"Huwezi kuwa unasonga mbele kama hawapo unaowaacha nyuma wala hawapo unaowapita mbele yako. Ukigeuka nyuma na usione wanaokukimbiza ujue wewe ndio wa mwisho. Ukitazama mbele usione wa kuwakimbiza ujue mwisho wako umekaribia. Nafasi zote hizi mbili ni hatari kwa ustawi wako."