‼️MAFEDHULI WAMEPANIC‼️
Mdau huyu amenikumbusha ule mpango wa kulisha sumu upo palepale na wamepanga kuutekeleza muda wowote kuanzia sasa ila sasa focus ni Lissu na Nchimbi huku Heche wanamwinda nje na hatakiwi kabisa kukaa mwenyewe
Muda wote @HecheJohn hakikisha umezungukwa na watu na wananchi MLINDENI!
Haya si matani au maneno tu - na mkithubutu kumsogelea Lissu gerezani hata usiku wa manane tutajua - komeni!
Nchimbi najua atawaweza mko naye kwenye mfumo na ana taarifa zenu!
Acheni kupanic nyie wauaji! Muda wenu umefika!
#FreeTunduLissu #TutaelewanaTu
Mtuhumiwa hawezi kujichunguza mwenyewe.
Tangu mwanzo tulisema tume ya Jaji Chande haiwezi kuleta ukweli, iliundwa kuficha ukweli na kusafisha watuhumiwa.
Ndio maana ile tume ilikuja na hoja za ajabu kwamba:
1. Watu wanatekwa kwasababu za kimapenzi
2. Kwasababu za ushirikina
3.kwasababu za kibishara.
Kuna familia zinasema na zina ushahidi wa ndugu zai kutekwa na kupotelea vituo vya polisi, lakini Chande hakusema hilo popote.
Kama ilivyokua tume ya Chande.
Hiki kinacholazimishwa kitaharibu na kuwagawa Watanzania zaidi.
Jaji wa Museveni ambapo wapinzani wanauwawa, wengine wako jela na wengine wamekimbia Nchi.. labda atawapa uzoefu zaidi wa namna ya kuumiza watu lakini sio kutafuta ukweli.
Hivi sasa kuna wimbi kubwa la mashambulizi ya maneno dhidi ya Makamu wa Rais, mheshimiwa Emmanuel Nchimbi. Wimbi hilo limeibuka kufuatia hotuba yake kwa watetezi wa haki za binadamu. Katika hotuba hiyo, Mhe. Nchimbi alisisitiza umuhimu wa Watanzania kupambania Katiba mpya, kauli ambayo kimsingi si ngeni ndani ya mjadala wa kitaifa, bali imekuwa sehemu ya ajenda ya muda mrefu ya mageuzi ya kisiasa nchini.
Hata hivyo, kilichozua mjadala mkali si wito wa Katiba mpya wenyewe, bali tafsiri iliyopotoshwa ya baadhi ya kauli zake, hasa pale aliposema kuwa “Katiba ya sasa inampa Rais madaraka yasiyo na maana.” Kauli hii imechukuliwa na baadhi ya wadau kama ishara ya kumkosoa au hata kumsaliti Rais, Samia Suluhu Hassan. Lakini je, huo ndio ukweli?
NCHIMBI ALIMAANISHA NINI HASA?
Kwa mtazamo wa kiintelijensia, ni muhimu kuchambua kauli katika muktadha wake halisi. Nchimbi hakuwa akimdhalilisha Rais wala kupunguza mamlaka ya kikatiba ya urais, bali alikuwa akitoa hoja ya kitaasisi: kwamba Katiba ya sasa imejikita katika mfumo unaokusanya madaraka makubwa mno kwa mtu mmoja.
Hii si hoja mpya, ni mjadala uliowahi kujitokeza mara nyingi katika historia ya siasa za Tanzania.
Kwa kusema “madaraka yasiyo na maana,” tafsiri sahihi si kwamba madaraka hayo hayana thamani, bali yanaweza kuwa yasiyodhibitiwa ipasavyo (unchecked powers), jambo linaloweza kuleta hatari kwa utawala bora na uwajibikaji wa taasisi. Kwa lugha nyingine, Nchimbi alikuwa akisisitiza haja ya kuweka mizani ya madaraka (checks and balances) ili kuimarisha demokrasia na kuondoa uwezekano wa matumizi mabaya ya mamlaka.
JE, HII NI KINYUME NA RAIS SAMIA?
Kinyume chake, Nchimbi alieleza wazi kuwa wazo la Katiba mpya ni sehemu ya maono ya Rais Samia mwenyewe. Hii ina maana kuwa hotuba yake haikuwa ya kupingana na Rais, bali ya kuunga mkono ajenda ya mageuzi ambayo tayari imeashiriwa na uongozi wa juu wa nchi.
Kumshtumu Nchimbi kwa “usaliti” ni ama kutokuelewa kwa kina hoja yake, au ni jitihada za makusudi za kupotosha umma. Kiintelijensia, hali hii huashiria uwepo wa makundi yenye hofu ya mabadiliko hasa wale wanaonufaika na mfumo uliopo wa madaraka usio na mizania.
NAFASI YA NCHIMBI KIKATIBA
Ni muhimu pia kuzingatia kwamba Nchimbi yuko hatua moja tu kutoka kushika madaraka ya juu kabisa ya nchi endapo kutatokea dharura. Hivyo basi, kauli yake ina uzito wa kipekee kwani ni mtu anayeelewa uzito wa madaraka hayo na athari zake kwa taifa. Kwa mantiki hiyo, kauli yake inaweza kutafsiriwa kama tahadhari ya kiuongozi na sauti ya mtu anayejua hatari ya mfumo usio na uwiano wa madaraka. Hii ni ishara ya ukomavu wa kisiasa, si udhaifu.
NANI ANAPOTOSHA NA KWA AJENDA GANI?
Swali ambalo kila mtu anapaswa kujiuliza ni hili, “ni nani wanaopotosha kauli za Nchimbi, na kwa faida ya nani?” Uchambuzi unaonesha uwezekano wa makundi matatu. Kwanza ni kundi la Wanaonufaika na mfumo uliopo ambao wanaona Katiba mpya kama tishio kwa maslahi yao binafsi au ya kisiasa. Pili ni Wanasiasa wa taharuki, wanaotumia propaganda ili kujijengea mtaji wa kisiasa kwa kuibua migogoro isiyokuwepo. Kundi la tatu ni “CHAWA” wa kisiasa: kundi la watu wanaotafuta kujipendekeza kwa viongozi kwa kupotosha ukweli na kueneza hofu. Makundi haya yanaweza kuwa na lengo la kuzima mjadala wa Katiba mpya kwa kugeuza hoja ya msingi kuwa mgogoro wa kisiasa binafsi.
Katika mazingira haya, ni wazi kuwa Mhe. Nchimbi hajafanya kosa la kisiasa, bali ameibua mjadala wa msingi kuhusu mustakabali wa taifa. Huu ni mjadala unaohitaji ujasiri, si lawama.
Ni muhimu kwa viongozi wenye maono kama Nchimbi kutotikiswa na kelele za upotoshaji. Taifa linahitaji mjadala wa wazi, wa kina, na wa ujenzi, sio propaganda.
Kwa hiyo, ujumbe wa mwisho ni huu, Makamu wa Rais Nchimbi asitikiswe na “chawa” wa kisiasa wasioitakia mema Tanzania. Historia inaonesha kuwa mageuzi ya kweli huanza kwa sauti chache jasiri zinazothubutu kusema ukweli, hata pale ambapo ukweli huo haupendwi na wengi.
Serikali ya dikteta Museven ilitoa wanajeshi waje kuuwa raia wa Tanganyika Oktoba 29. Leo imempa Samia Jaji kuchunguza waliolipwa waandamane na kuuwa raia. Huu ujinga unaudhi sana, ila ni ishara zilezile za maji kulowana na mwisho wa kuvuja kwa pakacha. Mungu ni mwema!
Huyu jamaa anazunguka kila kona kutaka kummaliza @HecheJohn
Polisi wanamjua vizuri sana huyu kijana wa Abdul ambaye anawazimu kichwani kutokana na Roho nyingi za Watanganyika
Ukimwangalia machoni huyu muuaji unaona kabisa ameshakubuhu kwenye haya maukatili na ujinga wake, hana hofu wala haya anachowaza ni kuua watu.
Wanaojua ndugu za huyu mpumbavu it time Share details zao tuwaulize wanajua huyu mshenzi kazi yake ni nini?
Ndugu za watu kama hawa wote tunatakiwa kuongea nao, wote mpaka marafiki zake tunatakiwa kuongea nao na kuwauliza wanajua huyu mshenzi ameua watu wangapi?
Mahakama ya Uganda imetumika kuwatesa wapinzani wa dikteta Museven kwa kuwanyima dhamana, matibabu, na fair trial. Samia ameomba Jaji kutoka mahakama hiyo aje amchunguze kwa mauwaji aliyofanya Oktoba 29. Kwanini Samia anadhani Watanzania wote wana elimu kadha wa kadha kama yeye?
Tanganyika AMKA 🔥👊🏽
Vijana usiku huu wako bize wanasambaza vipeperushi kuamsha watanganyiks tupambane!
Kila mtu apambane anavyoweza! Hakuna kuwapa muda wa kupumua hawa wauaji mafedhuli!
Hadi tupate Haki 💪🏽🔥
#TutaelewanaTu#JusticeForMO29
Nchimbi on record kagoma kujiuzulu - kawa preempt wasije wakaleta barua kama ya Ndugai bure 👊🏽😁
Kaa humuhumu @nchimbie pambana hadi mwisho hakuna kujiuzulu wala kujitoa 💥
Bi Msumi presha inapanda ama inashuka? Na watanganyika ndani ya CCM amkeni! Mnaendeshwaje na akili za Kizimkazi?
#TutaelewanaTu
Katika Nchi ambayo uhusiano wa serikali na wananchi ni wa kikatiba.
Uhusiano wa Mwananchi kama muajiri na serikali kama muajiriwa huwezi kuona upuuzi kama huu.
Nchi hii wananachi wanachukuliwa kama watumwa na watawala kama watwana au wamiliki wa watumwa.
Nimeona utetezi wa jeshi la polisi kwenye upuuzi huu, inathibitisha kiwango cha dharau walichonacho hawa watu dhidi ya raia.
Mwananchi huyu masikini amelima alizeti imekaa shambani miezi minne, mbegu amenunua mwenyewe, pengine kwa jembe la mkono na mvua kidogo akavuna.
Hapo ilipo hiyo alizeti kuanzia mbegu imelipiwa kodi, akivuna tu kodi… huko anakopeleka kuna Mageti ya mazao kila kona..
Baada ya kuuza akinunua sukari kuna kodi , kiberiti, Sabuni na chumvi vyote kodi za kulipa askari huyo mshahara.
Hata kama huyo bwana amekosea:
Sheria gani inampa mamlaka askari kuchukua mzigo wake na kutupa mtaroni?
PGO namba ngapi inamwambia askari mtu akifanya kosa kama hilo unaharibu mali yake kwa kuirusha kwenye mtaro unaopitisha maji machafu tena mzigo wa chakula?
Kwanini usimkamate na kufuata utaratibu wa kisheria?
Kwa utetezi huu wa polisi kwa askari hao ni uthibitisho wa namna serikali hii ya kidkteta inavyowaona wananchi…
Haishangazi kama waliua mamia kwa maelfu ya watu na wanaona ni kawaida itakua kutupa mzigo mtaroni?
Watanzania mnapaswa kubadilika wale mnaofikiri hayawahusu kwasababu nyie sio huyo bwana, watawafikia kwa njia nyingine.
Kama alivyowahi kusema Martin Luther king kwa watu weusi kule Marekani.
“We must learn to live together as brothers or perish together as fools“
Lazima tujifunze kuishi pamoja kama ndugu, kwa kuteteana, kusaidia na kulindana au tuangamie pamoja kama wajinga.
TAARIFA KAMILI YA KIJANA ALIEPIGWA NA POLISI KWENYE MSAFARA WA MWENGE.
Tukio hili limetokea Kijiji cha Nkololo Kata ya NKOLOLO Wilaya ya BARIADI, Kijana mwendesha bodaboda aliepakia alizeti kwenye pikipiki yake aliingia barabarani kutoka barabara za mitaa inamaana alikuwa HAJUI kinachoendea njia Kuu alivyotokeza ghafla Polisi walimsimamisha kwa Kasi ikawa ngumu kusimama kwa haraka kama unavyojua vyombo vya Moto.
Baada ya kusimama Polisi na mgambo wakaanza kumpiga hapo mchukua video amechukuwa wakati Kijana huyu ameshapigwa, Baada ya kipigo wakamwaga alizeti zake mtaroni kama inavyoonekana kwenye video.
Kisa cha yote haya ni MSAFARA wa MWENGE kama unavyoona mwisho wa video hii inaonekana MSAFARA wa MWENGE unapita.
Baada ya hapo Kijana huyu alikamatwa Mpaka sasa yupo kituo cha Polisi Nkololo.
Kwa SASA nimempata MTU aliechukuwa video ya tukio nikamuomba video za ziada amenitumia.
Baada ya tukio hili kusambaza mtandaoni Polisi wamemfuata mtu aliechukuwa video na kusema watamkomesha kwa SASA Kijana aliechukuwa video yupo katika mashaka makubwa, anahitaji Masada wetu aweze kuondoka kijijini hapo kuokoa maisha yake.
Amenipatia namba yake kwaajili ya Msada wa dharula nimeshindwa kuiweka hapa Namba kwaajili ya usalama wake, kama kuna MTU anahitaji kumpa msaada wa haraka aje inbox.
Pia tunaomba wanasheria wafuatilie ili dereva BODABODA aachiliwe huru
Naomba tupate sauti Vijana hawa wawe salama.
Twaha Mwaipaya mtetezi wa haki za binadamu
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tanzania Bara, John Heche, amedai kuwa mahakama na magereza vinatumika kama nyenzo za kuwakandamiza na kuwadhoofisha wapinzani wa kisiasa, akidai waliopaswa kushindana na chama chake kupitia siasa sasa wamehamishia mapambano hayo mahakamani.
Heche ametoa kauli hiyo nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Shinyanga, baada ya kutajwa kwa mara ya pili kwa kesi zinazowakabili wanachama 17 wa CHADEMA, akisema mwenendo wa mashauri hayo unaibua maswali kuhusu matumizi ya mfumo wa haki dhidi ya wapinzani.
Amemtaka Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kutafakari mwenendo wa mashitaka yanayowakabili wanachama wa CHADEMA, akidai kuwa ofisi hiyo imeendelea kufungua kesi nyingi za uhaini na ugaidi dhidi ya viongozi na wanachama wa chama hicho.
Heche pia amelalamikia utaratibu wa vyombo vya dola wa kuwakamata watuhumiwa na kuwaweka mahabusu kabla ya kukamilisha uchunguzi na ukusanyaji wa ushahidi, akisema hali hiyo inawanyima haki ya msingi na kuwasababishia mateso kabla ya kesi kusikilizwa.
Aidha, amedai uwepo mkubwa wa askari polisi ndani na nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Shinyanga uliwazuia wananchi wengi kuingia na kufuatilia mwenendo wa kesi hiyo, jambo alilosema linapunguza uwazi wa usikilizwaji wa mashauri ya umma.
Awali, watuhumiwa 17 wanaokabiliwa na mashitaka yanayohusiana na ugaidi walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Shinyanga kwa ajili ya kutajwa kwa mara ya pili kwa kesi zao.
Katika mashauri hayo, wanachama hao wa CHADEMA, akiwemo Katibu wa Kanda ya Serengeti, Jackson Mnyawami, wanakabiliwa na makosa tofauti ambapo watuhumiwa watatu wanadaiwa kupanga kufanya kosa la ugaidi, huku watuhumiwa wengine 14 wakishtakiwa kwa kula njama za kutenda kosa hilo.
Kesi hizo zilitajwa kwa mara ya kwanza Julai 24, 2026 na kutajwa tena Agosti 4, 2026 mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Glory Mwakihaba.
Upande wa mashtaka uliwakilishwa na mawakili Leonard Kiwango, Joseph Mwakasege na Nyamnyaga Magoti, huku upande wa utetezi ukiwakilishwa na mawakili Peter Kibatala, Gaston Garubindi, Alex Masaba na Gloria Ulomy.
Mahakama iliahirisha mashauri hayo na kuyapanga kutajwa tena Agosti 17, 2026.
Misaada sio kupungua tuu, ITAISHA KABISA.
Nyie si mlijifanya ni KISIWA kwamba mnaweza kuuwa watu wenu na dunia ikawachekea tuu.
Kila siku wananchi wakitangaza Maandamano mnaanza kuteka watu na kuwaita MAGAIDI na kuwafunga MAGEREZANI. Mnafikiri dunia haioni.
Nchi ambayo IMEJAA MAGAIDI unataka ikopeshwe pesa watalipaje? Mnafanya haya na jeshi lenu la polisi mkijua mnaisaidia nchi kumbe ndio mnaizika kabisa.
Kenya wapo uchumi wa kati kitambo kila siku wanapokea MIKOPO mikubwa sana kwasababu ya DEMOKRASIA yao.
Wewe unatupanga eti kwasababu tumekuwa kiuchumi ndiomaana hatupewi mikopo, ENDELEA kuuwa watu, kuteka watu, kufunga wakosoaji wako na uone kama HATA HIZO BILIONI 500 UNAZOPATA SASA KAMA UTAPATA.
Hii nchi unaenda kuizika kabisa wewe MALAYA tupo hapa.
TUTAKUWEPO🫵🏾😎
Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, John Heche, amesema mazingira ya siasa nchini yamebadilika na kutofautiana na enzi za viongozi wa upinzani kama Freeman Mbowe, Agustino Mrema, Profesa Ibrahim Lipumba na Dk. Wilbrod Slaa, akidai kuwa kwa sasa badala ya ushindani wa hoja kumekuwepo matukio ya utekaji wa wanasiasa na wanachama wa vyama vya siasa.
Akizungumza leo Jumatatu, Agosti 3, 2026, katika kikao na viongozi wa Chadema Wilaya ya Tarime, Heche amesema hata viongozi na wanachama wa chama hicho wamekuwa wakikumbwa na matukio ya kutekwa bila Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoa kauli ya kuyalaani.
"Ametekwa hapa aliyekuwa mgombea udiwani, mjumbe wa Mkutano Mkuu na diwani wao. Hata Humphrey Polepole, mmeshawahi kusikia wakitoa taarifa kulaani matukio hayo?" amehoji Heche.
Amesema tofauti na ilivyokuwa kipindi cha nyuma ambapo kulikuwa na ushindani wa kisiasa baina ya CCM na viongozi wa upinzani akiwemo Agustino Mrema, Freeman Mbowe, Profesa Ibrahim Lipumba na Dk. Wilbrod Slaa, kwa sasa mazingira hayo hayapo.
Heche ametoa kauli hiyo akimjibu Katibu wa NEC, Organaizeshen Paul Matiko Chacha, aliyedai kuwa Chadema ya sasa haina nguvu za upinzani kama ilivyokuwa kipindi cha viongozi waliotajwa.
Akijibu madai hayo, Heche amesema Chadema hakijioni tena kama chama cha upinzani bali ni chama kikuu cha siasa nchini.
"Sisi sio chama cha upinzani," alisema.
Pia alimjibu Chacha kuhusu madai kwamba alimdhalilisha Waziri wa zamani na mwanasiasa mkongwe, Stephen Wasira, akisema hakutoa matusi bali alieleza mtazamo wake kuhusu umri wa mwanasiasa huyo.
"Nilisema Wasira ni mzee wetu, amechoka, anasinzia kwenye vikao vya msingi. Sasa hapo nimemtukana nini? Kusema anasinzia? Mimi nimesema yule mzee sasa hivi ni muda wa kukaa na wajukuu," amenukuliwa akisema.
Aidha, Heche amemkosoa Chacha kwa kauli yake kwamba hakuna upinzani wa aina ya zamani, akisema wakati viongozi kama Mbowe, Mrema, Lipumba na Dk. Slaa walipokuwa wakifanya siasa, CCM ya wakati huo ilikuwa ikijibu hoja za wapinzani badala ya kutumia vitendo vya ukandamizaji.
@MwijakuBurton Tukiwambia hii Serikali ya ccm itoke haiwezi kuiongoza hii nchi tuna maanisha.
Ujinga wa kutokuwa na akili wa bodi ya wadhamini ni kwa sbb mifumo ya nchi hii ni mibovu kupindukia kila sekta na hayo ndo matokeo yake.
Serikali ya ccm inatakiwa kutoka madarakani haraka iwezekanavyo.
VIDEO:
Katibu Mkuu wa @ChademaTZ2 John Mnyika ametoa wito kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) kutumia hekima na utaratibu uliotumika kufuta kesi ya ugaidi iliyokuwa inamkabili aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe utumike kwa Mwenyekiti wa sasa wa chama hicho Tundu Lissu ambaye anashtakiwa kwa uhaini.
Mnyika amesema hayo leo Agosti 3, 2026 akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam huku akitoa wito kwa wananchi kwenda kuhudhuria kesi ya Lissu itakayoendelea Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam kuanzia Agosti 10 mwaka huu.