#TajiriLaKihaya
KUNA MASWALI MAKUBWA YANAYOPASWA KUJIBIWA MUHIMBILI NA JKCI.
Leo familia yetu imepoteza mdogo wetu. Moyo wangu umejaa huzuni, uchungu na maswali mengi ambayo hadi sasa hayajajibiwa.
Siku ya kwanza nilipofanikiwa kumpeleka mdogo wangu JKCI na kupata chumba cha VIP, nilifurahi sana. Niliona kama tumepata mwanga wa matumaini. Baada ya vipimo, tuliambiwa tatizo lake la moyo lilihitaji upasuaji mdogo tu na angeweza kuendelea na maisha yake kawaida.
Tukaahidiwa upasuaji ungefanyika ndani ya siku mbili au tatu.
Lakini siku zikageuka wiki.
Kabla hata ya kulazwa, tulikuwa tumepambana kwa zaidi ya mwezi mzima tukizungushwa kutoka leo hadi kesho. Mara daktari hayupo, mara jopo la wataalamu halijakaa, mara kipimo kirudiwe, mara tusubiri dawa zifanye kazi kwanza. Kila siku ilikuwa ni ahadi mpya na tarehe mpya.
Baada ya kulazwa tuliamini safari ngumu imekwisha. Lakini ndipo mateso makubwa zaidi yalipoanza.
Mdogo wangu aliingia hospitalini akiwa bado anaweza kutembea, kuongea, kula na kujitambua. Kila siku tulisubiri upasuaji ulioahidiwa, lakini haukufanyika. Badala yake hali yake ilianza kuzorota mbele ya macho yetu.
Wiki moja ikapita.
Wiki mbili zikapita hadi wiki tatu
Hakukuwa na upasuaji.
Kulikuwa na sababu mpya kila siku.
Kisha tukahamishwa kutoka chumba tulichokuwa tumepewa kwa madai kuwa kingefanyiwa fumigation. Lakini usiku huo huo mgonjwa mwingine akawekwa kwenye chumba hicho. Hadi leo hatujui ukweli ulikuwa nini- lazima UFISADI ULITUMIKA HAPA!
Tulihamishiwa chumba kingine JAPO kilikua VIP… ila hakikua kwenye standard sawa!
Hata nakumbuka kuna Daktari wa Kihindi alikuja kusoma vipimo akasema ile MONITOR haipo sawa! Mapigo ya moyo na oxygen haisomeki kwa usahihi…
Sasa kwa nn tulihamishwa chumba? Kutoka chumba kizuri kuja hiki?? Kwa nn kile tulichokuwepo alipewa mwingine usiku huo tumehamishwa? CORRUPTION!
Baada ya hapo hali ya mdogo wangu ilizidi kuwa mbaya zaidi. Akapoteza nguvu, akashindwa kuzungumza, akashindwa hata kuwatambua watu waliomzunguka.
Tulikuwa tunauliza maswali. Tulikuwa tunaomba msaada. Tulikuwa tunaomba hatua zichukuliwe haraka.
Lakini muda uliendelea kwenda.
Leo asubuhi mdogo wangu amefariki dunia.
Siandiki haya kwa hasira pekee. Naandika kwa maumivu ya familia iliyokuwa na matumaini makubwa ya kumuona mpendwa wao akirudi nyumbani akiwa mzima.
Kama kweli kulikuwa na uzembe, kucheleweshwa kwa huduma, ukosefu wa uwajibikaji au mifumo mibovu ya utoaji huduma, basi kuna haja ya uchunguzi wa kina na hatua kuchukuliwa. Maisha ya Watanzania yana thamani. Wagonjwa hawapaswi kupoteza maisha wakisubiri tarehe nyingine, kikao kingine au ahadi nyingine.
Tunataka majibu.
Tunataka uwajibikaji.
Na zaidi ya yote, tunataka familia nyingine isipitie maumivu tuliyoyapitia sisi.
Kama hapa ni VIP… je wagonjwa wa kawaida wanapata huduma gani???
Pumzika kwa amani mdogo wangu. Tulipambana kwa kila tulichoweza. Mungu akupokee katika makao ya milele. 💔🕊️
As the civil war in Sudan enters its 4th year, the RSF continues to commit genocide with impunity.
As I told this Trump official — if ending this genocide is a priority we need ACTION. To get results, the US must use our immense leverage to get the UAE to stop arming the RSF.
“They tried to bury us, they didn’t know we were seeds.”— Poet Dinos Christianopoulos
@AAgather and I survived the most gruesome, vilest forms of human torture. But here we are smiling, healing, and continuing to fight for a better world. We shall die on our feet, fighting!
“There must be an independent, transparent and inclusive investigation of these events to ensure accountability and that the fundamental freedoms and constitutional rights of all Tanzanians are protected.” - UK's Human Rights Ambassador, @ESandersFCDO
https://t.co/B3MY6toKOB
ALERT: Samia amepokea wito kutoka mahakama ya kimataifa ICC inayomtaka kuudhuria kesi yeye binafsi. Ametakwa afike kwa hiari kujibu shutuma dhidi yake zinazohusiana na mauaji ya alaiki. Akikataa, mahakama itatoa amri ya kumkamata. Wito ulipokelewa zaidi ya wiki moja iliyopita
Wewe ni rais. Unakerwa na mtoto wa miaka 20, Shadrack Chaula, aliyechora picha inayofanana na sura yako akaichoma. Unaagiza atekwe, ateswe, auwawe.
What kind of a dubious human are you?
Enough is enough!!