Kama unamjua mpanga mauaji kwa nini serikali iingie gharama zote hizo. Nashuari peleka maandiko kwa Mama ili tume isiwe na kazi ngumu ya uchunguzi. By then unaamika na mfumo.
HAWA WATU NI WENDAWAZIMU KABISA
Kuna muda unajizuia kuwasema hawa watu lakini inashindikana maana kiwango chao cha wehu ni cha hali ya juu sana na kwa kweli kinatisha mno.!
YAANI mpaka leo mko kwenye denial hamtaki kukubali kuwa Rais Samia ndiyo Rais na kiongozi halali wa hii nchi na nchi imeshaondoka kwenye poroho zenu za kutaka kufanya mapinduzi na sasa watu wanaangalia mambo mengine ya maana kwa ajili ya watanzania.
YAANI leo mkiwa na akili zenu timamu kabisa mnaweza kuikataa tune ya Jaji Lila? Kwani mnaogopa nini? Au mnaogopa kuwa mtakutwa na hatia maana tayari tunajua kuwa moja ya watu waliohusika kupanga machafuko na vurugu zile alikuwa ni Heche aka Domo Kaya.
AU haya mnayafanya sasa baada ya kuona Chiba hana nafasi ya kuvua kitanzi ambacho kuna kila dalili ameshakivaa ni suala la muda tu kukifyatua aende na maji?
TUME ya Jaji Lila iliundwa kwa mujibu wa sheria na kwa muongozo wa mambo yakiyobainika kwenye kazi ya tume ya Jaji Chande na ikaagizwa iundwe tume ya jinai kwa kuwa kuna jinai za kutosha zimefanyika kwenye machafuko yale.
TUME ya Jaji Lila itakuja na majibu ya nani alipanga na kufadhili vurugu zile na machafuko yale.. Itakuja na list ya wahusika na walifandhili mapinduzi yale yaliyofeli.!
NA TUME hii iliundwa kwa mujibu wa sheria na mnalijua hilo lakini leo kwa kuwa mmeshahisi kuwa joto limekuwa kali sana mnataka kuanza porojo na kutilisha huruma hapa!..
CHADEMA mbona kama mna wasiwasi sana na hizi tume? Kwani mna shida gani? Kama hamkuhusika na vurugu zile mbona presha na kisukari kinawapanda sana? Kulikoni yaani?
NYIE si hamumtambui Rais na hamtaki kuheshimu mamlaka zilizopo!.. Endeleeni tu mtafika sehemu mnayoitaka siku si nyingi
#KigogoMediaUpdates
🚨LEO TUNAAMKA NA HABARI KUBWA ANZA KWA KUREPOST.
COMMONWEALTH MINISTERIAL ACTION GROUP
WAMETOA RATIBA YA HATUA ZA UTEKELEZAJI KWA TANZANIA NDANI YA SIKU 30, 60 NA 90
Pamoja na mambo mengine Serikali haram ya Nduli Idd Amin Mama imepewa siku 30 iwe imetatua suala la kuzuiliwa kwa Mhe. @TunduALissu kupitia njia ya kisiasa na kisheria lakini pia kuwaachilia huru watu wengine wote wanaoshikiliwa kwa sababu tu ya kutumia haki zao za msingi kwa njia ya amani.
Ndani ya siku 60 wameambiwa warejeshe upatikanaji kamili wa majukwaa ya kidijitali (digital platforms) kusitisha vitendo vya vitisho na unyanyasaji dhidi ya vyombo vya habari na watetezi wa uhuru wa kujieleza.
Ndani ya siku 90 wahakikishe waitishe jukwaa la kuaminika na shirikishi la mashauriano kati ya vyama vya siasa, likiwa na wawezeshaji wasioegemea upande wowote yani Jukwaa hilo liwe na mamlaka ya kujadili na kukubaliana kuhusu marekebisho ya mfumo wa uchaguzi, ushindani wa kisiasa, suala la watu waliowekwa kizuizini na uwajibikaji.
Lakini pia wametoa Onyo la Septemba 2026 kwamba Tanzania imeamriwa kuwasilisha ripoti ya utekelezaji wa mambo hayo kabla ya mkutano maalum utakaofanyika Septemba 2026.
Onyo la Novemba 2026 (Hatua Kali): Jumuiya ya Madola imetoa onyo la mwisho kwamba isipoona maendeleo yoyote kufikia Novemba 2026, itachukua hatua kali zaidi dhidi ya Tanzania (ambayo kwa sasa tayari ipo chini ya uangalizi kwenye Agenda Rasmi
Acha kuendelee kuwaka.
TUTAKUWEPO🫵🏾😎
Jana nilipokwenda kuhuduria Kongamano la wanafunzi wa vyuo vikuu Chaso.
Walitumwa baadhi ya vijana kutoka UVCCM, kwa kulipwa vifedha kidogo…
Sina tatizo na vijana hata kama ni wa ccm kuhudhuria na kusikiliza sera, misimamo na hoja zetu.
Lakini huyu kijana, watu wetu walipomgundua na kumhoji alisema alikua ameambiwa kwamba tukianza kuzungumza kuhusu ripoti ya Chande wazomee..
Lakini pia wafanye fujo na kutoka ukumbuni, ionekane vijana hawakutusikiliza.
Kwenye simu yake alikua anawasiliana na mtu anaitwa Shangwe Mtei ambae ni kiongozi wa Uvccm.
Huyu Shangwe akawa anamhakikishia kwamba hata kama wako wachache wafanye fujo kwasababu OCD alikuwepo nao pale.
Ghafla huyu kijana akiwa anahojiwa na watu wetu kwanini yuko pale na nia yake ni ipi, Magari mawili ya polisi yalikuja pale kitendo kinachoonesha kwamba tukio hili lilikua limepangwa kwa ushirikiano huo.
Huyu kijana alikua ametumiwa muamala wa sh 50,000 kwa madai yake walitumiwa wote na wenzake, na walipatwa hofu na kutokufanya fujo kwasababu vijana wa Chaso walikua wengi zaidi na pia ulinzi ulikua imara..
Fikiria kwamba huyu ni kijana wa chuo kikuu ana fikra na mawazo ya kutumwa na kulipwa sh 50 elfu!!
Tuna safari ndefu kama Nchi Lakini lazima tufike..
Asante watu wetu wa ulinzi kwa kazi nzuri.
@HakiBalozi255@joeselasini Tatizo kabla lako. Tangu enzi huwa mnajiona mnafikra bora kuliko wengine. Umri sio tija ya fikra kama unaweza ondoa nyeti ili uepuke fikra za 18, 20.Acha dharau