Leo tarehe 28 Mei 2026 Mahakama Kuu Masijala ya Dar es salaam imetoa uamuzi na kukubaliana na hoja Chama kwamba kitendo cha waleta madai kushindwa kuonesha lini hasa madai yao yalianza kinainyima mahakama nafasi ya kujiridhisha kama kweli inayo mamlaka ya kusikiliza madai husika.
Kufuatia hali hiyo, kesi hiyo namba 8323/2025 imefutwa rasmi leo.
‼️HASHAURIKI SSH SI KWAMBA HAJASHAURIWA‼️
Nina taarifa za kutosha kuwa Suluhu the Butcher aka Mwuaji In Chief ameshauriwa SANA tokea Novemba na watu ndani na nje ya nchi, wakubwa kwa wadogo, wastaafu na walio in active duty!
Alishauriwa na kila mtu amwachie Tundu Lissu na awaachie wafungwa wa kisiasa, akubali na akiri mauaji halaiki na awajibishe waliotekeleza mauaji - kwa njia hii atapunguza joto kali! (FYI Hakuna aliyemshauri ajiuzulu 🙄 ila mi nasema ndo ushauri pekee anatakiwa kupewa!)
Eniwei hiki kimama kiburi sana na ana bifu za kitaarab kagomea ushauri wa kila mtu! Hata Chadema kakubali ifunguliwe kwa sababu anataka kurudisha Njaa 54 waivuruge na waingie maridhiano! Completely delusional! 🙄 She is a lost cause!
Sasa watu wote wenye akili na upeo wa kuchanganua wamenawa mikono! Ndo mnaona action hizi zimeanza kimataifa na soon kila kitu kitasimama kitaifa! Hajui hata namna ya kulipa mishahara na wanamwangalia tu! Wamemwacha aendeshe mambo anavyojua - sasa ye kutwa washauri ni Abdul, Madilu na Bashite - wao wanachojua ni kuteka, kuua, weka ndani, kutisha na kuleta maigizo!
Nchi ina kwenda kwisha hivo! Kwa nini mnaogopa kumwambia aondoke!?
Kweli tusumbuliwe watu milioni 70 na genge ndogo hivi?
Lissu mwachieni tupate kiongozi wa kweli, nchi ikae sawa kwanza huyu kimama atoke!
Save this country! Hatuwezi wanaharakati au CHADEMA peke yetu! Wake up everyone and take action!
#FreeTunduLissu #SamiaMustGo
Mtamdao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) kwa kushirikiana na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), wametoa wito mzito kwa wananchi kote nchini kuunda vikundi vya ulinzi shirikishi (polisi jamii) ili kukabiliana na wimbi jipya la matukio ya utekaji na kupotezwa kwa watu linaloendelea kutikisa taifa. Taasisi hizo zimesisitiza kuwa mshikamano wa dhati wa raia ndio ngome kuu ya sasa katika kulinda usalama wa maisha yao na haki za kikatiba.
Katika tamko la pamoja lililotolewa leo Mei 22, 2026, na Mratibu wa Kitaifa wa THRDC, Wakili Onesmo Olengurumwa, pamoja na Rais wa TLS, Wakili Boniface Mwabukusi, mashirika hayo yamepongeza ujasiri wa madereva bodaboda na wananchi wa Bunju, Dar es Salaam, waliojitokeza kufuatilia gari lililomteka David Joseph Mghanja (Jumbe), msaidizi binafsi wa Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, usiku wa tarehe 20 Mei, na kufanikiwa kuokoa maisha yake. Kitendo hicho kimetajwa kama mfano wa kuigwa wa namna jamii inavyopaswa kukataa hofu.
Mawakili hao wakuu wameeleza kusikitishwa kwao na takwimu zinazoonyesha kuwa watu zaidi ya 300 wameshatekwa katika mazingira tatanishi ndani ya miaka saba iliyopita, huku takwimu za hivi karibuni za Tume ya Jaji Chande zikitaja idadi hiyo kufikia zaidi ya watu 800. THRDC na TLS zimebainisha kuwa kuongezeka kwa matukio hayo huku kukiwa hakuna hatua madhubuti zinazochukuliwa, kunadhoofisha utawala wa sheria na taswira ya nchi katika kuheshimu haki za binadamu na demokrasia.
Kufuatia hali hiyo, taasisi hizo zimeitaka Serikali kuunda chombo huru cha kiraia kuchunguza tuhuma za uwepo wa mtandao wa utekaji unaodaiwa kushirikiana na baadhi ya watu ndani ya vyombo vya usalama, zikisema Jeshi la Polisi haliwezi kufanya uchunguzi huru kwani lenyewe ni sehemu ya watuhumiwa. Aidha, wametoa wito kwa Serikali kuridhia haraka Mikataba ya Kimataifa Dhidi ya Mateso na Kupotezwa kwa Nguvu ili kuimarisha uwajibikaji na kulinda uhuru wa raia kwa mujibu wa Katiba.
Mwenyekiti wa Chama Taifa Mhe. Tundu Lissu akiwasili Mahakama Kuu Masijali ya Dar es salaam ambapo leo tarehe 25 Mei 2026 shauri lake la kutaka ajumuishwe kwenye kesi ya mali za Chama iliyofunguliwa na Saidi Issa Mohamed na wenzake wawili itaanza kusikilizwa.