Mwanariadha wa Kenya Abel Mutai alikuwa karibu na mstari wa kumaliza mbio, akachanganya alama za kumaliza mbio na kusimama akifikiri ameshaliza na ni mshindi, ingawa hakuwa amevuka mstari ili kuwa mshindi wa kwanza, mita kumi kabla ya finish line.
Mwanariadha wa Hispania Ivan Fernandez alikuwa nyuma yake na akagundua Mutai amechanganya na kusimama kabla ya kuvuka mstari wa ushindi.
Angempita na kuvuka mstari ili awe wa kwanza?
Aliamua kumkumbusha bado hajavuka mstari wa ushindi na kumtaka amalize, akimwambia kwa Kihispania ambacho Mutai hakuwa anaelewa hivyo alitumia nguvu ya ziada hadi kumsukuma avuke mtari ndio afuate yeye katika nafasi ya pili๐
Fernandez alimpelekea Mutai kumaliza mbio zile na kuwa wa kwanza na yeye wa pili.
Alipoulizwa kwa nini alimsadia Mutai na yeye akawa wa pili licha ya kuwa na nafasi ya kuwa wa kwanza akasema
"Ndoto yangu ni siku moja kuwa na maisha kwenye jamii inayoweza kusaidiana na kusukuma kwenye mafanikio "
"Sijamfanya ashinde, hizi zilikuwa mbio zake, alistahili kushinda yeye kwani alikuwa na nafasi ya kufanya hivyo"
"Nini faida ya ushindi huu? Heshima ya medali hiyo itakuwa wapi? Mama yangu atanichukulia vipi?"
"Wengi wetu tunajinufaisha na madhaifu ya wenzetu badala ya kuchukua nafasi hiyo kuwapa nguvu na kuwafanya kuwa Bora"
Hii ilitokea kwenye mbio za Burlada, Hispania mwaka 2012.
Ivan hakushinda mbio hizo kuwa wa kwanza lakini alishinda mioyo ya wengi.
Angeshinda huenda asingekumbukwa kama anavyokumbukwa kwa alichokifanya kwa Mutai.
Watu wema hawajaisha, tenda wema!