOCHA OKENG’O (Daktari Bingwa wa Mishipa ya Fahamu na Ubongo Hospitali ya Taifa Muhimbili): Tofauti ya Kifafa na #Degedege ni kuwa, Degedege ni dalili za kuelekea kupata Kifafa
Ukipata Degedege zaidi mara mbili hiyo ni tafsiri ya kwanza ya kuugua #Kifafa
Kuna wengine wanaweza kupata Degedege kutokana na kushuka kwa Sukari na hukaa sawa Sukari ikipandishwa. Huyu hatuwezi kusema kwamba ana Kifafa moja kwa moja
#JamiiForums #Afya #PublicHealth #Epilepsy #EpilepsyAwareness
DKT. KIGOCHA OKENG’O (Daktari Bingwa wa Mishipa ya Fahamu na Ubongo Hospitali ya Taifa Muhimbili): Kuna #Kifafa cha Ubongo mzima, cha upande mmoja na kingine ni cha kurithi japo ni kwa asilimia chache
Asilimia kubwa ya Kifafa inaweza kusababishwa na Ajali kwenye Ubongo au kwa Mtoto wakati wa kuzaliwa au Mtoto akiwa mdogo kupata Magonjwa kama Degedege
Upande wa Watu wazima inaweza kusababishwa na Maradhi kama Kiharusi (stroke) au maradhi mengine kwenye Ubongo
#JamiiForums #Afya #PublicHealth #Epilepsy #EpilepsyAwareness
DKT. KIGOCHA OKENG’O (Daktari Bingwa wa Mishipa ya Fahamu na Ubongo Hospitali ya Taifa Muhimbili): #Kifafa kina visababishi vingi, mojawapo ni ulaji wa Nyama ya Nguruwe, ambapo kuna minyoo inayoweza kwenda kwenye Ubongo na kusababisha kovu ambalo mwisho wake linaweza kusababisha Kifafa
#JamiiForums #Afya #PublicHealth #Epilepsy #EpilepsyAwareness
DKT. KIGOCHA OKENG’O (Daktari Bingwa wa Mishipa ya Fahamu na Ubongo Hospitali ya Taifa Muhimbili): Kabla ya kuacha Dawa za Kifafa ni vizuri kurudia kufanya Kipimo cha Kichwa ambacho kinaweza kuonesha kama Kifafa kimeisha au bado kipo
Ikitokea ukabaini #Kifafa bado kipo hata kama hakijajitokeza zaidi ya Miaka mitatu, utalazimika kuendelea kutumia Dawa
#JamiiForums #Afya #PublicHealth #Epilepsy #EpilepsyAwareness
DKT. KIGOCHA OKENG’O (Daktari Bingwa wa Mishipa ya Fahamu na Ubongo Hospitali ya Taifa Muhimbili): Kila aina ya Kifafa ina Dawa yake
Zipo Dawa zinazotibu #Kifafa cha upande mmoja na zipo za Kichwa kizima. Ukitumia Dawa tofauti inakuwa ngumu kupona
#JamiiForums #Afya #PublicHealth #EpilepsyAwareness
#MAKALA | MAMBO MUHIMU KUFAHAMU KUHUSU #KIFAFA - #ElimikaWikiendi
KIFAFA 🧠 : Ugonjwa unaoathiri mfumo wa fahamu na kusababisha mtu kupata degedege, kukakamaa, kuanguka chini na kupoteza fahamu.
Degedege
➡️Mgonjwa anaweza kuanguka mara kadhaa kwa mwezi
➡️Ugonjwa huu unadhibitiwa kwa kuzingatia matibabu sahihi
⚠️ Changamoto kubwa wanayopitia wagonjwa wanaoishi na kifafa ni kutopelekwa hospitali na kupatiwa tiba sahihi
⚠️Baadhi uhusisha kifafa na imani za kishirikina na kuishia kupoteza muda na pesa kwa waganga
⚠️Pia wagonjwa hukutana na unyanyapaa ilhali tatizo hili lina matibabu
#VISABABISHI | Kwa nini baadhi ya watu huugua KIFAFA?
- Kurithi
- Kuumia kichwa
- Magonjwa mengine (mfano homa ya uti wa mgongo)
- Uvimbe kwenye ubongo
- Matatizo wakati wa kuzaliwa
- Kiharusi
KUMBUKA:
❌ Ugonjwa wa kifafa hautokani na nguvu za giza au kurogwa.
KIFAFA huja na dalili hizi mara nyingi :
- Kuona maluweluwe
- Kisha kupoteza fahamu
- Kuanguka na kutupa miguu au mikono
- Kukaza mdomo
- Kutoa povu
- Kumalizia kwa kutoa haja ndogo au kubwa
Ukiona mojawapo ya dalili hizi, nenda haraka kwenye kituo cha huduma za afya
#MSAADA | NAMNA SAHIHI YA KUMSAIDIA MGONJWA AKIWA ANAPATA DEGEDEGE
- Mzuie mgonjwa asijiumize kwa kuweka kitu laini kama mto chini ya kichwa chake
- Ondoa vitu vyenye ncha kali karibu yake
- Usimlishe wala kuweka kitu chochote kwenye mdomo wake hadi apate fahamu
- Usimshike kuzuia mizunguko yake au anavyotikisika
- Degedege likiishi mgeuze , weka kichwa chake alalie upande mmoja ili maji/mate yasiingie njia ya hewa
- Kaa na mgonjwa hadi degedege liishe
#MATIBABU |
- Dalili za ugonjwa wa kifafa zinatibika na mtu anaweza kuishi maisha yake kawaida bila kuanguka.
- Mgonjwa anatakiwa kumeza dawa kulingana na maelekwezo
- Vituo vya huduma za afya ndo sehemu sahihi ya kwenda kwa tiba mara unapoona dalili za ugonjwa huu
Karibu kwa Maswali kuhusu Ugonjwa wa Kifafa.

Prof. William Matuja, raisi was chama cha @tzneuroscience alisisitiza kua kongamano hili litawajengea uwezo madaktari apa Tanzania kuweza kugundua kwa haraka na kutibu wagonjwa wa mishipa ya fahamu. Magonjwa kuu ni #Kiharusi #Kifafa #Ganzi au #neuropathies n.k.
It's Monday again ...have a great week!
.
.
.
#Epilepsytz #kifafa #endstigma
@WHOAFRO @FloBaing @alicenah @ChildpsychTz @rodcataldi @TashMisbah

Washindi walitangazwa kwenye Kiungo cha Gleam.
🔹Timu ya #NeuraMatrix inaungwa mkono na #TsinghuaUniversity
🔹Matokeo yao yanaweza kutumika kutibu #kifafa
Hongera!🎊
Hebu tufuate @MatrixAINetwork!
Winners announced in the Gleam Link.
🔹The #NeuraMatrix team is supported by the #TsinghuaUniversity
🔹Their results can be used to treat #epilepsy
Congratulations!🎊
Let's stay tuned to @MatrixAINetwork!
Last Seen Hashtags on Sotwe
Most Popular Users

Elon Musk 
@elonmusk
241.5M followers

Barack Obama 
@barackobama
118.8M followers

Cristiano Ronaldo 
@cristiano
114.5M followers

Donald J. Trump 
@realdonaldtrump
111.8M followers

Narendra Modi 
@narendramodi
107.1M followers

Rihanna 
@rihanna
98.7M followers

NASA 
@nasa
92.3M followers

Justin Bieber 
@justinbieber
91.8M followers

KATY PERRY 
@katyperry
90M followers

Taylor Swift 
@taylorswift13
84M followers

Lady Gaga 
@ladygaga
75.5M followers

Virat Kohli 
@imvkohli
73.5M followers

Kim Kardashian 
@kimkardashian
70.9M followers

YouTube 
@youtube
68.8M followers

Neymar Jr 
@neymarjr
66.5M followers

Bill Gates 
@billgates
65.3M followers

Selena Gomez 
@selenagomez
63.1M followers

The Ellen Show
@theellenshow
62.2M followers

CNN 
@cnn
61.7M followers

X 
@x
60.7M followers















