@RevenueTra Naomba mtoe list ya vyombo ambavyo mnasema ni vya biashara ili watu wa kawaida tujue na tusinunue. Mtu ukinunua hata kirikuu kwa binafsi na kulipa kila kodi stahiki unakamatwa mnasema cha biashara? Toeni orodha ya vyombo ambavyo kwenu ni biashara by default.
@dna_bongo@godbless_lema Nafikiri ukisoma comments utaelewa zaidi juu ya OIC na Vatican. Ni dhahiri huyo kiongozi unaupotosha umma na kutengeneza chuki na udini kati yetu watanzania. Kwenye vitabu vya dini tumeonywa kuhusu manabii wa uongo na hili ni moja wapo.
@qwaryvicent2 Tuachage unafki jamani, wananchi wanaumia sana.. Hivi ingekuwa ndo mwanao anajisomea hapo chini na kuuza karanga usiku tena ungependezwa..?? Miaka 60 na hatuna stable power supply.
@TBConlineTZ Miradi tunawapa wachina lakini watendaji wakuu ni sisi watanzania tunaajiriwa kufanya kazi zote wenyewe. Bora tuzipe kampuni mama Miradi hii, kwani wao wakiwa consultants kama ilivyo sasa itakuwaje? Tuthamini kampuni zetu na tuziwezeshe. Mbona zipo nyingi tu jamani?!
@amina7yusuph@CloudsMediaLive Mimi binafsi sioni logic yoyote hapo, Bado ni kitu kile kile anarithi mali sababu anakuwa na mali za baba ila hatotangazwa au kusomwa kwenye wosia tu na anakuwa amewahi kugawiwa mali kuliko wengine.. anyway, dini ni imani na iheshimiwe na kila mtu kwa nafasi yake.
@amina7yusuph@CloudsMediaLive Ukiacha Imani, sisi sote ni binadamu dada yangu. Kwahiyo lazima ubinadamu utumike sio kusema huyo mtoto hana haki wakati hakutaka mwenyewe kuja hapa duniani, kaletwa na wazazi wawili walioamua kujamiiana, kitendo ambacho hata wanandoa wanafanya so he/she has every right.
@CloudsMediaLive Wazazi majukumu yao ni kukusomesha hadi kuhitimu elimu ya juu baada ya hapo hawana tena majukumu juu ya mtoto na hasa ambaye ameshafikisha miaka 18.
@HKigwangalla Nchi itasonga mbele pale ambapo tutakuwa na requirements za kuwa mbunge. Inasikitisha kuona madereva wenu serikalini wana elimu kuliko huyo mbunge anaemuendesha. Vyeo hivyo ni kazi kama kazi zingine, kuwe na requirements kushika madaraka.
@eastafricatv Watanzania sasa hivi sio wajinga. Pia sisi tumesoma nje huko mlipo na tunajua wanavyofanya kazi. So please continue na mnachofanya, ipo siku just one fine day tukichoshwa vya kutosha itajulikana tu.
@eastafricatv Kodi ni sawa lakini sio mara mbili mbili.. mfanyakazi wa kawaida tu unalipa kodi ndipo unawekewa pesa kwenye bank au simu, bado mfanyakazi huyo huyo anakatwa tena anapohamisha au kutuma pesa. Tunategemewa jamani sio kisa nyie hamkatwi ndo muone ni sawa tu kila kitu..
@earadiofm@SuluhuSamia@bobbymongi@Evansbukuku@ChrisIncc Kodi ni nyingi sana.. ukipata mshahara unakatwa kodi, ukitoa hela benki unatozwa kodi, kutuma unatozwa kodi, na kutoa unatozwa na serikali hiyo hiyo.. bado kuna tozo kwenye kodi za nyumba sasa wanataka tuponee wapi na tujiendeleza kimaisha..?!