. @realDonaldTrump After Iran, please turn your attention to Tanzania.
The CCM regime is a carbon copy of the brutal Islamic regime in Iran. If they had a capable army, they would gladly join the war and stand beside Iran. The only reason they have not is because they know their limits. Their weapons are only strong enough to kill unarmed citizens, but not strong enough to play with the big boys. They are cowards.
Just three months ago, Samia Suluhu and the CCM regime murdered more than 10,000 Tanzanians who were protesting. They simply opened fire and shot people in the streets. Now they are openly showing the world which side they stand with.
This is who CCM truly is , a regime of cold-blooded killers.
@realDonaldTrump, Samia Suluhu is the Khamenei of East Africa. We Tanzanians will keep fighting for our freedom on our own if we must. But if there is any way you can help us win this fight, we desperately need it. Without help, this regime will continue shooting its own people just to cling to power.
@SFRCdems@SenateForeign@StateDept@HouseForeignGOP@HouseForeign@Europarl_EN
I would like to say publicly that representing Tundu Lissu, a far brighter lawyer than me is one of the highlights of my career. Shot over a dozen times and campaigning with a verve and strength that defies imagination. Gd bless him and Tanzania!
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 216
Jaji Ndunguru: Mshitakiwa Maswali ya Dodoso.
Anasimama Mheshimiwa Lissu kwa ajili ya kumfanyia Cross Examination Shahidi ambae anaitwa Coplo Amani.
Mhe. Lissu: Waheshimiwa kwa kuanzia naomba nipatiwe kielelezo D12, waheshimiwa majaji haya ni maelezo ya P3.
Mhe. Lissu : Sasa shahidi naomba uwaeleze majaji kama uliandika maelezo polisi
Coplo Amani : ni sahihi
Mhe. Lissu: waeleze majaji kama unaweza kuyatambua ukionyeshwa
Coplo Amani : nikionyeshwa nitaweza kuyatambua
Mhe. Lissu: naomba shahidi aonyeshwe maelezo yake aliyoandika polisi.
Coplo Amani : haya ndio maelezo yangu
Mhe. Lissu: asante sana, sasa shahidi hayo maelezo yako naomba uwaeleze majaji kama uliyaandika mwenyewe au uliandikiwa na askari mwingine?
Coplo Amani : haya maelezo niliandikiwa na askari mwingine
Mhe. Lissu: mtaje jina tafadhali
Coplo Amani : Anaitwa H9207 detective coplo Robert
Mhe. Lissu: Kwenye maelezo yako hayo waeleze majaji kama ni utaratibu mtu anayeandika maelezo ya shahidi hawezi akawa ndio mtu huyohuyo kama shahidi?
Coplo Amani : ni sahihi
Mhe. Lissu: Waheshimiwa majaji pamoja na majibu mazuri ya shahidi huyu nataka ku-impeach credibility yake, nitamsomea maelezo yake, nitamuonyesha maeneo nitakayotaka kumuuliza maswali halafu nitamtaka ayawasilishe kama kilelezo.
Mhe. Lissu anamsomea maelezo yake
Mhe. Lissu : Haya ndio maelezo yako kama nilivyoyasoma?
Coplo Amani : Waheshimiwa majaji mshtakiwa kuna maeneo amekosea naomba nimrekebishe, sio kata ya Isuesue ni Isyesye 😁
Mhe. Lissu: Waheshimiwa majaji kwakua na nyie mnarekodi hii mimi nimeona imeandikwa isuesue waheshimiwa…
Kwenye maneno “ni dereva wa bodaboda isuesue Mwintengule”… kwenye original Isyesye… kwahiyo tutaenda na ya kwako.
Kuna eneo lingine ambalo lina shida?
Coplo Amani : hapana.
Mhe. Lissu : Sasa kuna maeneo nataka kukuhoji kwa ajili ya kukukanusha kama ifuatavyo;
1. Kwamba unafanya kazi chini ya OCCID Mbeya mjini
2. Kwamba wewe ni msaidizi wa upelelezi ndani ya Mbeya mjini
3. Umeelezea Kituo cha Polisi cha Ilomba kwamba ni kituo kidogo kilichopo chini ya kituo cha Kati Mbeya umesema ni kama out post.
4. Umeeleza kwamba kaimu OCCID Inspekta Jorum alipokupa maelekezo ya kwenda kumkamata P3 alikupa namba ya simu ya askari wa kitengo cha intelijensia kwa ajili ya kwenda kumkamata P3
5. Kwamba hawa askari huwa wanajichanganya na raia kama dereva boda boda n.k
6. Baada ya kupewa namba ya simu ukawasiliama nae na mkakutana Isyesye.
7. Kwamba kulikua na watu wengi na mlipita na akakuonyesha mtuhumiwa kwenye kituo cha boda boda.
8. Taarifa mlizopewa na Jorum ni mtuhumiwa ndiye anayehamasisha wenzake kufanya vurugu uchaguzi wa 2025
9. Baada ya kuonyeshwa huyo mtuhumiwa ulimfata na kumtoa pembeni ya kijiwe na kisha ulijitambulisha kwake kwa jina na kumueleza tuhuma zake.
10. Ulimwambia baada ya kumtoa pembeni kwamba anahitajika Kituo cha Polisi Ilomba na yeye alikubali kwenda.
11. Ni ushahidi wako maelezo aliyoandika mtuhumiwa ni uchochezi, kusababisha vurugu na kuzuia uchaguzi mkuu wa 2025.
12. Shitaka uliloandika lilikua ni kukiuka masharti ya kifungu cha 390 cha Penal code
13. Wakati ukimhoji alikwambia kwamba aliona taarifa kwenye YouTube akamuona Lissu akiwa anahamisisha uasi, kufanya vurugu na kuharibu uchaguzi 2025.
14. Baada ya kuandika maelezo yake ulimjulisha inspeka Jorum akakuelekea kumuachia kwa dhamana na we anaripoti kila baada ya siku tatu
15. Ni ushahidi unaohusu tareh 17 april 2025 kwamba siku hiyo wakati ukiwa Ilomba Kituo cha Polisi ulielekezwa na inspekta Horum kuandika maelezo ya mtuhumiwa kama shahidi kuhusiana maelezo ya Mwenyekiti wake Tundu Lissu na yeye kuwa mstari wa mbele kuhamasisha vijana wenzake kufanya vurugu.
16. Baada ya kurekodi malezo hayo na ulimjulisha Inspekta Jorum na ukamkabidhi malezo hayo.
Part 217 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
Lissu amewauliza mashahidi WOTE wa kificho kama wametishiwa maisha na mtu yeyote, na wote wamejibu HAPANA. Kwa msiofahamu, DPP aliiomba mahakama kuficha mashahidi hawa kwa sababu WAMETISHIWA maisha yao. Anachokifanya Lissu ni kuithibitishia mahakama kuwa DPP & POLISI ni waongo.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo February 17, 2026
Jana tuliishia Part 182 so leo tunaendelea na-;
Part 183
Mhe. Tundu Lissu ameingia muda huu leo makamanda wanaimba Shujaaa Shujaaa Shujaa.
Amepiga Tshirt yake nyeusi hapa.
Majaji nao wanaingia kama kawaida yupo
1. Jaji Dunstan Ndunguru Kiongozi wa Jopo.
2. Jaji James Karayemaha
3. Jaji Ferdinand Kiwonde
Wote watatu wapo wakiwa kwenye majoho yao mekundu na Beib nyeupe.
Renatus Mkude anasimama, yupo na ajuaye, Thawabu Issa, Ignas, Winiwa Kasawa pia.
Anasema leo wako na mashahidi watatu na tuko tayari kuendelea.
Jaji anamuuliza Mshitakiwa nae anamjibu niko tayari.
Majaji wanaandika kidogo.
Ukimfuatilia Mwenyekiti wa Jopo la Majaji, Jaji Ndunguru amekuwa anaonekana ni mtu mstaarabu.
PF 1864 ASP Geofrey Lutufye
Anaingia hapa kizimbani huyu ni askari huyu ni PW 9 ni shahidi ambae muonekano wake yupo kama amekesha hajanyoa nywele, ameshika kipaza sauti anatetemeka.
Naitwa PF18544 ASP Geofrey Aggrey Lutufye
Umri wa miaka 47.
Naishi Arusha.
Mkristu.
Huyu shahidi leo atadondoka kizimbani maana kwa anavotetemeka wote tunamuona hapa, Ukikutana nae barabarani huwezi sema ni Polisi maana amidevu na minywele yupo rafu sana.
Anaongozwa na Renatus Mkude.
Anaanza Renatus Mkude kumuuliza Maswali.
Wakili: Ikumbushe mahakama majina yako.
ASP Geofrey Lutufye: Anataja majina yake hapa
Wakili: Kazi yako?
ASP Geofrey Lutufye: upelelezi, niko ofisi ya mkuu wa upelelezi Arusha na mimi ni kiongozi wa kikosi cha Anti Robbery
Wakili: Anti Robbery ni nini?
ASP Geofrey Lutufye: Kikosi cha kuzuia uhalifu kama vile uporaji.
Kumbe ndio maana ana hali hii huyu askari. maana kiukweli amekaa hovyo sana kumbe anadeal na mambo ya kupora.
Wakili : Umepata mafunzo gani?
ASP Geofrey Lutufye: Nilipata tarehe 28/04/2003 Chuo cha Polisi Moshi.
Nilijifunza upelelezi na mafunzo mengine mbalimbali, nilimaliza mwezi wa 11, 2003.
Mafunzo mengine nilipata ya nyota ya kwanza, nilisomea Chuo cha Polisi Moshi ilikuwa ni Mwaka 2013 na baadae mafunzo ya cheo cha Mrakibu Msaidizi wa Polisi. Nililipata chuo Dar es salaam Polisi Academy hapa Dar es salaam nilimaliza mwezi wa 11 mwaka 2023.
Wakili: kingine ni nini?
ASP Geofrey Lutufye: Mengine ni on job trainning yaani mafunzo kazini.
Wakili: Una uzoefu kazini wa mwaka gani?
ASP Geofrey Lutufye: Miaka 15 ya upelelezi ninayo.
Wakili: Arusha uko tangu lini ofisi ya upelelezi.
ASP Geofrey Lutufye: Tangu mwaka 2023.
Wakili: kabla ya hapo ulikuwa wapi?
ASP Geofrey Lutufye: Nilianzia Polisi Oysterbay Dar es salaam, nilianza kama General Duty na baadae nikapelekwa Geita Ofisi ya Upelelezi wa makosa ya jinai mkoa wa Geita ndo nikahamia mkoa wa Arusha baada ya huko.
Wakili: Majukumu yako hapo ofisi ya Upelelezi Arusha ni yapi?
ASP Geofrey Lutufye: Kufanya doria mbalimbali, kukamata watuhumiwa, kufanya upelelezi na kuwafikishia watuhumiwa Mahakamani.
Wakili: Tarehe 03/04/2025 kilitokea nini?
ASP Geofrey Lutufye: Nilikuwa na wenzangu tukiwa na section 1 ambayo ni askari 9 hadi na dereva tukiwa kwenye doria.
Wakili: Nini kiliendelea?
ASP Geofrey Lutufye: Tulikuwa tunafanya doria tukiwa tunatumia gari la Polisi aina ya Toyota Landcruiser na nikapata maelekezo kutoka kwa kaimu mkuu wa upelelekezi ASP Bonny Mgogo.
Wakili: kwa njia ulipata maelekezo?
ASP Geofrey Lutufye: Nilipata kwa njia ya radio call ambayo ni kifaa cha mawasiliano. Maelekezo kuwa amepata taarifa kutoka kwa msiri kuwa kwa Mromboo kijiwe cha Bajaji kuna vijana wanahamasishana kuzuia uchaguzi wa mwaka 2025.
Wakili: Baada ya kufika huko kwa Mromboo nini kiliendelea?
ASP Geofrey Lutufye: Nilikuta vijana wakila njama za kuzuia uchaguzi Mkuu 2025.
Jaji anasema umesema Walikuwa wanakula nini?
ASP Geofrey Lutufye: Walikuwa wanazungumzia uchaguzi mkuu wa 2025.
Jaji: Kumbe walikuwa wanazungumzia sio kula tena?
Watu wanacheka.😂😂😂
Part 184 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 184
Wakili wa Serikali anaendelea kumuongoza shahidi
Jaji: Endeleeni
Wakili: Eheee kikaendelea nini?
ASP Geofrey Lutufye: Nilivyowakuta wale vijana waliokuwa wanakula njama nikawaambia wako chini ya Ulinzi.
Jaji: Hiyo MIC ameshikaje mbona hasikiki?
Wakili: ikawaje shahidi?
ASP Geofrey Lutufye: Tuliwakamata P4 na P7 ambao walikuwa wameanza kukimbia baada ya hapo nilitoa maekekezo wapelekwe kituo cha Polisi Murieti, hao askari ni wanne, kituo cha Murieti kipo Mkoa wa Arusha.
Wakili: Nini kiliendelea?
ASP Geofrey Lutufye: Sisi tuliendelea kuwatafuta waliokuwepo pale lakini hatukufanikiwa kuwakamata.
Wakili: Nini kingine kiliendelea?
ASP Geofrey Lutufye: Waliacha Bajaji zao tukazichukua na kuzipeleka kituo cha Polisi Murieti na mbili zilikuwa za wale watuhumiwa tuliowakamata.
Wakili: Nini kiliendelea?
ASP Geofrey Lutufye: Majira ya saa moja ndio tulizipeleka hizo Bajaji kituo cha Polisi Murieti.
Wakili: Kituo cha Polisi Murieti nini kiliendelea?
ASP Geofrey Lutufye: Ulipata maelekezo kutoka kwa kaimu mkuu wa upelelezi Arusha.
Maelekezo hayo yalinitaka niwapeleke ofisi za mkuu wa upelelezi Arusha, tukiwa njiani tunawapeleka P4 na P7 niliwahoji kwamba kwanini mnahusika kula njama kutaka uchaguzi mkuu wa 2025 usifanyike?
Wakili: Ikawaje?
ASP Geofrey Lutufye: Wote walikiri kuwa wanamuunga mkono Mwenyekiti wa Chadema Tundu Lissu kutokana na ile kauli yake aliyoitoa kwenye Mtandao kuwa atazuia Uchaguzi, ataleta uchochezi na atakinukisha.
Wakili: Nini kiliendelea?
ASP Geofrey Lutufye: Tuliwafikisha Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Arusha majira ya saa mbili.
Wakili: Nini kiliendelea?
ASP Geofrey Lutufye: Nilipewa maelekezo tena nifungue jalada la Uchunguzi, nilifungua jalada hilo ambalo ni ARS/D/CID/B/40/2025.
Wakili: Kikaendelea nini?
ASP Geofrey Lutufye: Nikapewa maelekezo tena na Kaimu Mkuu wa Upelelezi Arusha yakinitaka niwahoji watuhumiwa hao kwa kuchukuliwa maelezo yao.
Wakili: Nini kiliendelea?
ASP Geofrey Lutufye: Mimi niliwaa asign maaskari wengine wa RCO wawachukue maelezo na mimi nikaendelea na majukumu mengine.
Wakili: Kingine kilichoendleea?
ASP Geofrey Lutufye: Niliandika maelezo yangu Tarehe 18/04/2025.
Renatus Mkude, Wakili wa Serikali. Ni hayo tu Mheshimiwa Jaji kwa shahidi huyu.
Watu wanaangalia usoni wanacheka.😂
Jaji Ndunguru: Maswali ya Dodoso
Mhe. Lissu anasimama: Shahidi naomba nikuulize maswali na ujibu maswali yangu kwa kadri nitakavyokuuliza.
Sasa waeleze majaji, Huko Polisi mnakojifunzia hizi kazi huwa mnafundishwa kuwa waongo?
ASP Geofrey Lutufye: Hatufundishwi kuwa waongo.
Mhe. Lissu: waeleze majaji kama huwa mnafundishwa mnapotoa ushahidi mahakamani kuongeza maneno ambayo hayapo?
ASP Geofrey Lutufye: Hatufundishwi.
Mhe. Lissu: waeleze majaji kama huko Polisi mnafundishwa kutokuwa na heshima?
ASP Geofrey Lutufye: Sio kweli
Mhe. Lissu: Waeleze majaji kama huko Polisi mnafundishwa watu wasio na maadili?
ASP Geofrey Lutufye: Sio kweli
Mhe. Lissu: Sio kweli nini sasa?
ASP Geofrey Lutufye: Tunafundishwa kuwa watu wenye maadili.
Mhe. Lissu: Unafahamu kitu kinaitwa PGO?
ASP Geofrey Lutufye: Amekaa kimya kidogo, PGO naifahamu mimi.
Mhe. Lissu: waeleze majaji kama ni sahihi au sio sahihi kwamba PGO inasema askari wanapaswa kuwa weledi kwenye kazi zao?
ASP Geofrey Lutufye: Ni kweli inasema hivyo.
Mhe. Lissu: Waeleze majaji kwa mujibu wa PGO Polisi wanatakiwa kuwa waaminifu. Anamsomea PGO hapa. Wasiwe mafisadi na wawe wakweli
ASP Geofrey Lutufye: Ni kweli.
MheLissu: Hii PGO leo tutacheza nayo sana. Umesema uliandika maelezo yako Polisi?
ASP Geofrey Lutufye: Ni kweli niliandika na naweza kuyatambua.
Mhe. Lissu: Mheshimiwa Jaji naomba apewe maelezo yake.
Anatafutiwa na kupewa hapa.
ASP Geofrey Lutufye: Haya ndio maelezo uliyoandika Tarehe 18/04 mwaka jana.
Part 185 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo February 16, 2026
Jana tuliishia Part 177 so leo tunaendelea na-;
Part 178.
Majaji wanaingia wakati huo sauti ya Courtttt imepigwa kwa sauti kubwa.
Kelele za Rais Rais Rais kama ilivyo ada pia zinapigwa zikianzia kule juu.
Mh. Lissu amepiga Tshirt yake ya No Reforms, No Election.
Majaji wanaandika kidogo.
Kama kawaida Mawakili wa Serikali wapo karibia 10 siku zote huwa wanajitahidi kuwa wengi sana. 😂
Mhe. Lissu pia anateta kwa mbali na vijana wake pale wapo Mawakili Ikoti Lissu, Deogratias Mahinyila, Michael Lugina na Sisty Aloyce.
Anasimama Renatus Mkude anawatambulisha wenzake na kusema wana mashahidi wawili wanaolindwa na wako tayari.
Shahidi amesubiriwa kwa muda mrefu sana.
Jaji anauliza mmeenda kumatafutia wapi?
Yupo Mheshimiwa anajibiwa.
Jaji huyo shahidi ni nani?
Renatus mkude: Ni P2 huyu.
Jaji: Shahidi una miaka mingapi?
Shahidi wa kificho P2: 38
Jaji: Dini yako?
Shahidi wa kificho P2: Mkristu.
Shahidi wa kificho P2 amefika na anajibu hivyo.
Jaji: Haya tuendelee. Muapisheni.
Anasimama Renatus Mkude anasema huyu Shahidi ataongozwa na Wakili Ignas Mwinuka.
Anasimama Ignas kuendelea.
Ignas Wakili wa Serikali: Shahidi nitakuuliza maswali na hutakiwi kutoa utambulisho wako.
Unaitwa nani?
Shahidi wa kificho P2: Mimi naitwa P2 mkazi wa matalawe, Songea Ruvuma.
Wakili: Kazi gani unafanya?
Shahidi wa kificho P2: Mimi ni fundi umeme.
Wakili: Wewe ni mfuasi wa Chama gani?
Shahidi wa kificho P2: mimi ni mfuasi wa Chadema toka 2021.
Wakili Ignas: unajishughulishaje ukiwa mfuasi wa Chama hicho?
Shahidi wa kificho P2: Huwa najishughulisha na mikutano na kulipa michango.
Wakili: tukumbushe tar. 04/04/2025 ulikuwa wapi?
Shahidi wa kificho P2: Nilikuwa manispaa ya songea kwenye shughuli zangu, nakumbuka nikiwa napitia mitandao ya kijamii nilikutana na ujumbe wa Antipass Tundu Lissu akiwa katika mkutano na wanahabari.
Wakili: Mtandao gani:
Shahidi wa kificho P2: Youtube nilikuaa naangalia.
Wakili: ukabaini nini?
Shahidi wa kificho P2: Nilikutana na ujumbe wa mwenyekiti wa Chama akisema hakutakuwa na uchaguzi, wanaotaka kugombea wasahau mwaka huu. Alisisitiza namna ya kuzuia uchaguzi ni njia ya kuleta mabadiliko na alihamasisha kila mmoja awe jasiri.
Wakili: ulifanya nini wewe?
Shahidi wa kificho P2: Nilivyopata ujumbe huo nikapata hamasa na kuanza kuwatafuta viongozi walioko songea ili tujue linatekelezeka vipi hilo.
Wakili: Kingine kilichoendelea?
Shahidi wa kificho P2: Nilimtafuta Essau Said Mwenyekiti wa Vijana Songea kwa ufafanuzi zaidi.
Alinielekeza atafanya mawasiliano na viongozi wengine na ilipofika tarehe 07/04/2025 kwahiyo alituambia tutoe michango ya hiari na mimi nilichangia elfu 10 hiyo michango ya hiari inaitwa Tonetone.
Wakili: Mwendelezo wa ziara ya Mwenyekiti wa Chadema Taifa?
Shahidi wa kificho P2: Niliendelea na shughuli zangu nikawa nasubiri tarehe 10/04/2025 ambayo itakuwa ndio siku ya Mkutano na tuliambiwa hivyo sisi.
Tarehe 09/04 nilipata taarifa kuwa amekamatwa Mwenyekiti Lissu na kwa vile siku na taarifa za kutosha.
Wakili: Ikawaje?
Shahidi wa kificho P2: Nilijiandaa tar. 10/04 ile asubuhi ili niende kwenye mkutano na kupata ufafanuzi wa nini kimeendelea hadi Mwenyekiti kukamatwa.
Nilipofika mjini nikakutana na polisi wengi na wakawa wanatuambia hakuna mkutano siku hiyo.
Wakili: Ikawaje?
Shahidi wa kificho P2: Nikaona nielekee ofisi za Chama maana tuliambiwa Makamu Mwenyekiti wa Chama atakuwa anazungumza na wanachama pale Ofisini.
Wakili: Makamu Mwenyekiti anaitwa nani?
Shahidi wa kificho P2: John Heche.
Wakili: Nini kiliendelea?
Shahidi wa kificho P2: Tukiwa pale Ofisi za Chama wakati tunasubiri Mh. Heche azungumze wakaja polisi na mimi nilikamatwa katika tukio hilo na kupelekwa kituo cha Polisi.
Part 178 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 178
Wakili wa Serikali anaendelea kumuongoza Shahidi wa kificho ambae kapewa jina la P2
Wakili: Nini kiliendelea kituoni?
Shahidi wa kificho P2: Niliwekwa mahabusu na baadae nikahojiwa kwa tuhuma za kufanya fujo na uchochezi.
Wakili: Nini kiliendelea?
Shahidi wa kificho P2: Waliniachia kwa Dhamana na nilitakiwa kuwa naripoti kila jumatatu.
Tarehe 14/04 niliripoti na tare21/04 nilipaswa kuripoti tena, I kawa sikukuu nikarudi tarehe 22/04 ambapo nilipofika nikapelekwa Central kuchukuliwa maelezo kwa mara ya pili.
Wakili: Maelezo gani?
Shahidi wa kificho P2: Akaniambia nieleze Mwanzo mwisho hadi nilipokamatwa. Nikamueleza kuwa mimi ni mwanaChama na akayachukua hayo maelezo afande Juma Batazary.
Wakili: Mh. Tundu Lissu umemtaja sana unamfahamuje?
Shahidi wa kificho P2: Nikiwa Songea nimemfahamu Mh. Tundu Lissu anafahamika karibu na kila mtu toka akiwa Bungeni na alikuwa Makamu Mwenyekiti na baadae akawa Mwenyekiti.
Wakili: huo uchaguzi ungezuiwaje? Kwa mujibu wa Lissu.
Shahidi wa kificho P2: Sijui ungezuiwaje lakini yeye alisema kwa uasi, Mwenyekiti wa Chama alikuwa anakuja Ruvuma na tukajua angekuja kutupatia mbinu hizo maana alisema wanaotaka kwenda nae ataenda nao na mimi nilikuwa kwenye kundi hilo.
Jaji: Shahidi unaongea mfululizo, hatujui unaelekea wapi wala unaongea nini? Sasa Wakili muongozeni shahidi tujue ameanzia wapi na anaelekea wapi?
Wakili: Ulikuwa unajua uchaguzi utazuiwaje?
Shahidi wa kificho P2: Nilikuwa sijui. 😂
Wakili: Kwa shahidi huyu ni hayo tu Mheshimiwa Jaji.
Jaji Ndunguru: Wakili unasema nini nini sikuelewi.
Wakili Ignas: Mh. Jaji nimesema ni hayo kwa shahidi huyu.
Jaji Ndunguru ohoo kumbe mmemaliza. Haya sawa.
Watu wanacheka sana 😂😂😂
Jaji: Naombeni utulivu tafadhali.
Majaji wanaandika kidogo na wanasema maswali ya Dodoso tafadhali Mshitakiwa. Anasimana Lissu.
Mhe.Lissu: Shahidi unanisikia sawasawa?
Shahidi wa kificho P2: Sikusikiii.
Jaji: humsikii kweli?
Shahidi wa kificho P2: Namsikia Jaji.
Mhe.Lissu: Habari ya Matarawe?
Shahidi wa kificho P2: Nzuri tu.
Mhe. Lissu: Uliandika maelezo Polis?
Shahidi wa kificho P2: Ndio
Mhe.Lissu: Ndio haya tar. 24/04?
Shahidi wa kificho P2: Ndio nilisaini pia.
Mhe. Lissu. Mh. Jaji naomba shahidi aonyeshwe maelezo yake ya Polisi hayo ya tarehe 24/04.
Hayo maelezo ni ya kwako?
Shahidi wa kificho P2: Ni maelezo yangu ndio.
Mhe. Lissu: Uzuri umesema mwenyewe kuwa ni mfuasi wangu sasa nikikuuliza jibu haraka ndio au hapana ili tuendelee. Sawa Bwana mkubwa?
Shahidi wa kificho P2: sawa
Mhe. Lissu: Naomba nimsomeee maelezo yake haya.
Anaanza kumsomea hapa.
Anamsomea maelezo yake hapa anasema mimi ni mwanaChama wa Chadema sina kadi lakini pia nilikuwa mfuasi wa Mh. Lissu hata kipindi anagombea uwenyekiti wa Chama, hapa songea niko chini ya kiongozi wa Vijana Essau.
Nimeshiriki pia kuchangisha pesa za Tonetone nikishirikiana na kiongozi wa vijana na pia mimi nimechangia Elfu 10 kutokana na hali yangu ya kiuchumi. Ziara hiyo atakuwepo Gobless Lema, Makamu Mwenyekiti, Twaha Mwaipaya.
Baadae nilipata taarifa Mh. Lissu amekamatwa na nilipomuuliza Essau Chiza nikaambiwa taarifa Rasmi nitapewa kwenye mkutano, nilipofika ofisini niliwakuta viongozi na baadae nikakamatwa.
Leo nimekuja kuripoti nikaletwa kwako na wewe unasema unataka kunihoji.
Amemaliza kumsomea maelezo yake.
Mhe. Lissu: Niliyosoma ndio maelezo yako?
Shahidi wa kificho P2: Yes ni yenyewe na yako sahihi.
Mhe. Lissu: nakuonyesha maeneo ya kukukanusha: yafuatayo:
1. Tarehe 04/04/2025 uliona mkutano wa Lissu na waandishi wa Habari.
2. Video ya mkutano inasema Mwenyekiti alisema hakutakuwa na Uchaguzi na wanaotaka kugombea wasahau.
3. Uliposema unamfahamuje Mh. Lissu.
Anamsomea maeneo kadhaaa hapa. Ambayo atamuuliza maswali.
Mhe. Lissu: Je ungependa maelezo yako yawasilishwe Mahakamani kama ushahiidi?
Shahidi wa kificho P2: Yawasilishwe tu
Part 179 itaendea kwny post inayofuata,
Naomba repost yako
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 180
Mhe. Lissu anaendelea na maswali ya Dodoso
Mhe. Lissu: Ulivyoandika maelezo ya Tarehe 22/04 waeleze majaji kama umewahi kuwasiliana na polisi juu ya jambo lolote kuhusiana na kesi hii.
Shahidi wa kificho P2: Waliponiletea wito wa kuja kutoa ushahidi huu tar. 11
Mhe. Lissu: Ni mwaka huu?
Shahidi wa kificho P2: Ndio.
Mhe. Lissu: Kuna mahali kokote umeandika. Maelezo katika kipindi hicho ulipomaliza kutoa maelezo tar. 22/04 hadi leo
Shahidi wa kificho P2: Sijaandika.
Mhe. Lissu: Kuna kiongozi yeyote wa Chadema amkutishia kukuua?
Shahidi wa kificho P2: Hapana.
Mhe. Lissu: Kuna mwanachama je aliyekutishia?
Shahidi wa kificho P2: Hapana.
Mhe. Lissu: Kuna mtu yeyote aliyekutishia chochote?
Shahidi wa kificho P2: Viko vya mitandao ya Kijamii.
Mhe. Lissu: nani aliyetoa?
Shahidi wa kificho P2: Siwafahamu.
Mhe. Lissu: kuna mfuasi, mwanachama au shabiki wa Lissu amekutishia?
Shahidi wa kificho P2: Hapana.
Mhe. Lissu: Angalia D6 mambo yanayohusu 07/04 majira ya saa saba kama ulikuwa na mwandishi yeyote wa habari wa Jambo Tv ?
Shahidi wa kificho P2: Sikuwa naye.
Mhe. Lissu: Je siku hiyo mlienda na askari wa upepelezi mkakutana na Andrew Churu kule Dodoma?
Shahidi wa kificho P2: Sio kweli.
Mhe. Lissu: Yupo askari anaitwa Andrew Churu anasema wewe P2 na P mlienda Dodoma kuonana nae.
Shahidi wa kificho P2: Sio kweli.
Mhe. Lissu: Ulishuhudia hayo makabidhiano.
Shahidi wa kificho P2: sikushuhudia.
Mhe. Lissu: Polisi wanasema ulikuwa Dodoma, Wewe unasemaje?
Shahidi wa kificho P2: waongo mimi sikuwepo.
Watu wanacheka. 😂😂
Huyu kweli ni P2, jina lake ni kama vile vidonge ambavyo wadada tunatumiaga kuzuia mimba for emergency ila yeye katoa ushaidi wa kuzuia Mhe. Lissu asiende jela kunyongwa maana hana hatia.😂
Mhe. Lissu: Kwenye hotuba yangu nilisema watu wakafanye fujo?
Shahidi wa kificho P2: Hukusema.
Mhe. Lissu: Hivi kusema tutazuia uchaguzi ni kosa la jinai kwa mujibu wa sheria za nchi hii?
Shahidi wa kificho P2: Sifahamu sheria.
Mhe. Lissu: Uliamini maneno niliyosema. Umesema hapa mahakamani sasa je ni kosa kuamini maneno ya mwanasheria nguli?
Shahidi wa kificho P2: Sijui.
Mhe. Lissu: Sina maswali zaidi Mh. Jaji.
Jaji Ndunguru: Kuna Re Examination.
Wakili wa Serikali Ignas: Hatuna Re Examination.
Majaji wanaandika kidogo hapa.
Wanasema sasa tuendeleee.
Shahidi wewe umemaliza kutoa ushahidi unaweza kwenda.
Renatus Mkude anasimama anasema tuko tayari kuendelea na P8.
Jina la shahidi ni shahidi ni P8 lakini ni Shahidi wa nane wa Jamhuri (PW 😎.
Jaji Ndunguru: Sasa muiteni huyo shahidi ili tuweze kuendelea.
Anaingia Shahidi.
Umri wako shahidi.
Anajibu ni miaka 26.
Mimi ni Mkristu.
Jaji: Utaapishwa hapo kabla hujaanza kutoa ushahidi.
Renatus Mkude: Anasimama anasema Mh. Jaji shahidi ataongozwa na Nasoro Katuga.
Katuga: Unaishi wapi?
Shahidi wa kificho P8: Moshi Kilimanjaro, njoro ya Pepsi.
Katuga: Unajishughulisha na nini?
Shahidi wa kificho P8: Mfanyabiashara wa matunda soko la Manyema lililoko Mbuyuni.
Katuga: Je unajishughulisha na siasa na kivipi?
Shahidi wa kificho P8: Najishughulisha nayo ingawa sio kiundani sana.
Katuga: Kupitia Chama gani?
Shahidi wa kificho P8: Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Katuga: Pale Chadema wewe ni nani?
Shahidi wa kificho P8: Mimi ni mwana Chama.
Katuga: Unamfahamu Tundu Lissu?
Shahidi wa kificho P8: Namfahamu kama Mwenyekiti wa Chama.
Katuga: shughuli zako katika Chama ni zipi?
Shahidi wa kificho P8: Hizo ni shughuli zangu binafsi siwezi kuzielezea.
Katuga: Tarehe 04/04/2025 unakumbuka nini?
Shahidi wa kificho P8: Nilikuwa kwenye biashara zangu soko la Manyema Mbuyuni.
Shahidi anaongea ni kama anakula konyagi halafu hajala msosi wa maana.
Part 181 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 181
Wakili wa Serikali anaemdelea kumuongoza Shahidi wa kificho P8
Shahidi wa kificho P8: Nikiwa katika shughuli zangu nilimuona Mh. Lissu Youtube na Faceebook.
Katuga: Shahidi ongea vizuri tukusikie.
Katuga: Uliingiaje huko mitandaoni.
Shahidi wa kificho P8: niliingia kupitia simu janja na akaunti yangu ndio nilitumia.
Katuga: simu gani?
Shahidi wa kificho P8: Oppo F1S
Katuga: Uliwezaje kuingia Youtube na nini kilikuwezesha?
Shahidi wa kificho P8: Nilitumia akaunti yangu na nilikuwa na bando.
Katuga: uliingia kwenye channel gani huko youtube?
Shahidi wa kificho P8: Jambo TV
Katuga: Uliona nini?
Shahidi wa kificho P8: Niliona tamko la mshitakiwa Tundu Lissu akisema juu ya uasi dhidi ya serikali na kukinukisha.
Katuga: Kutokana na nini?
Shahidi wa kificho P8: Tutaenda kukinukisha, alisema tutakinukisha kama serikali haitafanya mabadiliko.
Katuga: Uchaguzi gani huo?
Shahidi wa kificho P8: uchaguzi wa 2025 ule wa Oktoba.
Katuga: Unahusu nini?
Shahidi wa kificho P8: Nahisi ni Rais.
Katuga: Nini kiliendelea kuhusu wewe?
Shahidi wa kificho P8: Nilipata hamasa kutokana na kauli ya No Reforms, No Election.
Katuga: Shahidi sasa
Shahidi wa kificho P8: Nakusikiliza.
Jaji: unamuuliza leading questions sana. Jielekeze vizuri.
Shahidi wa kificho P8: Mimi nilipata hamasa ya kuhamasisha vijana wenzangu wanaotuunga mkono.
Katuga: vitu gani vilikupa hamasa?
Shahidi wa kificho P8: Nilihamasika uchaguzi wa serikali za mtaa mwaka jana.
Watu wanacheka. Shahidi yuko kama Harmorapa haeleweki kabisa. 😂
Katuga: Unasema ulishawishika na kauli ya Mzee Mwenyewe, huyo Mzee Mwenyewe ni nani?
Shahidi wa kificho P8: Mshitakiwa Tundu Lissu.
Katuga: Ulifanyaje?
Shahidi wa kificho P8: Kuwaonesha video vijana wenzangu wa mtaani. Nikawa nawahamasisha.
Katuga: Kuwahamasisha nini?
Shahidi wa kificho P8: Kwamba tukakinukisha na tukafanye uasi.
Katuga: Tarehe 08/04 unakumbuka nini?
Shahidi wa kificho P8: Nikiwa maeneo ya Njolo ya Pepsi nikihanasisha Vijana kuhusiana na No Reforms, No Election.
Katuga: Nini kilitokea?
Shahidi wa kificho P8: Nilishangaa nimekamatwa tu na vijana wenzangu wamekimbia, nilikamatwa na Askari.
Katuga: Ikawaje Ulipokamatwa.
Shahidi wa kificho P8: Nilipelekwa Ofisi ya RCO pale Moshi Kilimanjaro. Nikakabishishwa kwa afande Rashidi kwa ajili ya kuchukua maelezo yangu.
Katuga: Sababu za kukamatwa kwako uliambiwa?
Shahidi wa kificho P8: Niliambiwa
Katuga: Kwahiyo ulimwambia Rashid kitu gani?
Shahidi wa kificho P8: Kwamba nilikuwa nafanya uasi dhidi ya Serikali na nilikuwa namuunga mkono Mwenyekiti wa Chama cha Chadema.
Katuga: Nini kiliendelea?
Shahidi wa kificho P8: Nilipelekwa mahabusu na kuachiwa kwa dhamana, nikajidhamini mwenyewe. Nilipewa masharti kila mwanzo wa week siku ya jumatatu niwe naripoti.
Katuga: Nini kiliendelea?
Shahidi wa kificho P8: Tarehe 22/04 nikafika ofisi ya RCO na baadae nikafuatwa na afande mwingine na kupelekwa kwa fande Michael akanichukua maelezo kuhusu hiki nilichotoka kuongea kutoka awali.
Katuga: Waheshimiwa ni hayo kutoka kwa shahidi huyu..
Jaji Ndunguru: Karibu kwa maswali ya Dodoso Mshitakiwa.
Mhe. Lissu: Sasa Shahidi najua uliandika maelezo na unayajua maelezo yako.
Shahidi wa kificho P8: Hilo ni jukumu la mawakili mimi sijui.
Mhe. Lissu: Sasa kaka unabishana na Mwenyekiti wako?
Shahidi wa kificho P8: Sasa hivi wewe ni mshitakiwa.
Mhe. Lissu: Sasa kwa vile na mimi ni mshitakiwa na wewe ni shahidi jibu swali langu.
Shahidi wa kificho P8: Mawakili ndio wataamua.
Anasimama Katuga anasema shahidi jibu swali.
Shahidi wa kificho P8: Nitaweza kuyatambua mimi si ndio nilioyatoa.
Mhe. Lissu: Kama wamekwambia napiga watu wanakudanganya. Mimi nauliza maswali.
Shahidi wa kificho P8: Nayatambua mimi ndio nilioyatoa.
Part 182 itaendelea kwny post inayofuata,
Naomba repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 179
Mhe. Lissu anaendelea na maswali ya dodoso
Jaji Ndunguru: Vipi Jamhuri?
Renatus Mkude: Hatuna pingamizi.
Jaji Ndunguru: Hiyo itakuwa ni D6.
Mhe. Lissu: Waheshimiwa Majaji naomba shahidi apewe D6.
Mhe. Lissu: Shahidi umesema kwamba Tarehe 22/04 ulipelekwa Central Polisi Songea kwenda kuchukuliwa maelezo haya?
Shahidi wa kificho P2: Ni kweli.
Mhe. Lissu: Sasa angalia hayo maelezo yako na uwaeleze majaji kuwa umesema chochote kuhusu hiyo tarehe?
Mhe. Lissu: Shahidi kuna mahali kokote?
Shahidi wa kificho P2: sijazungumzia chochote isipokuwa saini.
Mhe. Lissu: Kwahiyo hayapo?
Shahidi wa kificho P2: yapo.
Mhe. Lissu: Kuna tarehe 22/04 kokote.
Shahidi wa kificho P2: Haipo hiyo.
Mhe. Lissu: Kuna mahali umetaja Central Polisi Station Songea? Kituo Kikuu cha Polisi.
Shahidi wa kificho P2: sijakitaja.
Mhe. Lissu: Ulisema unamfahamu Lissu kwasababu ni mwanasiasa maarufu na anafahamika na kila mtu. Si ni kweli?
Shahidi wa kificho P2: Ni kweli
Mhe. Lissu: Uliyasema Polisi hayo?
Shahidi wa kificho P2: sijayasema.
Mhe. Lissu: Tar. 04/04/2025 hayo maelezo kuwa uliangalia youtube yapo?
Shahidi wa kificho P2: yapo
Mhe. Lissu: Wafuasi wangu huwa wana akili sasa unaanza kunitia wasiwasi yapo hayapo?
Shahidi wa kificho P2: Hayapo kiukweli.
Mhe. Lissu: wafuasi wa Chadema wana alama usoni?
Shahidi wa kificho P2: Sijui
Mhe. Lissu: Una kadi?
Shahidi wa kificho P2: Sina.
Mhe. Lissu: Majaji watajuaje?
Shahidi wa kificho P2: Sijui
Mhe. Lissu: Tutajuaje wewe kama sio Chawa wa Mama?
Shahidi wa kificho P2: Sijui
Watu wanacheka.😂😂😂
Mhe. Lissu: unajua utaratibu wa kulipia michango ya Chama.
Shahidi wa kificho P2: Sijui.
Mhe. Lissu. Ulimlipa nani hiyo hela?
Shahidi wa kificho P2: Mwamba wa Kigoma Essau Chiza.
Mhe. Lissu: Ushahidi wowote umeleta?
Shahidi wa kificho P2: Hapana.
Mhe. Lissu: Umesema kuhusu video. Je umewaonyesha hiyo video?
Shahidi wa kificho P2: Hapana.
Mhe. Lissu: Umewasilisha hiyo video kama kielelezo.
Shahidi wa kificho P2: Sijui
Mhe. Lissu: Ulisema ulikamatiwa eneo la Ofisi za Chama Mfaranyaki Songea?
Shahidi wa kificho P2: Kweli
Mhe. Lissu: Ulienda Mfaranyaki kupata ufafanuzi?
Shahidi wa kificho P2: Ni kweli
Mhe. Lissu: Sasa kwenda kutafuta ufafanuzi wa kwanini Mwenyekiti amekamatwa ni kosa?
Shahidi wa kificho P2: Sijui sheria.
Mhe. Lissu: Hata kwa akili ya Kujiongeza tu. Ni kosa hilo?
Shahidi wa kificho P2: Sijui
Mhe. Lissu: Wewe huwa unamfuatilia Lissu kwenye nini kama hujui vitu namna hii maana nimekwambia wafuasi wangu wana akili.
Shahidi wa kificho P2: Sifahamu.
Mhe. Lissu: Mkutano huo wa tarehe 10 unajua ulikuwa umetolewa taarifa Polisi?
Shahidi wa kificho P2: Sifahamu.
Mhe. Lissu: Ulihojiwa kwa tuhuma za uchochezi?
Shahidi wa kificho P2: Ndio.
Mhe. Lissu: wewe ulienda kufanya uchochezi ofisi za Chama?
Shahidi wa kificho P2: Ndio
Mhe. Lissu: kwahiyo ulikamatwa ukiwa hujafanya kosa lolote?
Shahidi wa kificho P2: Sijui.
Watu wanacheka.😂😂😂
Mhe. Lissu: Kwahiyo ulisema ulichukuliwa maelezo ya Uchochezi?
Shahidi wa kificho P2: Ndio.
Mhe. Lissu: Yako wapi hayo maelezo?
Shahidi wa kificho P2: Sijui.
Mhe. Lissu: Je ulifunguliwa kesi ya Uchochezi au kesi yoyote?
Shahidi wa kificho P2: Sikufunguliwa kesi yangu iliishia tarehe 22/04
Mhe. Lissu: Mkutano wangu wa Tarehe
03/04 wewe ulikuwa kwenye huo mkutano wangu?
Shahidi wa kificho P2: Sikuwepo.
Mhe. Lissu: Umekuja kufanya nini sasa?
Shahidi wa kificho P2: Kusema nilichoona tu.
Part 180 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 174
Anaendelea Mhe. Lissu
Mhe. Lissu: Mhe. Jaji hawako serious hawa kwanza ukisoma D4 kila kitu chake kipo hata jina lake hawajaficha lipo na taarifa zake zote zipo, hawajielewi hawa.
Katuga: Anasimama anasema Mh. Sisi ni maafisa wa mahakama aonywe mshitakiwa kwanini anasema hatuko serious.
Mhe. Lissu: Mh. Jaji ni kweli hayupo serious ila nataka niliondoe neno hilo lakini kama anasema nionywe siko tayari kuonywa naomba nifanye submission ya kuonesha ni kwa namna gani hawako serious?
Jaji Ndunguru: Basi Mshitakiwa tuishie hapo kama umesema umeliondoa.
Watu wanacheka sana. 😂😂😂
Mhe. Lissu: je umesema kokote kuwa uliwahi kutishiwa maisha?
Shahidi wa kificho P6: Sijawahi kutishiwa maisha mimi.
Mhe. Lissu: Kuna mwanachadema au kiongozi amewahi kukutishia kukupiga au kukudhuru kwa wewe kwenda kutoa maelezo haya Polisi?
Shahidi wa kificho P6: Hayupo kabisa.
Mhe. Lissu: Je kuna ndugu yako ametishiwa pia?
Shahidi wa kificho P6: Hayupo hata mmoja.
Mhe. Lissu: Waheshimiwa Majaji sina swali lingine kwa shahidi huyu.
Majaji wanaandika kidogo pale mbele.
Kwa sasa ni saa 7 na dakika 15 mchana, huu ni huwa ni muda wa kwenda Break, ngoja tusubiri Kitakachoendelea muda mfupi ujao.
Jaji: Re Examination Jamhuri?
Wakili Cathbert: Hatuna swali lolote Waheshimiwa Majaji.
Jaji Ndunguru Kiogozi wa Jopo la Majaji watatu anateta tena ma wenzake kabla hajasema nini kiendelee.
Anawasha kipaza sauti.
Shahidi umemaliza sasa unaweza kwenda.
Renatus Mkude tunaomba ahirisho tukawaandae mashahidi, lisaa limoja.
Mhe. Lissu: Sawa sina pingamizi.
Jaji Ndunguru: Basi tukutane baada ya lisaa limoja.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 152
Anaendelea Mhe. Lissu.
Tuna haki yakutembelewa, waheshimiwa Majaji kuna masharti kwenye hiyo kanuni ikiwemo sharti la kutembelewa na mfungwa mwenzako, sharti lingine ni askari magereza wakuone na kukusikiliza ila kwa Mawakili kanuni haisemi hivyo.
Waheshimiwa Majaji tangu tarehe 10/04/2025 mpaka 12/11/2025 nilikuwa natembelewa bila tatizo.
Na ndugu, familia, marafiki na Mimi ni Mwenyekiti wa Chadema Taifa, walikuwa wananitembelea wana Chadema
Tanzania nzima.
Niliitwa kwa Bwana Jela nikaambiwa ni marufu kwa viongozi na wanaChadema kukutembelea Gerezani.
Chadema ni Chama halali na sio kosa kwa wanaChadema na viongozi wenzangu kunitembelea lakini kuanzia Tar. 12/11/2025 hawajaruhusiwa.
Maafisa magereza ni maafisa wa umma so yale magereza sio mali zao binafsi.
Hawana mamlaka ya kubagua nani aje gerezani nani asije. Katiba inasema usibague watu kwa mtizamo wao wa kisiasa, dini au kabila na hili vilevile naomba niwaeleze mlifahamu kuhusu violation ya haki ya Mfungwa kutembelewa.
Waheshimiwa Majaji sasa naomba swala la tatu niliseme.
Linahusu uendeshaji wa kesi hii. Na naomba niweke wazi kuwa siwalaumu kwa chochote nitakachosema hapa. Na hiki nitakachosema siwalaumu mawakili wa serikali na nyie majaji.
Haki zangu zimekiukwa sio kwa kosa lenu wala la Mawakili wa Serikali.
Waheshimiwa Majaji leo hii ni siku ya 307 tangu niwekwe mahabusu.
Miezi 10 week 44 niko mahabusu. Waheshimiwa majaji katika siku zote hizi kesi hii imesikilizwa kwa siku 14 tu na leo ni siku ya 15 kesi hii inasikilizwa katika siku 307.
Kuna siku 88 ambazo kesi haijasikilizwa kabisa, niko gerezani hakuna kinachoendelea.
Haki iliyocheleweshwa ni haki iliyokiukwa. Justice delayed is justice denied.
Na Katiba yetu inaelekeza Mahakama ziendeshe mashauri kwa namna ambayo haitachelewesha Haki. Ibara ya 147 ya Katiba inasema.
Kifungu cha 5 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai kinasema mashauri yanaendeshwe kwa haraka.
Tatizo lipo kwenye utaratibu wa session ndio tatizo na hilo ni tatizo la wanaoamua kesi iendeshe kwa njia ya session.
Naomba niwasomee kilichosemwa na Tume ya Haki jinai kuhusu kuendesha mashauri ya jinai kwenye ripoti ya July 2023, ukurasa wa 17 na 18 unasema kuhusu vikao vya mahakama kuu (high court session) tume inasema uendeshaji wa mashauri kwa njia ya vikao huchelewesha mashauri hayo.
Kati ya mashauri 2000 ni mashauri 700 tu ndio yalisikilizwa pekee kwa mtindo wa session.
Hivyo basi uendeshaji wa kesi kwa kutumia session unaamuriwa na Jaji Mkuu zikiisha siku tunasubiri aseme tena ndo maana zimepita siku 88 bila kesi hii kuendelea hadi atakapopanga tena huyo Jaji Mkuu.
Ucheleweshaji huu sio kosa lenu wala mawakili wa Serikali ni kosa la utaratibu tulionao.
Je huu utaratibu wa session uko wapi kwenye CPA ambayo ni sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai.
Leo hapa High Court Dar es salaam kuna majaji wakutosha lakini ili kesi yangu isikilizwe lazima Jaji atoke Songea, mwingine Mtwara sijui na lazima walipwe, Usafiri, Chakula na kila kitu.
Usipowalipa kesi haiendelei na mimi mtuhumiwa nateseka huko jela. Walishindwa nini kuwapangia majaji wa hapa ili kesi isikilizwe kila siku.
Zamani majaji walikuwa wachache sana lakini siku hizi kila mkoa kuna majaji. Nashangaaa mambo haya kwa utaratibu huu sasa.
Jaji anasema soma kifungu cha 185 na anakisoma hapa kinasema Mahakama inamamlaka ya ku conduct seatings.
Mhe. Lissu anasema kuna tofauti kati ya seatings na sessions.
Kwahiyo kwenye hili ni tofauti na ku conduct seatings. Mahakama kuu zote zinakaa kusikiliza kesi hizo ni seatings zote.
Mimi nasema utaratibu wa sessions ni mbaya zaidi kwa kesi kama ya Uhaini.
Jaji ameleta kifungu namna Lissu alivyolitafsiri ameishia kusema hebu tuendeleee basi mshitakiwa 😂😂😂
Kosa la Uhaini ni Sue Generis sio sawa na wizi wa kuku, ujambazi na makosa mengine.
Part 153 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.