#TANZANIA: MWANACHAUMMA AJISALIMISHA KWA LISSU MAHAKAMANI, "UTATUELEZA VIZURI"
Kesi ya uhaini ya Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu imeahirishwa leo Septemba 11, 2026 hadi Jumatatu ijayo.
Pia, aliyewahi kuwa mwanachama wa chama hicho na baadaye kuhamia chama cha CHAUMMA kisha akatangaza tena kukihama chama hicho na kurejea CHADEMA, ajisalimisha kwa Lissu leo, Lissu amemtaka ajieleze kwanza kilichomuamisha.
Zaidi: https://t.co/yxhrSnWgjM
@HildaNewton21 Maswali yao ni predictive:
1. Kamusi inasema nini kuhusu uasi, kuvuruga, kukinukisha.
2. Matumizi ya mahakama
3. Umeonyesha kwa majaji hizo report. Ataanza Katuga, Mrema atarudia, Ajuaye naye atazunguka humohumo n.k
Tatizo watakutana na mwalimu atawafungulia encyclopedia.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 408.
Makam Mwenyekiti John Heche anaendelea kutoa ushahidi wake.
Mhe. Lissu: Uhusiano wa izo taasisi na Tanzania?
Heche: Uhusiano ni Mzuri na hatuna ugomvi nao kwa mfano Tanzania imekuwa founder member wa OUA tangu mwaka 1963.
EAC pia tumekuwa founder na SADC Tanzania imepigania uhuru wa nchi nyingi za kusini mwa Afrika kwahiyo uhusiano wetu ni mzuri.
EU pia wamekuwa marafiki zetu wa muda mrefu na wamekuwa wakitoa msaada mkubwa wa fedha za maendelea na Balozi zao nyingi ziko hapa na UN pia Tanzania sisi ni Wanachama na uhusiano wetu ni mzuri tu.
Mhe.Lissu: Nimeshtakiwa kwa uhaini na niko ndani zaidi ya mwaka sasa tunaelekea na nusu, kwa ufahamu wako hii kesi ikoje???
Heche: Kwa ufahamu wangu hii ni kesi ya uongo yenye lengo la kukandamiza Demokrasia, kurudisha nyuma harakati za Chama chetu cha CHADEMA kudai mabadiliko.
Hii ni kama kesi zingine nyingi za kisiasa ambazo Wanachama na Viongozi wetu wamekuwa wakifuguliwa ambazo hawawezi kushindana ila Wanatumia mfumo wa Haki jinai na Vyombo vya dola kukandamiza wapinzani wao.
Hii ni kesi ambayo inatumia rasilimali za nchi na malengo yake ni kuumiza Uongozi mzima wa Chama chetu kwasababu Mwenyekiti wetu anayetuongoza ameshikiliwa kwa muda mrefu zaidi Gerezani bila kosa.
Mhe. Lissu: Nimemaliza Waheshimiwa majaji nilisema leo hii ngoma hailali waheshimiwa majaji.
Jaji Ndunguru: Upande wa mashtaka mnasemaje?
Katuga: Tuna maswali mengi sana ya dodoso kutokana na ushahidi uliotolewa na tulijiwekea utaratibu wa kuishia saa kumi na moja ni ombi letu kwa leo tuishie hapa.
Jaji Ndunguru: Tumekuelewa tulitaka kupima stability ya shahidi, Jumatatu mtaweza kumaliza cross examination?
Katuga: Tutajitahidi Waheshimiwa majaji.
Jaji Ndunguru: Tunaomba mmalize cross examination Monday, kwasasa shauri linaahirishwa hadi Jumatatu.
Inapigwa High Coooouuuuurrrrttt
Majaji wanatoka, tukutane Monday.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 407.
Makam Mwenyekiti John Heche anaendelea kutoa ushahidi wake.
Mhe. Lissu: Taarifa ya EAC ilisema nini juu ya tarehe 29/10/2025???
Heche: Taarifa ya EAC ilisema uchaguzi wetu ulikuwa mzuri, huru na haki.
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji hiyo taarifa ya EAC kama ilizungumzia mauaji ya Oktoba 29, 2025??
Heche: Haikueleza jambo lolote baya wala mauaji wala uharibu wa mali yaani wanatofautiana hata na Tume ya Chande ambayo ilisema kulikuwa na mauaji na uharibifu wa moundombinu.
Mhe. Lissu: Nchi zinazounda EAC ni zipi?
Heche: Uganda, Kenya, Rwanda, Burundi, Congo, Sudan Kusini, Uganda, Somalia.
Mhe.Lissu: Waeleze majaji hali ya kidemokrasia ya nchi hizo.
Heche: Kwa nchi zote ukiitoa Kenya kidogo hali ya demokrasia ni mbaya sana, Uganda iko chini ya Museven kwa zaidi ya miaka 30, Rwanda iko chini ya Kagame na Uchaguzi wa mwaka jana alipata 98% walipishana kidogo tu na Samia aliyepata 97%
Mhe. Lissu: SADC walisemaje kuhusu uchaguzi wa mwaka jana
Heche: SADC wanaona uchaguzi wa Tanzania haukufikia viwango vya kidemokrasia kuendesha uchaguzi huru na haki, haukufikia viwango vya SADC ili Uchaguzi uitwe huru na haki.
Walizungumza pia kuhusu matatizo waliyoyapata siku ya uchaguzi ikiwemo kuzuiwa, ilivyotokana na curfew iliyotangazwa baada ya Maandamano siku ya uchaguzi.
Mhe. Lissu: Walisema nini kuhusu mauaji???
Heche: Walisikitishwa na matukio ya mauaji, matumizi makubwa sana ya nguvu ya vyombo vya dola yaliyojitokeza siku ya uchaguzi.
Mhe. Lissu: Taarifa za kikanda ni zipi waeleze majaji???
Heche: Thabo Mbeki Foundation
Mhe. Lissu: For the record, Thabo Mbeki ni nani ?
Heche: Rais wa Pili wa Afrika Kusini na amekuwa kiongozi wa ANC ambao ni rafiki wakubwa wa CCM.
Mhe. Lissu: Thabo Mbeki Foundation walisema nini kuhusu uchaguzi?
Heche: kutokana na ripoti za SADC na AU walizoziona na mapungufu makubwa yaliyobainishwa, Tanzania inakosa serikali halali iliyochaguliwa na wananchi. Serikali iliyoko madarakani imejengwa kwa nguvu (mabavu) na njia za udanganyifu.
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji Taarifa za Taasisi za Kimataifa:
Heche: Taarifa za EU, World Council of Churches, UN, Jumuiya ya Madola
Mhe. Lissu: Taarifa ya EU ilisema nini kuhusu uchaguzi?
Heche: Ililaani mauaji ya raia, ilitaka Serikali ifanye uchunguzi huru, waliohusika kuwajibika na kuchukuliwa hatua za kisheria
Mhe. Lissu: World Council of Churches walisemaje
Heche: Walilaani kuhusu mauaji na walisema kwamba Haki ya kuishi hutolewa na Mwenyezi Mungu ambayo haipaswi kuondolewa na mtu yeyote, walizungumzia kuwa Uchaguzi haukuwa na viwango vya kidemokrasia unaoruhusu haki na kukosekana kwa mizania inayoruhusu Uchaguzi kufanyika kwa haki na kwa usawa.
Mhe. Lissu: Taarifa ya UN ilisemaje?
Heche: Walizungumzia kuhusu Uchaguzi kuwa haukuwa Huru na wa Haki na uliwamnyima Wananchi haki yao ya kidemokrasia.
Walisema pia kuhusu kukamatwa kwa Viongozi wa upinzani na kubambikiwa kesi za uongo na kutaka wote waliobambikiwa kesi za uongo waachiwe.
Part 408 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
Mwenyekiti anasema there's no giving up the fight, you must stand up for your rights. Kesi imeahirishwa mpaka siku ya jumatatu ambapo cross examination itaanza Kwa shahidi namba 5 Mhe John Heche.
Walipoanza na wapinzani na Kanisa Katoliki, wahadhiri, madaktari na wengine wakakaa kimya. Walipowafuata wahadhiri na vyuo vyao, madaktari wakakaa kimya. Sasa wamewafuata madaktari, lakini wengine wetu bado tuko kimya.
Tusisubiri hadi watufikie. Uonevu ukinyamaziwa leo, kesho utagonga mlango wangu au wako, na huenda asiwepo wa kutusemea!
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 406.
Makam Mwenyekiti John Heche anaendelea kutoa ushahidi wake.
Mhe. Lissu: Hebu fafanua hilo la mauaji na vita vya majimaji?
Heche: Waheshimiwa Majaji nafahamu historia ya nchi hii na nafahamu hakuna mauaji yamewahi kufanyika kwa pamoja.
Taarifa ya Jaji Chande inasema Dar es salaam watu zaidi ya 100 na Mwanza watu 90 Arusha na Mbeya na kwa historia hiyo walikufa watu wengi sana katika siku iliyopaswa kuwa ya Uchaguzi.
Mhe. Lissu: Je kuna muhusika yoyote amewajibika kwa namna yoyote kutokana na mauaji hayo yote?
Heche: Kwa ufahamu wangu sina taarifa ya mtu yeyote kutoka Chombo chochote ambaye amewahi kuwajibika kwa mauaji ya kutisha kiasi hicho yaliyotokea kwa siku ambayo ilipaswa kuwa siku ya Uchaguzi.
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kwa ufahamu wako kuhusu kiongozi yeyote wa Serikali kuwajibika kwa mauaji hayo?
Heche: Hakuna kiongozi yoyote wa Serikali ambae amewahi kuwajibika kwa mauaji hayo makubwa.
Mhe. Lissu: Eleza kuhusu Jaji Chande kutaja kiongozi yeyote aliyetoa amri ya kuuwa watu wote hao?
Heche: Hakuna mahali kokote Jaji Chande alitaja kiongozi aliyetoa amri ya kuua watu wote hawa.
Mhe. Lissu: Je kuna mtu yeyote aliyekamatwa kwa kuhusika na kuuwa watu hao?
Heche: hakuna hata mmoja aliyekamatwa
Mhe. Lissu: Ufahamu wako kuhusu serikali kuuwa raia wake?
Heche: Hakuna uhalali wa Serikali kuuwa raia tena kwa namba kubwa kiasi hicho.
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji hoja ya kuahirisha Uchaguzi ingekuwaje kama ingekubaliwa?
Heche: Hiyo hoja ingekubaliwa maafa na mauaji hayo makubwa yasingetokea.
Mhe. Lissu: Jaji Mkuu Chande alisema kisababishi cha hayo machafuko ni nini?
Heche: Madai ya muda mrefu ya watanzania kutaka Katiba Mpya, Tume huru ya Uchaguzi, Rushwa na ufisadi, Ukosefu wa Ajira na watu kutekwa nyara na kupotezwa.
Mhe. Lissu: Alisema nini Chande kuhusu utekaji nyara na kupotezwa watu?
Heche: Alisema watu wanatekwa kwasababu za Kimapenzi, ushirikina na sababu za kibiashara.
Mhe. Lissu: Wimbi la Utekaji wa Viongozi umewataja wa Chadema na vyama vingine hili ulisemaje ulimtaja hadi Polepole?
Heche: Alisema wametekwa kwasababu za kisiasa.
Mhe. Lissu: Kwa akili yako tu ya kawaida kuhusu uwezekano wa mtu kujiteka mwenyewe?
Hilo swali lilekebishwe anasema Jaji.
Kuhusu taarifa ulizopata sema zingine?
Heche: Nilipata taarifa kutoka kwenye vyombo vya habari kwa kusoma na kuangalia, waangalizi wa Kimataifa, Taarifa za jumuiya za kimataifa na taasisi za jumuiya za kimataifa, Taasisi ya dini.
Mhe. Lissu: Eleza taarifa za kidini ulizozipata??
Heche: Shura ya maimamu na Kanisa Katoliki.
Mhe. Lissu: Elezea tarehe za hizo report???
Heche: Zilikuwa za Mwezi Novemba 2025.
Mhe. Lissu: Taarifa ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania ilisemaje???
Heche: Ilianza kwa kulaani kilichotokea Oktoba 29, ilihimiza uchunguzi huru wa Kimataifa, ililaani matumizi ya nguvu kupita kiasi katika kukabiliana na wananchi au waandamanaji, ilisema pia sio kila Maandamano ni Maandamano ya uhalifu, ilizungumzia wananchi kunyimwa haki yao ya kidomokrasia ya kuchagua kiongozi wanayemtaka tangu mwaka 2016.
Lakini pia ilizungumzia kuhusu hali ya kiusalama, kwamba wananchi wamekuwa wakiishi kwa hofu na kutekwa nyara na kupotezwa kwa watu bila hatua kuchukuliwa na kumekuwa na hofu kubwa miongoni mwa wananchi.
Mhe.Lissu: Shura ya Maimamu walisemaje??
Heche: Shura ya maimamu walilaani matukio ya mauaji, walieleza namna ambayo uchaguzi ulikosa sifa za uchaguzi, walilaani vyombo vya dola kutumia nguvu kuua raia wakati wa Uchaguzi.
Mhe. Lissu: Watajie majaji taarifa za waangalizi wa uchaguzi.???
Heche: Nilisoma taarifa za African Union, Taarifa ya waangalizi wa Uchaguzi ya SADC na ya East African Community.
Mhe. Lissu: Waeleze majaji taarifa zilitolewa tarehe gani???
Heche: Zote ni za Mwezi Novemba 2025.
Part 407 inaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 405
Mahakama inaanza majira saa tisa kasoro alasiri.
Majaji walishaingia, Mhe. Lissu yupo na Upande wa Jamhuri wapo.
Anasimama Nassoro Katuga anasema mchana huu hayupo Ajuaye na Job Mrema na sisi tuko tayari kuendelea.
Mshitakiwa Mheshima Tundu Lissu anasema yupo tayari kuendelea pia.
Shahidi no. 5, John Heche tayari alishapanda zake kizimbani hata kabla hajaitwa, hana muda wa kupoteza 😂
Jaji Ndunguru anamwambia Shahidi nakukumbusha kwamba upo chini ya kiapo.
Mhe. Lissu anasema nikumbushwe nilipoishia ili tuendelee.
Anakumbushwa.
Mhe. Lissu: Waeleze majaji uwepo wa jambo lingine mlilozungumzia kwenye hivyo vikao?
Heche: Kukomeshwa vitendo vya utekaji nyara, ubambikaji wa kesi za uongo kwa watu kwa ujumla ni kuupitia mfumo wote wa Haki jinai na kurudisha Demokrasia ya kweli.
Mhe. Lissu: Kuhusu ratiba ya mambo hayo mliyokuwa mnayazungumzia?
Heche: Katika mapendekezo yetu tulikuwa na roadmap ya namna ya kukwamua mchakato wa Katiba mpya na ratiba nzima ambayo ilisema mambo yote yangekamilika kabla ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa za mwaka 2024.
Mhe. Lissu: Mazungumzo hayo yaliishaje?
Heche: Wakati wote tulipokuwa tunazungumza tulipeleka kwa maandishi ratiba na mapendekezo yetu.
Wajumbe wa CCM walikuwa wanatusikiliza na wanabeba kwamba wanaenda kufanya consultation na Rais ambae aliteua hiyo timu kumueleza hayo tunayozungumza ili tuwe kwenye picha moja.
Kuna wakati Mh. MBOWE NA KINANA wameenda kumuona Rais kwa Pamoja kupeleka mazungumzo tuliyokuwa tumefanya kwenye kikao.
Makubaliano ilikuwa Mbowe na Kinana wafanye Press conference ya pamoja kuelezea walichokubaliana, mazungumzo yaliisha pale tuliposema tujibiwe kwa maandishi kuwa tuandikieni na nyie upande wa CCM na Serikali kuwa kati ya mapendekezo yetu yote yapi tumekubaliana.
Mhe. Lissu: Waliwajibu kwa njia gani?
Heche: Walitujibu kwa njia ya maandishi na kwenye majibu yao walisema kwamba wamekataa mambo yote tuliyokubaliana kwenye vikao hivyo vya Maridhano.
Mhe.Lissu: Hayo majibu waliyaleta lini?
Heche: Siwezi kukumbuka exactly tarehe lakini ilikuwa mwaka 2023 na sisi tuliendelea na ziara zetu kwenda kwa wananchi so mazungumzo yetu na CCM yakaishia hapo.
Mhe. Lissu: Siku ya Tarehe 29/10/2025 wewe ulikuwa wapi na kama ukishiriki kwenye kupiga kura?
Heche: Hiyo Tarehe 29/10 nilikuwa kituo cha Polisi Mtumba Dodoma ambapo nilikamatwa tangu tarehe 22/10 huo huo.
Nilipotoka Polisi nilipata taarifa nyingi kuhusiana na kilichotokea, watu kuuwawa kwa zaidi ya watu 518 na Mzee Joseph Warioba anasema watu waliouwawa ni wengi kuliko waliokufa kwenye vita ya Kagera.
Anasimama Katuga anasema sio kwamba napinga lakini hiyo habari ya Mzee Warioba ni Hearsay Evidence haipaswi kuchukuliwa.
Mhe. Lissu: Waheshimiwa Majaji kama hapingi amesimama kufanya nini? Pia kuna mambo yanasemwa kama ni sheria vile lakini sio sheria kabisa.
Hearsay Evidence inahitaji kuwa Corroborated na ushahidi mwingine, mimi nimebaki na mashahidi wengine watatu kwahiyo atulie tu na mwisho yeye ana nafasi ya kuja kufanya Cross Examination sasa si asubiri aje kumuuliza maswali shahidi.
Jaji Ndunguru: Haya tuendeleee.
Mhe. Lissu: Ahsante. Haya ulisemaje hapo?
Heche: Nilitaka kumalizia kwa kusema hakuna Serikali imewahi kuua watu wengi toka vita vya majimaji hadi leo, hii ndo Serikali imeua watu wengi sana.
Part 406 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
FAM Aliumia sana kushindwa uchanguzi na tundu lissu imagine ukoga imekuwa mbali au posta mahakani imekuwa mbali kuliko kwenda kuvuka maji huyu jamaa anaroho mbaya sana����
DAY - 5 GEREZA IRINGA
Jana tarehe 10 September 2026 nimekamilisha ziara ya kuwatembelea wanachama wa CHADEMA wanaoshikikiwa magerezani baada ya kushitakiwa kwa makosa ya Ugaidi kwa kutembekea wanachama watatu Gereza la Mkoa wa Iringa.
Wanachama hao, walioshitakiwa kwa Economic P. I No. 16453/2026 ni Ndugu Aqhudy Aqnay Qhyqhalay, Rahim Hussein na Helman Beatus Sambala wote wanatoka wilaya ya Mafinga.
Wanachama hawa, kama ilivyokuwa kwa wanachama wengine walikamatwa na kuhojiwa kwa makosa ya uchochezi mtandaoni, baadaye wanadai kuletewa makaratasi mengi na kuambiwa wasaini ili ndugu zao wawadhamini bila kusoma kilichoandikwa.
Baada ya kusign nyaraka hizo, wakashangaa hawadhaminiwi tena badala yake wakapelekwa Mahakamani ambako walipandishwa kizimbani.
Wanachama hawa wanafanya ujasiliamali wa studio, wanarecord nyimbo , kupiga picha kwenye sherehe na matukio maalumu, kwenye ukamataji wao, nimeambiwa na vifaa vyao vyote vilichukuliwa.
Leo kesi yao inatajwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Iringa.
Pamoja nao alishitakiwa mwanachama ambaye nimejulishwa ni GreenGuard anayejulikana kwa jina la Ambi Daudi Mwaisomba, kutoka Mafinga pia, naye eti kashitakiwa kwa makosa ya ugaidi.
Mchakato wa Katiba usioshirikisha kikamilifu makundi yote ya kijamii hauzai utulivu — unazaa mzozo mpya. Kama ilivyotokea huko Misri mwaka 2012 #KatibaMpya
JOHN MNYIKA KAMALIZA KESI YA LISSU KWA MANENO CHINI YA 50
Katibu Mkuu John Mnyika ametumika ku-crack open na ku-summarize utetezi wote wa case ya uhaini dhidi ya M’kiti @TunduALissu kwa maneno chini ya 50.
Tundu Lissu: Umesema ni mashitaka ya uongo. Waeleze Majaji kwanini?
Mnyika @jjmnyika: Umetuhumiwa kwa uhaini kwa kusema maneno ya kawaida ya kisiasa. Wanasema uliitisha mkutano wakati hukuitisha wewe niliitisha mimi pamoja na sekretarieti. Unatuhumiwa kwa kuchapisha maneno hayo, wakati hukuyachapisha wewe, yaliyochapishwa yalichapishwa na waandishi wa habari.
Unatuhumiwa kuwa na nia ya kutenda kosa hilo, wakati ulichokifanya ni kutekeleza maazimio ya vikao halali vya Chama. Na swali linabaki: kwa nini utuhumiwe wewe peke yako, na si viongozi wengine waliokuwa sehemu ya maamuzi hayo?
#FreeTunduLissu #SamiaMustGo #TanzaniaMassacre