Unajiuliza ni mwizi? Hapana! Ana silaha? Hapana! Sasa una jiuliza kwanini itumike nguvu yote ile kwa mtu mmoja ambae anaweza dhibitiwa na watu wawili/watatu bila kutumia silaha?
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 12,
Anaendelea Mhe. Lissu
Hakuna aliyesema kuwa nilichapisha video, nilisambaza video. Hakuna aliyesema hayo. Kuna shahidi alieleza nilivyokamatwa
Nilikamtwa kule Ruvuma kwa kupigwa mabomu na sio nguvu kiasi kama mashahidi mapolisi walivyokuw wanasema kwenye maelezo yao hapa.
Hakuna waliponiambia kosa langu, walinipiga mabomu na watu walipigwa. Nilipelekwa kwa RPC Ruvuma Michael Chirya ule usiku akaniambia unapekekwa Dar es salaam usiku huu huu.
Nilimwambia kuwa anipe simu niongee na ndugu zangu na kuwapigia Mzee Alute na Dada yangu anileteee Chakula. Akaniletea Chakula ni nikatumia simu ya RPC. Nikawekwa Central shimoni na kujua makosa yangu niliambiwa hapa Dar es salaam kuwa makosa yangu ni uhaini.
Kukamatwa kinyume cha sheria na mashitaka ndio haya nimesema.
Hayo maneno yanayodaiwa kuwa nilisema. Sitaki tusumbuane huko mbele ya safari.
Ninachokisema hapa ni kwamba NI KWELI NILISEMA MANENO HAYO.
Sijawahi kukataa maneno yangu ni maneno ambayo nimeyasema kwenye mikutano ya hadhara mkoa wa Mbeya, mkoa wa Iringa, Songwe, Njombe, Rukwa na Mtwara.
Msimamo wangu kuhusu kuzuia uchaguzi haujawahi kuwa yakificho.
Swala je ni uhaini?
Wajibu hilo swali la msingi?
Msihangaike kwasababu sitabishia hao mashahidi wa video hao sina shida nao.
Mashitaka haya ni mashitaka ya kisiasa hilo linapaswa kueleweka kuwa mshitaka haya ni mashitaka ya kisiasa ili tumalize uchaguzi halafu tumuache.
The political nature of this charge is like this.
Historia ya miaka 22 ya makesi ya uongo dhidi yangu ni ushahidi mwingine kuwa makesi haya ni ya uongo.
Tangu nimekamatwa nimetendewaje huo pia ni ushaidi wa kuwa ni mashitaka ya kisiasa.
Nimetendewa mambo ya hovyo tangu siku ya kwanza kama mtu mwenye hatia ninavyokuwa treated ni kama nina hatia ya mauaji.
Nakaa wafungwa waliohukumiwa kunyongwa, nachanganywa na wafungwa wa kifo. Why? Kwanini hilo?
Hata hao waliohukumiwa kifo wanaruhusiwa hata kufanya ibada ya Mungu, nimenyimwa kufanya ibada.
Hadi nilipolalamika hapa ndo wakamleta Father George akaja chumbani kunifanyia ibada na amekuja mara mbili tu.
Wafungwa wenzangu wote ambao hawajahukumiwa kifo wanafanya ibada.
Mimi mfungwa ninaekaa na waliofungwa kifo siruhusiwi kufanya ibada. Kwanini wanafanya hivi sasa?
Wafungwa waliohukumiwa kifo wanalindwa na maaskari wawili 24hrs. Tangu ijumaa kuu nilipokamatwa nalindwa na Bwana Jela wako pembeni wawili. Mahali pekee ambako hawanisindikizi ni chooni.
Why tusiseme hii ni political persecution ni nini kingine?
Hii ni kesi za kubambikiza kwa maneno ya Rais wa Tanzania ni kesi zenye lengo la kuumiza watu hii ni kesi mojawapo ya kubambikiza.
Tarehe 18/05 Rais Samia alifunga mafunzo ya maafisa wa polisi kurasini alisema maneno yafuatayo kuhusu kesi za kubambikiza.
Katuga anasema asimseme Rais Samia haya hayahusiki hapa.
Lissu anasema nina kurasa 140 na leo hii ngoma haiishi.
Hakimu anasema ni wajibu wa ku control hizi proceedings.
Lissu anasema mheshimiwa nina kurasa 140 na sasa ni page 70 kwahiyo wewe vumilia tu nisome.
Wajibu wako wewe ni kuandika na sio kunielekeza nini chakufanya.
Lissu anasema mheshimiwa wenzangu wametumia siku zaidi ya siku 100 kwanini mimi siku moja inakuumiza?
Hakimu anasema hii ni committal Court hayo mengine nenda nayo high court.
LISSU anasema mimi naongea tu wewe ukiona nakuchosha utanisimamisha utasema niache kuongea.
Sasa naendelea.
Sasa Rais anasema niongee na Mapolisi mmekuwa na mlolongo mkubwa wa kubambikiwa kesi. Nanyi Polisi jikagueni kama kuna kesi za aina hii mzifute.
Anayefungua kesi sio mapolisi ni DPP hawa ndio wanapaswa kuzifuta kesi kama hizi.
Hii amri ya kuficha mashahidi ya kutengeneza star chamber Court inatokana na kifungu cha 194 cha CPA.
Part 13 itaendelea Post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 9
Anaendele Mhe. Lissu
Kifungu cha 263(3)(5) kinanipa haki ya kusema na nitakayosema yote uyaandike na uyasome kwangu ni muhimu kwasababu kwa kesi kama hii kubwa kuliko zote Tanzania.
Ambayo adhabu yake ni adhabu ya kifo kwa kesi ya aina hii,
Anasimama Katuga hapa anasema Mhehsimiwa kifungu namna anavyokitafsiri ni tofauti na maana yake. Hapaswi kusema kila kitu, yeye aseme ni kweli au sio kweli?
Tundu Lissu anasema huyu Wakili wa serikali tumemvumilia sana kasema yakwake. Sasa muda huu anisubiri na mimi niseme yakwangu. Anivumilie na awe mtulivu kabisa.
Hakimu anasema ntuhumiwa unapaswa kwenda direct. Lissu anasema hapana siwezi kwenda huko
Kwanza naomba niendelee na nipewe muda.
Jambo la kwanza nataka kusema kuhusu mimi. Masuala ya character ni muhimu sana kwasababu ni maswala relevant to the charge.
Jina langu ni TUNDU ANTIPHAS MUGH'AI LISSU. nimezaliwa Mahambe Ikungi Singida 20/01/1968. Nina miaka 57 ni mtoto wa Saba kati ya watoto 10.
Nilipata elimu ya msingi Mahambe.
Amesimama Katuga anasema mheshimiwa asiende kwa style hiyo asiseme mambo ya amesoma wapi?
Mheshimiwa anasema Lissu asome hati ya mashitaka
Amesoma yote.
Lissu anasema Mhehsimiwa Hakimu unapswa kulinda haki yangu ya kusema. Inakuwaje hawa wameongea yote kuanzia asubuhi hadi sasa hivi wamekaa siku zaidi ya 100 wanaandaaa haya makaratasi. Na wewe ulinde hiyo haki yangu sitakubali kabisa kwenye jambo hilo.
Nimesoma Ilboru, Galanos, nilienda kwa mujibu wa sheria JKT 1989/1990. Baaada ya JKT nilitakiwa kwenda kusoma chuo kikuu 1990 kutokana na mgomo wa wanafunzi kwahiyo nilifanya kazi shule ya sekondari Bondeni arusha.
1991 nilisoma kitivo cha sheria shahada ya kwanza pale UDSM.
Nilimaliza UDSM na kumaliza November 1994 na kuzawadiwa shahada ya sheria ya heshima. Honours degree. Mimi ndie niliyekuwa mwanafunzi bora wa sheria wa mwaka wa 3 pale UDSM.
Nilipograduate nilipata scholarship kwenda kusoma nje kutoka Serikali ya Wingereza, Mwaka 1995 hadi 1996 nilipata distinction na ndoto zangu nilikuwa nataka kurudi UDSM kufundisha sheria ilikuwa ni ndoto yangu siku zote.
Nilipata kazi LEAT ya Dar es salaam mwaka 1998 kama mtafiti wa masuala ya mazingira na haki za binadamu hadi mwaka 1999.
Nilipata kazi world resources institute (Taasisi ya Rasilimali za Dunia)
Nilifanya kazi WRI kwa miaka 3 na 2002 nilirudi Tanzania.
June 2003 nilipata uwakili wa mahakama kuu za Tanzania na chini yake. Nimekuwa Wakili wa nchi hii namba yangu ni 945.
Ni muhimu kuelewa maisha yangu ya ajira kwasababu yana uhusiano na kesi hii maana nimesikia wanasema kuhusu siasa zangu.
Katika maisha yangu yote nimekuwa mwanaharakati wa kisiasa. Na mwanahatakat wa haki za binadamu. Kwenye siasa mimi nilipiga kura kwa mara ya kwanza 1985 nikiwa kidato cha 5.
Kabla sijaenda chuo kikuu nilienda jeshini na majeshi yalikuwa ya CCM. Na mimi nikiwa jeshini nilikataa utaratibu wa majeshi kuwa ni mali ya CCM.
HAKIMU anauliza hiyo ni relevant Lissu anamjibu kuwa hiyo ni Character na ni muhimu sana urekodi.
Nayasema haya ili ujue mimi ni mtu gani yuko mbele yako. Nilianza harakati zangu jeshini sio tu huku mtaani.
Mwaka 1995 nikiwa mwanafunzi wingereza nilirudi nyumbani kuja kugombea ubunge singida kusini miaka ile. Nilikuwa mgombea ubunge kwenye uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi na baadae nilirudi shule.
Naomba kusema kuhusu Chadema, nilijunga Chadema 2004 July na nilipojiunga niliteuliwa kuwa mkurugenzi wa sheria na haki za binadamu. Na kwasababu nilikuwa wakili uchaguzi wa 2005 nilikuwa wakili wa wagombea wote wa Chadema walioshitakiwa kwenye uchaguzi.
Kwahiyo kwenye haya masuala ya Uchaguzi nina historia ndefu sana.
2010 nilichaguliwa kuwa mbunge kwa tiketi ya Chadema. Na nilikuwa mnadhimu mkuu wa kambi ya upinzani.
Part 10, itaendelea post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_SHAURI_LA_UHAINI
Part 1
Mahakama imeamuru kuwa committal itasomwa yote bila kurushwa live.
Wakili wa Serikali Katuga anaendelea kusoma kwa sasa.
Maajabu yaliyotokea ni kwamba mawakili wa serikali waliomba maelezo ya mashahidi wa siri yasirushwe live.
Lakini cha ajbu mahakama imesema maelezo ya mashahidi wote yafichwe na yasiwe live.
Kifupi mahakama imetoa uamuzi ambao hata serikali haijaomba. Imefunga kila kitu na kesi kuzimwa.
Katuga anaendelea, amemkumbusha Mtuhumiwa Shitaka lake na kumkabidhi taarifa ya mashitaka.
Anasema Jamhuri itakuwa na mashaidi 30 na vielelezo vya myaraka 9.
Maelezo yataanza kusomwa na Thawabu Isa wakili wa serikali.
Anasimama na kuanza kusema SSP Kangio, atakuwa shahidi wa kwanza. Ameapa kusema ukweli na maelezo yake ni kama ifuayavyo.
Nimeajiriwa 2003 polisi na mikoa mbalimbali ninefanya. Nimekuwa na vyeo tofauti na sasa ni mrakibu wa polisi kanda ya Dar es salaam. Nafanya majukumu ya kusimamia askari katika majukumu ya kiupelelezi.
04/04/2025 nikiwa ofisi afande Kaaya anayefanya Doria mtandaoni nilimtaka anipe picha mjongeo kuhusu maudhui yakiyokuwa yanatoa taarifa yenye uchochexi.
Maudhui hayo ni mapolisi wanakuja na mabegi ya kura feki kwenye vituo. Jambo ambalo ni uongo. Majukumu yetu ni ulinzi na sio kuiba kura.
Pia maelezo yaliyokuwepo ni kuhusu majaji ni MACCM hivyo wanafanya kazi kwa mujibu wa CCM. Na sio kweli kwamba majaji wanafanya kazi kuwaonea wapinzani. Na hivyo taarifa hii ni uongo na yalilenga kuleta chuki.
Pia alisema kuenguliwa kwa wapinzani ni mkakati wa serikali hivyo zilikuwa ni uongo na kutengeneza chuki dhidi ya Rais.
Na msimamo wetu ni wa uasi. Ni kweli ni msimamo wa uasi kwani tunaenda kukinukisha na huu uchaguzi tunaenda kuuvuruga kwelikweli.
Katika picha mjongeo hiyo mzungumzaji alikuwa ni LISSU. Na aliyokuwa anafanya yalikuwa na nia ya kuitishia serikali ili ayapate yeye na wafuasi wake.
Niliamuru Insp. Kaaya aanze kufanya uchunguzi wa jalada hilo na taarifa hiyo ndio akafungua kesi na kuanza uchunguzi. Na akaanza kujaza PF500
Baada ya kutoa maelekezo kutafuta mjengeo iliyoerekodiwa eneo husika nilitoa taarifa kwa mabosss wangu na kuhusu kile alichosema TUNDU LISSU mtandaoni. Niliripoti kwa afande DCI akasema tuendeleee
Nilimtafuta kiongozi wa JAMBO TV anipe video ile na baadae akasema video anayo P ambae kasafrir. Hivyo nikatoa taarifa kwa maboss kuwa video tutaipata kwa P ambayo yuko Dodoma.
DCP NG'ANZI nilimpa taarifa kuwa tutaipata kwa kijana wa Jambo TV ambae yuko Dodoma.
Haya ni maelezo ya George ambae ni kaimu mkuu wa upepelezi kanda ya Dar es salaam. Yansomwa maelezo yake hapa mahakamani.
Nikaeleza lifunguliwe kosa la uhaini kwasababu aliesema TUNDU lisuu hayo maneno yake, yeye ni Askari ambae ana cheti cha Kujenga taifa kutoka jeshi la JKT hivyo alikuwa na wajibu wa kulinda amani ndani ya Taifa letu. Kusema maneno kama hayo ni kosa kisheria.
Hayo ndio maelezo yangu yote. Yameisha maelezo ya George na anasemaa anayo maelezo ya nyongeza Ya huyo SSP George akasema pia nilikabidhiwa TUNDU LISSU akitokea RUVUMA.
Nilimpokea Lissu na wakati nafanya mahojiano walikuja mawakili wake pia Tulienda kwenye ofisi yenye utulivu na nikamuonya kuwa anatuhumiwa kosa la uhaini. Na kumpa haki zake za msingi.
Huyu George ni msaidizi wa Mafwele. Anasemaa Lissu aligoma kutoa maelezo yoyote.
ASP. John. Ni shaidi wa pili ambae ni mkazi wa Temeke. Amekula kiapo na ushaidi wake ukaanza kuandikwa.
Nimeajiriwa 2005 na nina elimu ya computer na mfanyakazi wa polisi. Nimesoma vyuo ikiwemo Chuo Cha Polisi kurasini.
Nafanya kazi kwa DPP dawati la Doria mtandaoni. Na huwa napeleleza makosa yanayofanywa mitandaoni.
Huyu sasa ni shaidi wa pili baada ya yule wa kwanza ambae ni George.
Part 2 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba Repost yako.
VIDEO:
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Makambako mkoani Njombe Deo Sanga (Jah People) akiomba kura kwa wajumbe wa CCM katika kata ya Kitisi amesema kuwa endapo akipata ridhaa kwa mara nyingine ya kuwa mwakilishi wao Bungeni atahakikisha anafanikisha ujenzi wa bustani kwa ajili ya wananchi kupunguza mawazo akidai kuwa tayari eneo limekwishapatikana.
Akizungumza siku ya Jumamosi katika kata hiyo, Sanga amesema, "Niliwaambia soko tumepata, tumepata tena eneo la kujenga dampo lakini pia na eneo la kujenga bustani kwa ajili ya watu wenye stress kwenda kupumzika huko", amesema Deo Sanga.
Akijibu swali la wajumbe juu ya ujenzi wa kituo kipya na cha kisasa cha mabasi Makambako, Sanga amesema tayari fedha zimepatikana na serikali inatarajia kuanza ujenzi.
Kwa mujibu wa Ripoti ya CAG 2023/24, Ukaguzi wa mafuta yaliyosafirishwa kupitia bomba la TAZAMA (Jan 2023 – Agosti 2024) ulibaini upungufu wa lita milioni
14.46 zenye kodi ya Tsh. Bil 12.6 ambazo hazikufika kituo cha Inyala, Mbeya. Mafuta haya yalibaki nchini bila kulipiwa kodi.
TANROADS ilisaini mkataba wa Sh 38.36B kujenga Barabara za Ibanda–Kajunjumele (22km), Kajunjumele–Kiwira Port (6km) na Kajunjumele–Itungi Port (4km) Songwe. Kazi haijafanyika baada ya mkandarasi kuwasilisha dhamana feki kutoka benki ya Azerbaijan iliyofilisika na haiwezi kulipa.
Kwa nini hatujengi balozi, tunalipia kodi majengo fedha nyingi mno. Balozi 39 kati ya 43 zimetumia Sh 22.63B kulipia kodi ya ofisi na makazi 2023/24, sawa na 14% ya bajeti yao.
Kwa miaka 3 mfululizo, tumeingia gharama ya Sh 56.56B kulipia kodi, sasa si bora tujenge tu balozi?
Hadi Julai 2024, taasisi 278 za umma zilikuwa na madeni yasiyolipwa kwa zaidi ya miezi 12, jumla tril 7.23, sababu kubwa ikiwa ni uhaba wa fedha serikalini na mwenendo mbaya wa biashara katika taasisi husika. Licha ya hayo, kiongozi bado anaahidi ya Tsh. Bil 1 kwa timu ya Taifa.
Tarehe 16 Feb 2022 M/Kiti Lissu alikutana na kuzungumza na Rais Samia huko Ubelgiji, huku Tanzania hapa M/Kiti Mbowe alikuwa jela kwa tuhuma za Ugaidi. Hatukuona matusi.
Juzi FAM amekutana na Rais Samia matusi ni kama tani 9000!. Kwa nini ?