@Kiganyi_ Zile pesa wanapewa chawa, 50% znaweza itoa hii familia kutoka hapo walipo to somewhere better.
Ikipatikana namna tunaweza support plz share.
Sad.
Museveni: When we discovered oil in Uganda, the major oil companies kept telling us refineries do not make money. But when I checked, a refinery in Uganda is actually very profitable.
Mwekezaji wa ndani anayenufaika na vivutio vya uwekezaji vitolewavyo na Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) amefungua kiwanda cha kuzalisha pikipiki katika Kata ya Mlowo, Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe, chenye uwezo wa kuzalisha pikipiki 10,000 kwa mwaka.
Akizungumza kuhusu mradi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Mbeya Line Company Limited Bw. Burton Mwakibwili amesema kiwanda hicho kilianza uzalishaji mwaka 2022, kikiwa na mtaji wa shilingi milioni 500 na kimeajiri Watanzania 13.
Ameeleza kuwa vipuri vya pikipiki huagizwa kutoka China kwa gharama nafuu na kufanyiwa uunganishwaji kiwandani hapo, hatua inayowezesha kampuni kuzalisha pikipiki zenye bei nafuu zaidi ukilinganisha na kuagiza pikipiki zilizokamilika.
“Tunazalisha pikipiki aina ya T-Better ambazo zimekuwa zikikubalika katika masoko ya mikoa ya Songwe, Mbeya na Rukwa, pamoja na nchi jirani za Zambia na Malawi,” amesema Bw. Mwakibwili.
Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano kwa Umma na Mawasiliano wa TISEZA, Bi. Aderina Rushekya, ametoa wito kwa wakazi wa Songwe na Watanzania kwa ujumla kuchangamkia fursa za uwekezaji zilizopo mkoani humo.
Amesema Mbeya Line Company Limited imenufaika na vivutio vya uwekezaji ikiwemo msamaha wa kodi wa asilimia 75 kwenye ushuru wa forodha pamoja na uwezeshwaji wa kupata vibali vyote muhimu kupitia Kituo cha Uwezeshaji cha Pamoja (One Stop Facilitation Center) cha TISEZA.
Bi. Rushekya amesisitiza kuwa uwekezaji wa ndani ni nguzo muhimu katika kukuza uchumi wa taifa, kuongeza ajira na kuimarisha viwanda vya uzalishaji nchini.