Hon. Judge Joseph Sinde Warioba asante sana kwa utumishi wako na muongozo wako!, Mungu akupe maisha marefu sana.
Uhuru una maana gani ikiwa unafaida kwa wachache na una mateso kwa wengi?
WE CELEBRATE YOU!, hawa ndo wazee sasa sio mkusanyiko wa mbogamboga ule.
"Mnabeba Silaha nzito Akili zenu zisiwe nyepesi, jeshi ni wito sio muujiza wa kupuliza GESI"🎵🎼
"Hamheshimu muhimili nyie makatili hamna maadili hamstahili injili labda ALBADILI tena Alfajiri, wanaofaidika boss zenu sio nyie askari wa chini kwa posho ndogo mnatumwa mtupige sasa kwanini?"🎵🎼
"Yani unamuua anaepambania kesho bora ya mwanao, huku unamlinda anaekuibia na ukistaafu hakupi MAFAO"🎵🎼
"Watoto wao wana MALI wanaendesha bugati , felari, we askari NJAA KALI unadaiwa kwa mangi SUKARI na huna GARI unagombania MWENDOKASI ni hatari, tukidai mabasi unapiga RISASI we ndio MUASI.".🎵🎼
Ebana Home boi katuletea goma la kuelekea kilele cha mapambano 29.10. Hili goma linalia sana mtaani mchana huu.
Asante sana Msanii wetu wananchi @Roma_Mkatoliki sisi hatuna cha kukulipa zaidi ya kukupa maua yako masta.
MAMAE TUKIKOMBOA HII NCHI OKTOBA 29 FIKILIA ROMA AJE KUPAFOMU HILI GOMA AFU SUB WANAKUJA "MAKOMBOLELO" OYAAA HII NCHI IKIKOMBOLEWA ITAKUWA TAMU SANA.
REPOST 200
#MO29
#MaandamanoOktoba29
#OktobaTunaToka
#SiriNiNamba
#TUTAKUWEPO🫵😎
🚮🚮 Absolute crap!
Police in #Tanzania finally admit holding the podcaster duo Wachokonozi and want to charge them with the Cybercrime offences
The state is using this repressive law since 2015 to instill fear and abuse our freedom of expression!
FYI This law was championed by @JMakamba - we will never forget 👊🏽
#FreeWachokonozi
ARUSHA: Jeshi la Polisi limesema linawashikilia Vijana wawili wanaojulikana kwa jina la Wachokonozi ambao ni Joseph Mrindoko (37) na Jackson Kabalo (32) kwa tuhuma za matumizi mabaya ya Mtandao, ambao awali taarifa zilizosambaa Mtandaoni zilidaiwa wamechukuliwa na Watu Wasiojulikana waliokuwa na silaha
Taarifa ya Polisi ya Juni 21, 2025 imesema Watuhumiwa hao walikamatwa na Jeshi la Polisi mnamo Juni 20, 2025
Aidha, katika taarifa hiyo Jeshi la Polisi limeonya watumiaji wa Mitandao ya Kijamii kuacha kusambaza taarifa ambazo hawana uhakika nazo zinazoleta taharuki katika Jamii, hasa zile za kuzusha kuwa Watuhumiwa wamekamatwa na Watu Wasiojulikana jambo ambalo sio la kweli.
Soma https://t.co/0QBuRZrFn7
#JamiiForums #JamiiAfrica #Uwajibikaji #Accountability #FreedomofSpeech
Vijana wawili Joseph Mrindoko na Jackson Kabalo wanaounda kundi la "Wachokonozi" wamevamiwa na watu wenye silaha waliojitambulisha kuwa ni Askari Polisi wakiwa nyumbani kwao maeneo ya Maji ya Chai, wilayani Arumeru mkoani Arusha.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, watu hao walikuja na gari aina ya Landcruzer wakiwa wamevalia kiraia na wamebeba silaha za moto. Walipoingia ndani waliwaweka vijana hao chini ya ulinzi lakini walipoambiwa watoe vitambulisho kuthibitisha kama wao ni Polisi kweli walikataa.
Walifanya upekuzi kwenye nyumba hiyo bila kufuata taratibu. Walipoambiwa waitiwe mjumbe wa serikali ya mtaa ili awe shahidi walikataa, na kusema wasifundishwe kazi. Katika upekuzi huo wamechukua vifaa mbalimbali ikiwemo camera, computer, microphones, tape revorder, na nyaraka mbalimbali zilizokuwemo, kisha kuwafunga pingu "Wachokonozi" na kuondoka nao.
Majirani walipouliza wanawapeleka kituo gani cha Polisi, watu hao hawakujibu bali waliondoa gari kwa mwendo mkali. Ndugu wameenda kituo cha Polisi Maji ya Chai lakini hawajawakuta. Hadi sasa, haijafahamika wamepelekwa kituo gani lakini ndugu wanaendelea kufuatilia.
Familia za "Wachokonozi" zinaomba tuwasaidie kupaza sauti ili ndugu zao wapatikane wakiwa hai. Wanaomba waliowakamata wasiwaue wala kuwapoteza bali kama wanatuhumiwa kwa makosa yoyote basi wawapeleke mahakamani kwa hatua za sheria.!
Vijana Wawili JOSEPH MRINDOKO Na JACKSON KABALO Wanaounda Kundi La “WACHOKONOZI” Wamevamiwa Na Watu Wenye Silaha Waliojitambulisha Kuwa Ni Askari Polisi Wakiwa Nyumbani Kwao Maeneo Ya Maji Ya Chai, Wilayani Arumeru Mkoani Arusha. #FreeWachokonozi
Naombeni RT 200🤝