🇨🇦 is deeply alarmed and saddened by the brutal killing of Ali Mohamed Kibao, and strongly supports President Samia Suluhu Hassan’s urgent call for an investigation. Canada supports the right to freedom of expression, including peaceful assembly within a peaceful and stable 🇹🇿.
Unapanga maisha yako na kazi zako Watanzania wenzio wamekaa sehemu wanapanga namna ya kukuua na kuwaacha wanao bila baba, wao wakirudi majumbani kwao wanapokewa na familia kwamba wametoka kazini, kumbe wametoka kuua baba wa familia nyingine. SO SAD 😭 REST EASY MZEE ALI KIBAO
Both parties are capable of violence(kwa sources hizi)
Pursuit of power makes/turns men into animals.
Hii CCM vs CHADEMA divide inaacha taifa nyuma.
How can we build and have the political maturity ya kuweka taifa mbele? Mwl employed the single party democratic system.
“Baba yake mkubwa MARHUM ALI MOHAMED KIBAO ni Hemed bin Jumaa bin Hemed ambaye amewahi Kuhudumu kama Mufti Mkuu wa Tanzania”. Ameandika @ExMayorUbungo
Huzuni kubwa ni kua Bakwata hawajatoa Tamko lolote mpaka sasa.
Ila CDM drama za nini msibani ?
Yule bwanyenye Mayai mpaka anataga kuzichapa ndo ana uchungu sana kuliko ndugu wa marehemu..
Busara za Freeman zimehitajika na zikafanya kazi.
Septemba 6,2024 zilisambaa taarifa kwenye mitandao ya kijamii ikieleza kuwa majira ya jioni maeneo ya Tegeta jijini Dar es Salaam mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina la Ali Mohammed Kibao , akiwa safarini na basi la Tashrif alichukuliwa na kushushwa toka kwenye basi hilo na watu ambao hawakuweza kujulikana majina https://t.co/qb7oRdKg7d nadra sana matukio ya namna hii kuripotiwa nchini Tanzania.
Mapema asubuhi ya Jumapili Septemba 08, 2024 Taifa liliamshwa na taarifa ya majonzi baada ya kuonekana kwa mwili wa mwanaume mmoja maeneo ya Ununio jijini Dar es Salaam ambapo baada ya taratibu za utambuzi mwili huo ulibainika kuwa ni Ali Mohammed Kibao.
Baada ya taarifa hizo za kuhuzunisha, wadau mbalimbali wakiwemo wanasiasa, viongozi wa serikali, wadau wa haki za binadamu pamoja na taasisi mbalimbali za serikali na binafsi zimepaza sauti kueleza kusikitishwa na tukio hilo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii ameeleza kusikitishwa na tukio hilo lilipolekea kupoteza maisha ya Kibao huku akiagiza vyombo vinavyohusika na uchunguzi kufanyia kazi suala hilo na kumpelekea taarifa ya kina kuhusu tukio hilo na mengine ya aina hiyo.
Katika kurasa hizo Rais Dkt. @SuluhuSamia ameandika
"Kwa masikitiko makubwa nimepokea taarifa ya mauaji ya kiongozi wa CHADEMA Bwana Mohamed Ali Kibao. Natoa pole kwa viongozi wa chama hicho, familia ya Mzee Kibao, ndugu, jamaa na marafiki.
Nimeagiza vyombo vya uchunguzi kuniletea taarifa ya kina kuhusu tukio hili baya kabisa na mengine ya namna hii haraka. Nchi yetu ni ya kidemokrasia na kila raia ana Haki ya kuishi. Serikali ninayoiongoza haivumilii vitendo vya kikatili vya namna hii."
Kwa upande wake Katibu wa Halmshauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi,Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa Ndugu Amos Makalla ameeleza kusitishwa na tukio hilo na pia ametoa pole kufuatia kifo cha ndugu Kibao.
Akizungumza Kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika leo wilayani Simanjiro mkoani Manyara, Makalla amekaririwa akisema
"Nimeona kwenye Vyombo vya Habari kuanzia asubuhi mpaka sasa nitoe pole kwa Chama cha Chadema kwa kumpoteza mmoja wa Wajumbe wa Sektarieti bwana Ali Mohamed Kibao, nimekuwa nikifuatilia sisi ni vyama vya siasa linapokuja suala la ubinadamu Chama unaweka pembeni, nawapa pole kwa msiba"
"Mimi niombe Jeshi la Polisi likatimize wajibu la kuendelea na uchunguzi wa jambo huo , na katika hili sisi ni binadamu ,utu na ndio mana nimesimama hapa kutoa pole kwa niaba ya Chama cha Mapinduzi"
Nao chama cha ACT Wazalendo, saa chache baada ya kufuatia taarifa za kifo cha Ali Mohammed Kibao, kilitoa taarifa za kulaani tukio hilo kupita taarifa kwa umma iliyotolewa na Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani kutoka chama hiko Ndg. Dahlia Majid Hassan yenye kichwa cha habari kinachosema TUNALAANI KUTEKWA NA KUUAWA KWA MZEE ALLY KIBAO.
Taarifa hiyo kwa kina inasema
"Chama cha ACT Wazalendo kimeguswa na kulaani vikali taarifa za kutekwa na kuuawa kwa aliyekuwa Mjumbe wa Sekretarieti ya CHADEMA Taifa Ndg. Ally Mohammed Kibao kinachohusisha vyombo vya ulinzi na usalama vya nchi.
Tumepokea kwa masikitiko makubwa kusikia mwili wa Mzee Ally Kibao umekutwa eneo la UNUNIO baada ya taarifa za kutekwa na watu wenye silaha akiwa katika basi la abiria la Kampuni ya TASHRIF lenye Na. T.343 EES linalofanya safari zake kutoka Dar kwenda Tanga juzi tarehe 06 Septemba 2024.
Tukio hili linaenda kuongeza idadi ya matukio ya utekaji, utesaji na mauaji ya raia nchini ambayo yanahusishwa moja kwa moja na vyombo vya ulinzi na usalama. Kuhusishwa kwa vyombo hivyo kwenye matukio ya utekaji na mauaji sio tu kunajaza hofu juu ya usalama na amani bali kunafuta imani kidogo iliyopo ya wananchi juu ya vyombo hivyo na kuongeza uhasama dhidi ya dola.
.
“Niwahakikishie waombolezaji wote hususan familia, kama Serikali hatutaliacha liende hivi hivi [mauaji ya Kibao], maelekezo ya Mheshimiwa Rais yameshaanza kutekelezwa, hatua zitachukuliwa kwa wale wote watakaobainika kuhusika.” – Hamad Masauni, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kwenye msiba wa Mjumbe wa Sekretarieti ya CHADEMA, Ally Kibao
Bi Mkubwa @SuluhuSamia Ikupendeze Sharifa atoe mkeka wa dharura ikigusa wale walioapa watalinda Usalama wa uraia na mali zao ili wajitathmini.
isifike tu mahala na wewe Mama ukatamani kuwa IJP kama mwafulani.
Politics is a dirty, bloody dirty game.
Pursuit for power and/or wealth turns men into animals.
A country turning into bloodshed ni jambo rahisi sana,no matter how tight and efficient the security organs are.
All it takes is dirrty politics igniting the fire.
Baba yetu hakutaka makuu wala umaarufu. Alidedicate maisha yake kwa wanawe na wajukuu zake, hayo kwake yeye ndo ilikuwa fahari yake.
Ni mtu wa msimamo, mbishi sana 😃 lakini mtu wa misimamo asiyeyumbishwa kirahisi.
Aliishi kwa principles zake na sasa wememuuwa, kitatili kabisa, kwa misimamo hiyohiyo. Haya ndo maisha tunayotaka kweli kama Watanzania?
Sisi hatukudhani hata siku moja kama jambo hili linaweza kutotokea. Mtu unaona habari, unadhani hayo ni ya wengine tu hayawezi kukufika na wewe. Haya, leo yametufika.
Baba yetu sisi alikuwa shujaa wetu. Lakini, kama damu yake, iliyomwagwa kwa uovu wa kupitukia, ndio itakuwa chanzo cha majibu na mabadiliko au kuepusha familia hata moja nyingine kupitia haya tunayoyapitia sisi, basi atakuwa shujaa maradufu.
Amenifunza mengi sana, mengine sikuyaelwa na bado mpaka sasa kuna mengine nayaelewa kadri siku zinavyokwenda.
Aliwagusa wengi sana, na hakukata malipo yoyote kutoka kwao, kuanzia ndugu wa karibu, na mbali na mpaka watu asiwojua.
Halafu kuna watu wakaamua, sio wamteke tu, bali wamtese, waharibu mwili wake, kisha wamtupe kama mbwa… kuna mwanadamu anayestahili kufanyiwa unyama kiasi hiki kweli?
Niachie hapa kwa sasa…
Kwa masikitiko makubwa nimepokea taarifa ya mauaji ya kiongozi wa CHADEMA Bwana Mohamed Ali Kibao. Natoa pole kwa viongozi wa chama hicho, familia ya Mzee Kibao, ndugu, jamaa na marafiki.
Nimeagiza vyombo vya uchunguzi kuniletea taarifa ya kina kuhusu tukio hili baya kabisa na mengine ya namna hii haraka. Nchi yetu ni ya kidemokrasia na kila raia ana Haki ya kuishi. Serikali ninayoiongoza haivumilii vitendo vya kikatili vya namna hii.