@ayubu_madenge Wenzetu wenye asili ya Asia na Ulaya, wana Utamaduni ambao ni mgumu kwa familia nyingi zenye asili ya Kiafrika. Mzazi mwenye asili ya Afrika yuko radhi mali zake wazijua marafiki zake kuliko watoto na mke wake.
@DevotaMinja@ChaummaT Ulishindwa kuupata ukiwa CDM, utaupata ukiwa Chaumma??? Hebu acha vichekesho basi. Wewe hujaona hata mkutano wako wa pale Stand ya zamani ulikua kama unajiongelesha mwenyewe? No body cared about what was happening!
@Jambotv_@ChaummaT Huyu Kule CDM alikua ana tembelea Mbeleko za Kaka yake FAM, huko Chaumma anajifurahisha tu kuchagamsha genge. Hata kura 1000 tu hawezi kupata.
@ayubu_madenge Wanafunzi wa vyuo vikuu jamii ya kina Kiliba una tegemea nini?? Hapo zamani chuo kikuu palikua sio pa kwenda kila aliye hitimu masomo ya Sekondari, vilienda vichwa vyenye akili inayo fikiri barabara.
Ndugu @CRDBBankPlc hizi meseji za “Swahiba!Ni BURE kutuma pesa kutoka CRDB akaunti Kwenda CRDB akaunti na NAFUU sana kuanzia SH. 8 tu kutuma pesa kwenda mitandao ya Simu na Benki zingine.Humu Tu!” Basi zinatosha jamani!
*DKT. JINGU AHIMIZA MATUMIZI YA TEHAMA KATIKA MALEZI*
Na WMJJWM- Mwanza.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. John Jingu amewataka Wataalam wa Sayansi ya Malezi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto kutumia teknolojia katika kutatua changamoto za Malezi na kuboresha Sayansi ya Malezi kwa watoto.
Dkt. Jingu amesema hayo wakati akifungua Kongamano la Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya mtoto linaloendelea katika ukumbi Jijini Mwanza.
Dkt. Jingu amesema kumekuwa na ombwe kati ya kizazi cha zamani na cha sasa katika suala la malezi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto hivyo Wataalam watatumia teknolojia vizuri itasaidia kuondoa ombwe hilo na kutatua changamoto zilizopo katika Malezi nchini.
"Sisi wote tulivyo leo ni kwa sababu ya malezi tuliyopata kutoka kwa wazazi wetu, hivyo ni muhimu na sisi kuendeleza malezi bora kwa watoto ili kuwa na Taifa imara na lenye maadili mema" amesema Dkt Jingu.
Aidha Dkt. Jingu ameongeza kuwa katika wakati huu ambapo Maendeleo ya TEHAMA yamechukua nafasi kubwa katika Jamii Wataalam wa Malezi watumie Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia kuhakikisha Jamii inapata elimu ya malezi kwa watoto.
"Tunaweza kuwa na Majukwaa ya wazazi katika mitandao kujadiliana kuhusu Malezi na changamoto zilizopo katika kuzipatia ufumbuzi hata kuwa na Majukwaa kwa watoto yatakayotoa elimu,burudani na michezo kwao yenye kuzingatia maadili yetu" amesisitiza Dkt. Jingu
Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Baladya Elikana amesema suala la malezi ni muhimu kuzingatiwa hasa katika kujenga taifa lenye watu wenye maadili na uzalendo kwa nchi yao.
"Najua lengo la kongamano hili ni kutathmini utekelezaji wa programu mbalimbali za malezi katika jamii na kutoa utatuzi wa changamoto mbalimbali za malezi na makuzi katika jamii hivyo tutumie Kongamano hili kuleta mabadiliko katika suala Malezi kwa watoto wetu." amesema Elikana
Kongamano la melezi ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya familia ambayo huadhimishwa Mei 15 kila Mwaka. Kongamano hilo limewakutanisha Wataalam wa malezi, Maafisa Ustawi wa Jamii, Maafisa Maendeleo ya Jamii na wadau kutoka Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yanayotoa Huduma za malezi kwa watoto pamoja na Watafiti wa malezi kutoka Taasisi za Elimu ikiwemo Chuo Cha Utafiti Ifakara, Chuo cha Ustawi wa Jamii, na Chuo Kikuu cha Dodoma.
MWISHO
@Thommunkondya Mwananchi atoke Kamsamba,Mkonko,Ivuna, Ntungwa,Utambalila kwenda kufuata huduma Chitete?? Lilikuwa wazo la ki binafsi sana. Wananchi wana pata mateso ya gharama kufuata huduma za Kiserikali kule Chitete.
@millardayo 2003-2005 hapo ilikua kama kambi ya JKT. Sema hio shule ni kama kuna kamzimu kakurithishana Undava. Enzi zetu kulikua na waimbisha Kimbembe mashuhuri kama Ghost face Killer, Bad Nyau n.k