@SB_Ladder Video za ngono ni sumu mbaya sana, inaua kiroho na kimwili, mtu anayeangalia picha za ngono anajiua mwenyewe na kupoteza uhusiano mzuri na Mungu wake.
Pitisha kijana wako kwenye mkondo wa Certificate ➡️ Diploma. Hakikisha anafanya kozi yenye vitendo ... mfano, upimaji ardhi, utaalamu wa umeme wa magari, automotive software engineering, machine tools, landscaping, oil and mining engineering
Msisitizie ajibidiishe kufanya yafuatayo:
- atie bidii ktk mafunzo ya vitendo
- apende kujitolea darasani na nje ya darasa
- atafute namna anavyoweza kuchanganya masomo yake ya vitendo na stadi za kompyuta
Uwe na Jumapili njema.
Wapo wahafidhina wanauliza, Balozi Polepole alikuwa wapi wakati watu wanatekwa, kupotea na kuokotwa katika viroba Coco Beach huku yeye akiwa kiongozi wa CCM, wakati wa uongozi wa Hayati J.P. Magufuli... Mbona hakujiuzulu..?
MAJIBU:
Soma paragraph ya nne ya barua ya Balozi Polepole inajieleza.
"kwa muda wote wa kuhudumu ndani na nje ya nchi,nimefuatilia kwa karibu na kushuhudia kwa masikitiko makubwa mwelekeo wa uongozi usiojielekeza ipasavyo katika kusimamia haki za watu, amani na kuheshimu watu,kufifia kwa dhamira ya kweli na uwajibikaji wa dhati wa kushughulikia kero na changamoto zao,na kudidimia kwa maadili ya uongozi katika ngazi mbalimbal.
Kudhoofika kwa utekelezaji wa majukumu ya msingi ya serikali kwa ajili ya ustawi wa wananchi; mambo haya yanateteresha maslahi mapana ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Haya yote yamezidi kunifanya nikose amani ya moyo na imani katika uongozi niliopo ndani yake sasa.."
SOMA:
Biblia takatifu kwa sisi wakristu inasema;
"Nawaambia, vivyo hivyo kutakuwa na furaha mbinguni kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye, kuliko kwa ajili ya wenye haki tisini na kenda ambao hawana haja ya kutubu." Luka 15:7-10
Yanakuja hata CCM hawataelewa kitakachowapata! Mngejua ninayojua mngekuwa mnacheka tu wanavyohaha
Anyway naendelea kuwakumbusha
Keep Calm na tusimame hapohapo bila kuyumba #NoReformsNoElection 👊🏽🔥
Kelele mingi tu upande wao! Sisi tuko calm and focused! 😁
Askofu Gwajima amefungiwa kanisa kwa kudai haki ya watu kuishi, kwa kupinga mauaji na utekaji..
Hakuna kosa mtu kupinga dhambi kanisani.
Wengine kwasababu wako karibu na utawala wanaona hayo hayawahusu, kwamba hayo ni ya Gwajima.
Ndio maana hata walipokutana na Mtawala walikua wanamsifia badala ya kumwambia kwmaba anakosea.
Jana mtu ametumia kanisa kuhamasisha watu kukatwa vichwa akapigiwa makofi.
Kwamba Nchi imefikia sehemu ukipinga dhambi unaadhibiwa ukitetea dhambi na uovu unashangiliwa..
Ukweli ni kwamba haki itashinda na dhambi itashindwa.
Dhamira yenu kutaka kumdhuru Lissu tunaijua…
Huyu hawezi kuzungumza mbele ya Rais jambo ambalo halielewi, the fact kwamba ameropoka ni kama ile Waswahili walisema “ulimi umeiba Siri ya moyo”
Chochote kibaya kikimtokea Lissu serikali hii itawajibika.#NorefomsNoelection
Ziko wapi zile Madhabau kama za wakina Shadrach, Meshach, and Abednego. Mwenyezi Mungu adhihakiwi na hawezi tengenezewa mikakati ya kumfanya mpumbavu.Malipo yanakuja haraka sana na kwa hasira yake.
🔴 #DHARURA | 05.07.2025
Tunaomba msaada wa damu Group O+ (Positive) kwa ajili ya mgonjwa aliyelazwa Hospitali ya HURUMA – Rombo.
Hali ni mbaya, anahitaji upasuaji wa dharura.
📞 Mawasiliano: 0744 904 621
Tafadhali sambaza ujumbe huu kuokoa maisha. 🙏
“Acheni Unafiki– Mauaji ya Enock ni zao la mfumo wa CCM”
Kuna jambo moja la kusikitisha kuliko mauaji ya kijana Enock Mhangwa ni unafiki wa viongozi wa UVCCM kujifanya wameshtushwa na jambo walilolilea.Enock hakuuliwa na majambazi. Ameuliwa na watu waliovaa mamlaka ya serikali ya CCM. Viongozi wa mtaa waliopaswa kumlinda ndio waliompiga hadi kufa kwa tuhuma tu. Huo ndio mfumo wa hofu, ubabe na uonevu ambao CCM mmeutengeneza kila ngazi ktk Nchi.Sasa mnakuja na kauli za “kulaani” wakati mmejenga mfumo wa kutokuwajibika, mmegeuza vyombo vya dola kuwa silaha za kisiasa, na mmelea utamaduni wa kujichukulia sheria mkononi.Hamna haki ya kusema “tunalaani” wakati mmewasha moto wenyewe. Kauli zenu hazina maana kama hamko tayari kusafisha mfumo wenu.Watanzania wanajua ukweli. Na hawadanganyiki tena.
Tumevumilia utawala wao kwa miaka 60. Ila wao hawataki kuvumilia maoni yetu. Tunatekwa na kuuliwa. Tunapewa kesi ngumu tuozee jela. Tunafilisiwa na kutengwa. Tunahitaji ishara gani zaidi ili tuseme imetosha? #NoReformsNoElection