Zimekuja Hadithi Kunako Ruhusa Kwa Yule Ambaye Chakula Kila Tayari Na Swala Inakimiwa Bas Awe Ni Mwenye Kuanza Kula,
Akasema Shaykh Ibn 'Uthaymin [Allah Amrehem]:
"Lakin Haitakikani Kwa Mtu Kujalia Chakula Chake [Kinapikwa] Wakati Wa Swala, Lakini Lau Kama Chakula Kitokea Kuafikiana Na Muda Wa Swala Kwa Bahati Mbaya [Hamna Shida],
Ama Kule Kuwa Mtu Anajaliaa Chakula Cha Usiku Au Mchana Wakati Wa Swala, Daima Kikawa Chakula Ni Chenye Mshughulisha Kunako Swala, Hili Ni Kosa"
[التعليق على صحيح مسلم (٣/٣٩٩)]
[Mwombe Allah Mahitajio Yako Ni Mwenye Maombi]
Anasema An-Nu'amaan bin Bashir [Allah Amridhie]:
قال النبيﷺ: الدعاء هو العبادة ، ثم قرأ :وَقَالَ رَبُّكُمُ ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ
Amesema Mtume [Swala Na Salaam Ziwe Juu Yake]: Dua Ni Ibadah, Kisha Akasoma:
"Na Mola Wenu Amesema: Niombenii Mimi, Nitajibu Maombi Yenu"
[40:60]
[حسن]
[كتاب الدعاء للطبراني (٥)]
Katika Wametaja Wanachuoni Ni Kuwa Mtu [Muislaam] Anaweza Kukufuru Kwa;
1. Matendo
2. Kauli [Matamshi]
3. Shaka
4. Kwa Itiqadi
يا مقلب القلوب ثبت قلوبنا على دينك
Ewe! Mwenye Kuzigeuza Nyoyo, Zithibitishe Nyoyo Zetu Katika Dini Yako... Aamiin
Ibn Baaz kuhusu kurekodi kwa video camera mihadhara ya dini
Swali:
Ni ipi hukumu ya kurekodi mihadhara kwa kifaa cha video camera ili maeneo mengine yaweze kufaidika nao na faida ienee zaidi?
Jibu:
Hili ni jambo linalohitaji kutazamwa vizuri. Kurekodi katika kanda ni jambo linalotakikana na hakuna haja ya kuchukua picha. Lakini nyakati fulani picha inaweza kuhitajika ili mtu awe na uhakika kuwa mzungumza ni mtu fulani. Kwa sababu picha inaweka wazi yule mzungumzaji.
Kuna vilevile kuwepo sababu nyinginezo.
Mimi nimechukua msimamo wa kunyamaza juu ya jambo hili. Nimefanya hivo kutokana na zile Hadiyh zilizopokelewa kuhusu kuchukua picha viumbe vyenye roho na matishio makali ya adhabu juu ya hilo.
Ingawa wako ndugu zetu katika wanachuoni ambao wameona hakuna neno kufanya hivo kutokana na yale manufaa yenye kuenea. Lakini hata hivyo mimi katika jambo hili nimechukua msimamo wa kusimama kutokana na ile khatari kubwa ya picha.
Jengine ni kutokana na zile Hadiyth zilizothibiti kwa al-Bukhaariy, Muslim na vitabu vyenginevo zinazobainisha kwamba watu wataokuwa na adhabu kali siku ya Qiyaamah ni wale watengeneza picha na pia Hadiyth zinazowalaani watengeneza picha. Zipo Hadiyth nyenginezo vilevile.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: https://t.co/sT55BsV5Nf
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (05/355)
Imechapishwa: 26/06/2020
https://t.co/QmzgbTokEY
[Nasubiri Kifo Nikiamka Na Sijuw Ntakuja Kwa Hali Gani]
Alisema Mtu Kumwambia Al-Hasan Al-Baswrī [Allah Amrehem]:
Ni Ipi Hali Yako?? Akasema Al-Hasan: Hali Mbaya Kabisa, Akasema: Kivip Una Hali Mbaya??
Akasema: Kwa Sababu Mimi Ni Mtu Ambaye Nasubir Kifo Pindi Kukipambazuka
[Tufanye Haya Kujikumbusha Akhera]
Anasema Mtume [Swala Na Salaam Ziwe Juu Yake]:
عودوا المريض، واتبعوا الجنائز تذكركم الآخرة
Tembeleani Wagonjwa, Na Wafateni Majeneza, [Kwan Kufanya Hivyo] Kutawakumbusheni Kunako Akhera
[حسن]
[مسند الإمام أبي يعلى (١١١٩)]
[Kushikamana Na Sunnah Ni Uongofu]
Anasema Al-Imaam Az-Zuhrī [Allah Amrehem]:
Walikuwa Waliotangulia Katika Wanachuoni Wetu Ni Wenye Kusema:
الِاعْتِصَامُ بِالسُّنَّةِ نَجَاةٌ،
Kushikamana Na Sunmah Ni Uongofu
[صحيح]
[سنن الدارمي (٩٧)]
[Kuoa Ni Sababu Ya Kuchakarika]
Anasema Sheikh 'Abdul'Aziz bin 'Abdillah bin Baaz [Allah Amrehem]:
"Mwanadamu Katika Hali Ya Ujanani Na Hali Ya Kupwekeka Kwake Anakuwa Ni Mwenye Kudhoofika Kunako Kufanya Asbabu [Kazi], Na Anakuwa Ni Mwenye Kuridhia Kitu Kidogo,
Na Kwa Sababu Yeye Hana Masu'uliyah [Uwajibikaji], Lakini Pindi Atakapo Oa Anakuwa Anatambua Ni Kipi Kinamlazimu Katika Uwajibu, Na Anaongeza Katika Juhudi Zake [Za Utaftaji], Na Achkua Sababu Na Allah Humfanyia Wepsi Katika Jambo Lake Na Riziki Inatoka Kwa Allah"
[دليل الزوجين (ص١٩)]
@Rahim_Meghji@imaamnawawi@husseinabui Nimeitafuta Sana Hapo Picha Yake Ila Kiukweli Kabisa Hata Mimi Ni Eric Cantona. Na Ndiye Aliyekuja Mara Moja Kwenye Mawazo Yangu.
Ila Ronaldinho ndio Mchezaji Wangu Pendwa wa Wakati Wote.